Lucas ukitaka isomwe weka picha ya gazeti la udaku juu chini bandika hii la hutusomi
On Oct 9, 2014 6:24 AM, "'lucas haule' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
-- Nimeipenda na nita i print kisha naiweka katika njia na mitini.
--------------------------------------------
On Thu, 10/9/14, 'Bart Mkinga' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: [wanabidii] TUSHIRIKIANE ILI KUPATA KATIBA HALALI
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, October 9, 2014, 2:02 PM
Bunge Maalum la Katiba chini ya
Mwenyekiti wake Samwel Sita limehitimisha kazi yake ya
kuandaa katiba itakayopelekwa kwa wananchi kwaajili ya
kupigiwa kura. Zoezi hilo lili lilihitimishwa kwa kupigiwa
kura na wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kwa namna ambayo
haijawahi kushuhudiwa hapa nchini wala Taifa jingine lolote
hapa Duniani. Baada ya kuwa na mashaka makubwa ya
kutopatikana kwa theluthi mbili kutoka upande wa Zanzibar,
Mwenyekiti alibuni njia mpya ya upatikanaji akidi ya
theluthi mbili kutoka pande zote mbili za Mwungano. Hatimaye
wajumbe walitangaziwa kuwa akidi amepatikana, jambo ambalo
liliwafanya wajumbe wa Bunge la katiba waliokuwepo ukumbuni
kuonesha furaha yao ambayo huenda ilikuwa ni vigumu sana
kuielezea kwa maneno. Walio wengi waliionesha kwa kucheza na
kushangilia.
Lakini
kwenye huu mchakato uliotengeneza hii katiba
inayopendekezwa, kuna mambo ya msingi ya
kujiuliza:Uhalali wa Katiba unatokana na
nini?Je, katiba inayopendekezwa ni
halali?Wajumbe wa Bunge la Katiba na viongozi wao,
wanaelewa utofauti wa katiba na ushindani wakati wa
uchaguzi?Ni nani mwenye haki ya kufurahia
kupatikana kwa katiba nzuri inayopendekezwa, ni waandaaji au
wananchi?Tunajua kwa nini mataifa mbalimbali huweka
hitaji la theluthi mbili katika kupitisha katiba lakini
huweka asilimia hamsini au ushindi wa uwingi tu wa kura bila
ya kujali ni asilimia ngapi kwenye uchaguzi?
UHALALI WA KATIBA HUTOKANA NA
NINI?
Nilimsikia
mara kadhaa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba akisema
kuwa atawashangaa Watanzania kama
hawataikubali katiba hiyo kutokana na mambo mazuri yaliyomo
ndani yake. Na jana pia nilikatishwa tamaa zaidi na
Mheshimiwa Rais ambaye alitumia muda mwingi sana kuelezea
mambo mazuri yaliyopo ndani ya katiba
inayopendekezwa.
Kuna
kitu cha msingi sana katika demokrasia mnapofanya uamuzi.
Katika mfumo wa kidemokrasi unaheshimu mamlaka ya umma,
hakuna kitu muhimu kama kitu kilichoamuliwa kuwa
'halali'. Na uhalali hautokani na ubora au uzuri
bali hutokana na uhalali wa mchakato wa ushirikishwaji. Kama
lengo letu lingekuwa kupata tu
katiba iliyo nzuri bila ya kuzingatia 'uhalali'
sidhani kama kungekuwa na haja ya kuunda Tume ya Kukusanya
maoni wala kusingekuwa na haja ya kuwa na Bunge Maalum la
Katiba au hata upigiaji kura katiba inayopendekezwa.
Tungepata katiba iliyo nzuri zaidi kama tungewatafuta
wanasheria wazuri kabisa ndani na nje ya nchi, wakajifungia
mahali, wakachambua katiba mbalimbali Duniani, wakafanya
utafiti wao binafsi, na baadaye wakatuletea Watanzania na
kutueleza kuwa hii ndiyo katiba mpya. Na huenda katiba hiyo
ingekuwa bora kuliko katiba ya nchi yoyote ile Duniani
lakini nina uhakika isingekuwa katiba halali.
Nina
hakika watanzania walichokuwa wanataka siyo katiba nzuri tu
bali muhimu zaidi walitaka iwe 'halali'. Na
ikumbukwe pia uhalali wa kitu hautokani na sheria pekee
yake. Kuna nchi ziliwahi kutawaliwa na viongozi madikteta na
wauaji lakini katika nchi hizo hata walipokuwa wanawaua watu
wao ovyo walikuwa wakitumia sheria. Hata makaburu kule
Afrika Kusini wakati wa utawala wa kibaguzi walikuwa
wakiwakamata Waafrika na kuwafungulia mashtaka ya kukiuka
sheria za kibaguzi. Kwa hiyo walikuwa wakitumia sheria. Hata
Yesu alihukumiwa kuuawa kwa kutumia sheria. Hapa
tunachotakiwa kujiuliza, mtu anaposema kuwa mchakato wa
upatikanaji wa katiba inayopendekezwa ni halali kwa sababu
umefuata sheria, Je, sheria yenyewe halali? Tutambue kuwa
uhalali ni zaidi ya sheria maana hata sheria yenyewe inaweza
kuwa sheria halali au sheria ya kibaguzi au sheria
gandamizi. Sisi sheria yetu ya mabadiliko ya katiba ilikuwa
halali? Kwangu mimi sheria ile haikuwa halali maana
haikulenga kuufanya mchakato wa upatikanaji wa katiba
usihodhiwe na makundi fulani, na hasa Bunge la Jamhuri ya
Mwungano, na wanasiasa na vyama vya siasa.
KATIBA INAYOPENDEKEZWA NI
HALALI?
Katiba
inayopendekezwa na Bunge Maalum la katiba inaweza kuwa ni
nzuri lakini siyo
halali. Wanaoipigie debe ikiwa ni pamoja na
Mheshimiwa Rais, wameelezea vizuri sana uzuri wa katiba hiyo
lakini hawajaelezea ni kwa namna gani katiba hiyo ni halali.
Katiba inayopendekezwa siyo halali kwa sababu mchakato wake,
kuanzia sheria iliyotumika kuitengeneza haikuwa
halali.
Katiba
ya wananchi ni lazima itengenezwe na wananchi wenyewe na
wala kusiwe na kundi la kuhodhi mchakato wake. Katika
mchakato wa utengenezaji wa katiba ilistahili kuondoa dalili
zozote zile za kuonesha kundi fulani ndilo lenye mamlaka ya
kuandika katiba kwaajili ya watu wengine. Tangu awali
ilitakiwa kuyatambua makundi ambayo yatabanwa zaidi na
katiba mpya. Kundi mojawapo kubwa ilikuwa ni wabunge wa
Bunge la Jamhuri ya Mwungano. Katiba mpya tulitaka idhibiti
ununuaji wa madaraka na uwakilishi kwa njia ya rushwa wakati
wa uchaguzi. Malalamiko mengi ya rushwa yamekuwa wakati wa
uchaguzi yakihusisha wagombea wa nafasi za ubunge na
mawakala wao. Kundi la wabunge ambamo ndani yake kuna wengi
wanajitambua kuwa nafasi zao wamekuwa wakizipata kwa njia ya
rushwa hawawezi kuwa ni watu sahihi wa kutunga katiba
itakayodhibiti rushwa wakati wa uchaguzi.
Wananchi
wengi wamekuwa wakilalamikia upeo na uwezo mdogo wa baadhi
ya wabunge kutokana na elimu zao kuwa ndogo kupindukia.
Itawezekana vipi wabunge ambao ni darasa la pili, la nne au
la saba wapitishe katiba inayotamka kuwa hitaji la chini la
elimu ya mtu anayetaka kuwa mbunge ni kidato cha nne? Hivyo
wabunge wa Bunge la Mwungano walistahili kuwakilishwa kwenye
Bunge Maalum la katiba kama taasisi nyingine lakini siyo
kila mbunge kuwa mjumbe na hivyo kuwa na maamuzi ya mwisho
juu ya Katiba inayopendekezwa. Kama Bunge la Jamhuri ya
Mwungano wa Tanzania
wangewakilishwa na wajumbe wachache kama taasisi nyingine,
kungekuwa na uwakilishi mpana zaidi wa wananchi kuliko
kulifanya Bunge la Jamhuri ya Mwungano kuhodhi mchakato wa
katiba.
Jambo
la pili la kujiuliza ni kuwa kulikuwa na ulazima gani Rais
kuteua wajumbe waliopendekezwa badala ya taasisi na makundi
mbalimbali kuwateua moja kwa moja?
DHAMIRA CHAFU HAIZAI KITU
HALALI
Uhalali
wa kitu kwanza hutokana na dhamira safi na wala hautokani na
uzuri wa kitu. Ningependa kuwalizeni - Mathalani nyumbani
kwako ulikuwa na upungufu wa visu na ulikuwa unahitaji sana
kisu kizuri chanye
makali lakini bahati mbaya huna uwezo wa kukipata. Siku
moja jambazi mmoja akaenda kutafuta kisu chenye makali sana
huku akiwa na dhamira kuwa akija nyumbani kwako akutoe uhai,
na baada ya hapo atoweke na mali zako. Lakini usiku aliokuja
akiwa anafikiria kuwa wewe upo pekee yako, akakukuta upo na
majirani waliokuja kukufariji kutokana na msiba wa ndugu
yako uliotokea kijijini kwenu. Jambazi alipoingia akawakuta
watu wengi ambao hataweza kukabiliana nao, hivyo naye
akajifanya ni mmoja wa waombolezaji. Baadaye yule jambazi
akagundua wapishi hawana visu vizuri vya kukatia nyama, naye
akatoa kisu chake ambacho alikichukua kwaajili ya kuja
kufanyia ujambazi. Wote mkafurahi maana tatizo la kisu
limekwisha. Kisu cha jambazi kinaonekana ni kizuri,
kimetatua tatizo lakini kisu hiki ni haramu kutoka na
dhamira mbaya ya aliyekuwa amekileta. JAMBO BAYA LIKIFANYIKA
KWA NIA NJEMA MUNGU HULITAKATIFUZA LAKINI JAMBO JEMA
LIKIFANYIKA KWA NIA MBAYA MUNGU
HULINAJISISHA.
Wale
waliofuatilia vizuri hotuba ya Mheshimiwa Rais Kikwete
watakuwa walimsikia Rais akisema kuwa alipotaka kuanzisha
mchakato wa uandaji wa katiba mpya, CCM haikutaka lakini
akachukua maamuzi yake. Nadhani kwaajili ya kumheshimu Rais,
CCM waliamua kumkubalia lakini miyoyo yao haikuridhia. Kuna
mengi yaliyotokea, na kwa kiasi kikubwa ndiyo
yaliyochelewesha upatikanaji wa katiba mpya, ukijiuliza
huelewi kwa nini mchakato umeenda kwa namna ulivyoenda.
Jambo lililodhahiri ni kuwa CCM japo walishindwa kumkatalia
Mheshimiwa Rais
lakini waliamua kuchukua njia nyingine kuhakikisha katiba
mpya haipatikani, na hilo lingewezekana kwa kuhodhi mchakato
wa upatikanaji wa Katiba. Mahali pekee ambapo waliona
wanaweza kuhodhi bila shida ni kuhakikisha Wabunge wa Bunge
la Jamhuri ya Mwungano ndiyo wanaokuwa na maamuzi makubwa
kuhusu katiba mpya, wakitambua kuwa ndani ya Bunge la
Jamhuri ya Mwungano, wabunge wa CCM ni zaidi ya 75%. Wabunge
hawa wa CCM nia yao kubwa haikuonekana kutengeneza katiba
mpya bali ilikuwa kuzuia kupatikana kwa katiba mpya. Dhamira
hiyo inaonekana wazi kwenye Katiba mpya
inayopendekezwa.
Mambo
ambayo wananchi wengi waliyaona ni muhimu kwenye katiba mpya
ni pamoja na:Kupunguza
madaraka ya Rais katika uteuzi. Kwenye hili wananchi wengi
wanaona kuwa uteuzi wa Rais kwa nafasi fulani, japo ni
nafasi muhimu sana kwa maisha yao ya kila siku lakini
wanaoteuliwa wanapewa kama zawadi maana baadhi yao
hawaonekani kuwa na uwezo wa kuzimudu kazi zao. Lakini pia
kudhibiti uteuzi wa Rais kungesaidia wateule hawa kufanya
kazi kwa kujiamini zaidi kuliko pengine kufanya kazi kwa
lengo la kumfurahisha aliyewateua. Pia kuna ukweli kuwa
ikitokea bahati mbaya mkampata Rais dikteta ni vigumu sana
kuweza kumdhibiti Rais ikiwa wasimamizi wa ofisi zote kubwa
za umma ni wateule wakeWananchi walitaka kuona katiba
ambayo ina miongozi mikali kwenye mambo ya kudhibiti rushwa
maana wananchi wengi wanaamini hili ni tatizo kubwa kwa nchi
yetu kwa sasa, na linahitaji
kudhibitiwa kwa nguvu zoteWananchi walitaka kuona nchi
inakuwa na dira. Dira hiyo ielezwe na tunu zetu kama Taifa.
Sababu kubwa ya kuwekwa tunu hizo ni kwa vile watu wengi
wanaamini kuwa pamoja na katiba yetu inazungumzia usawa wa
binadamu lakini kiuhalisia inaonekana kuna Watanzania
wengine na hasa viongozi na matajiri, wao ni binadamu zaidi
kuliko wengine. Kutambua tunu za Taifa kungesaidia kuundwa
kwa sheria kali kwa watakaokiuka au kutenda kinyume na yale
ambayo Taifa limeyaweka kama mambo makuu ambayo Taifa
linaamini.
Wajumbe waliobakia Bungeni
wameyaondoa mambo hayo ambayo yalichangiwa na wananchi walio
wengi na badala yake kumekuwa na majigambo sana kuwa katiba
inayopendekezwa imetambua haki za makundi mbalimbali kama
vile wafugaji, wakulima, walemavu, wasanii, n.k. Kwangu mimi
haya yanayotajwa ni sawa na mtu ambaye ana paka wake ambaye
ana njaa, na paka huyu wakati Bwana wake anakula naye
anataka apande juu ya meza ili apate kushiba. Bwana wake
anachukua mfupa anaurusha nje, paka anaufuata mfupi nje, na
kisha Bwana wake anafunga mlango. Paka alirushiwa mfupa nje
alidhani kilio chake cha njaa kimesikika kwa Bwana wake
kumbe Bwana wake alikuwa na nia ya kumwondoa ndani ya nyumba
asimsumbue tena. Paka atalamba mfupi na kisha kuendelea na
njaa yake.
Ukiwa
na katiba inayotambua na kuzingatia haki na usawa wa watu
wote na mahitaji yao yanayoendana na hali zao, tayari
mlemavu naye atakuwemo, mkulima yumo, mfanyabiashara yumo,
mvuvi,
mfugaji, na wengine wote. Tunatajiwa haki za makundi lakini
hatuambiwi ni wapi ndani ya katiba kiu yetu ya kuona
wanaoteuliwa wanapata nafasi hizo kwa uwezo wao na siyo
sababