Friday 31 October 2014

Re: [wanabidii] Polisi akamatwa kwa kumkata mfanyakazi wake vidole vinne

Tunahitaji kutoa huduma za ushauri kwa waajili wa wafanya kazi wa ndani.
--------------------------------------------
On Fri, 10/31/14, Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com> wrote:

Subject: [wanabidii] Polisi akamatwa kwa kumkata mfanyakazi wake vidole vinne
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Friday, October 31, 2014, 8:39 AM

ASKARI POLISI ASHIKIRIWA KWA KUMKATA MFANYAKAZI
WAKE VIDOLE VINNE KWA PANGA KWA MADAI YA KUMWIBIA DEKI YA
VIDEO NYUMBANI KWAKE.
JESHI
la Polisi mkoani Mwanza linamshikilia askari wake WP Fatuma
wa Kituo cha Polisi Igogo wilayani Nyamagana kwa kosa la
kumjeruhi mtumishi wake wa ndani kwa mkumkata vidole vyake
vinne vya mkono wa kulia kwa panga, akimtuhumu kumwibia Deki
ya Video nyumbani kwake. 

Tukio
hilo la kujeruhiwa kijana Steven Magessa (18), lilitokea
Oktoba 20 mwaka huu katika kijiji cha Magange Mugumu
wilayani Serengeti mkoani Mara nyumbani kwao kijana huyo
aliyekuwa amekimbilia huko baada ya kudaiwa kumwibia mwajili
wake nyumbani eneo la Igogo.

Akizungumza
na G.SENGO BLOG kijana huyo alieleza kuwa kufanya kazi kwa
askari huyo kulikuja 
mara
baada ya askari huyo kumfuata kijijini na kumuomba ridhaa ya
wazazi wa kijana huyo kuambatana naye jijini Mwanza ili
kumsaidia kazi za nyumbani ambapo walikubaliana malipo ya
kiasi cha Sh 50,000/= kila mwezi jambo ambalo askari huyo
alilikiuka na kushindwa kulitekeleza kwa muda wa miezi sita
bila kumlipa mshahara.

"Nilipoona
hajanilipa mshahara wangu kwa muda wa miezi sita huku kila
ni kimwambia ananijia juu na kunitukana matusi basi
nilimuomba ruhusa ya kwenda kijijini Oktoba 15 mwaka huu
kumuona mama yangu mzazi aliyekuwa anaumwa ili kupata nafasi
ya kurudi nyumbani" alisema.
Ni
kidole gumba tu kilicho nusurika kukatwa nacho ilikuwa ni
kama bahatikusalia kwani kilikwanyuliwa huku vingine vinne
vikifyekwa na panga mkono wa kulia wa Steven Magessa.
Steven
alieleza kuwa wakati akiwa kijijini askari huyo (Mwajili
wake) alikuwa akimpigia simu kumtaka arudi Mwanza kuendelea
na kazi na kudai kuwa atamlipa malimbikizo ya mshahara wake
kiasi cha Sh 300,000/= zilizokuwa kama deni, Steven
alikubali ombi hilo kwa kuomba atumiwe nauli na pesa kidogo
ya kumwachia mama yake, jambo ambalo askari huyo alikaa
kimya bila majibu.

"Siku ya Oktoba 20 mwaka huu majira ya saa 4:00 asubuhi
alifika kijijini akiwa na askari watatu kwenye gari la
Polisi (Difenda) wa Kituo cha Mugumu na kudai kuwa nipo
chini ya ulinzi kisha kunifunga pingu, akidai kuwa
nilimwibia Deki ya Video na kutoroka nyumbani kwake,
walinipandisha kwenye Difenda kunipeleka kituoni "
alisema.

Kijana huyo alieleza kuwa baada ya kufikishwa kituoni Mugumu
askari huyo na wenzake walianza kumuhoji huku wakimpa maneno
ya vitisho, kijana huyo alipokataa kuwa hakuiba wala
kutoroka, Sajenti Fatuma aliamuru kijana huyo kuvulishwa
shati alilovaa na kisha akafungwa usoni na kuombwa anyooshe
mkono mezani ili apewe 'Sapraizi'.


"Sekunde chache nilihisi kitu kikali kimenipitia kwenye
vidole vyangu vinne vya mkono wa kulia na kufuatiwa na
maumivu makali, niliusogeza mkono wangu mdomoni kuupoza kwa
kuupuliza ndipo nilipo gundua kuwa nimekatwa kabisa vidole
vyangu vinne vya mkono wangu wa kulia ikibakia dole gumba
tu" kijana Steven alisimulia kwa uchungu.

"Niliangua kilio kutokana na maumizu na sijui vidole
vyangu hadi sasa sijui vikowapi, askari wenzake baada ya
kuona nimetokwa na damu nyingi walimshauri anipeleke
hospitali ya Wilaya ya Mugumu ili nipatiwe matibabu kabla ya
kuondoka kuja Mwanza,"alisisitiza.


Steven alisema baada ya kupatiwa matibabu, tulienda kupanda
basi ili kuja Mwanza kwa madai kuwa amenifungulia kesi ya
wizi wa Deki ya Video na tuliopfika alinipeleka kituo cha
Polisi Kati Nyamagana na kuniweka Mahabusu akinituhumu wizi,
lakini nilipochukuliwa maelezo nilikana tuhuma za wizi na
kueleza ukweli wangu ili kupata msaada.

Huku taarifa zingine kutoka ndani ya jeshi zilizopatikana
zilidai kuwa askari huyo alikusudia kufanya ukatili huo
kutokana na udanganyifu ambao alifanya kwa uongozi wake
akiomba kupatiwa silaha (SMG) kwa ajili ya kuitumia kwenye
kazi za nje lakini lengo ikiwa ni kwenda na silaha hiyo kwa
ajili ya kumkamata na kumtishia kijana huyo, jambo ambalo
uongozi ulimgomea.

JESHI LA POLISI LINASEMAJE?

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza (RPC), Valentino
Mlowola, jana ofisini kwake amethibitisha kuwepo kwa taarifa
za tukio hilo na kueleza kuwa tayari Jeshi hilo limechukuwa
hatua madhubuti hatua ya awali ikiwa ni kumshikilia askari
huyo kwa kufanya ukatili huo kwa kuvunja sheria na
kujichukulia sheria mkononi kumjeruhi kijana huyo.

Mlowola alisema pamoja na kijana huyo awali kufunguliwa
jarada la kutuhumiwa kufanya kosa la wizi (Jinai) na kudaiwa
kutorokea kijijini kwao, bado askari huyo alitakiwa kufuata
mfumo wa kiutawala na kisheria uliopo kushughulikia suala
hilo badala ya kuamua kujichukulia maamuzi ya kumwadhibu
mtuhumiwa kabla ya uthibitisho wa mashitaka yaliyokuwa
yamefungulia.

"Nilipopokea taarifa hizi kwa mashangao na masikitiko
makubwa na zimenisitua sana, si kitendo cha kiungwana hata
kidogo kwa mtu ambaye anatakiwa kufuata taratibu za mfumo wa
utawala na sheria katika utekelezaji wa kushughulikia kero
na matatizo ya jamii, alitakiwa kutumia busara kwani tayari
aliishamfungulia jarada la kumtuhumu kumwibia ikizingatiwa
naye ni mzazi wa watoto watano ni lazima anaujua
uchungu,"alisema. 

Kamanda Mlowola alieleza kufatia ukatili huo kufanywa na
askari wake ameunda timu ya kikosi cha askari kwenda hadi
kijijini Magange wilayani Serengeti mkoani Mara ili kufanya
uchunguzi wa tukio hili ikiwa ni pamoja na kufanya mahojiano
na familia, wananchi wa kijiji hicho kisha Hospitali ya
Wilaya ya Serengeti alipopatiwa matibabu ya awali.

"Ili tupate ukweli wa jambo hili tumeunda timu hiyo, kwani
kijana Steven tumemhoji ametueleza jinsi askari Fatuma
alichomfanyia na kudai hakumwibia, lakini askri wetu pia
amehojiwa awali amedai hakufanya kitendo hicho bali wananchi
ndo walimfanyia ukatili huo hivyo ni mkanganyiko lakini
ukweli utapatikana tu japo kuwa tukio hili halikufanyika
Mwanza"alisisitiza.

Mlowola alisema kwamba tayari tunamshikiria askari huyu na
kumfungulia jarada la uchunguzi kwa taratibu za kijeshi na
ikibainika kutenda kosa hilo tutumfukuza kazi na kumfikisha
katika vyombo vya sheria ili kuchukuliwa hatua zaidi
kulingana na kosa alilofanya, lakini pia kijana Steven naye
anashikiriwa kwa tuhuma alizonazo za wizi kufatia jarada
lililopo.

"Hatuwezi kuendelea kucheka na kufumbia macho kitendo hiki
ni jambo ambalo linamgusa kila mtu hata mimi ni mzazi
ukiachana na utumishi wangu wa umma, ntahakikisha jambo hili
nalishughulikia kwa umakini na kutoa taarifa kwa umma ili
pia kueleza wananchi kuwa tukio hili limefanywa na mtumishi
kama mtu si Taasisi ya Jeshi la Polisi na ahidi kutenda haki
kwenye hili,"alisisitiza. 

Wito wangu kwa wananchi ni kuacha kujichukulia sheria
mkononi na kuwaadhibu watuhumiwa mbalimbali kabla ya
kuthibitika kwa makosa na tuhuma hizo, lakini wazingatie
kufuata taratibu za kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria ili
kushughulikia matatizo yao nawaomba waendelee kutoa
ushirikiana na kufuata mfumo uliopo badala ya kujichukulia
sheria mkononi.

GSengo blog: ASKARI POLISI AMKATA VIDOLE
VINNE MFANYAKAZI WAKE KWA PANGA AKIMTUHUMU KWA KUMWIBIA DEKI
YA VIDEO.



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment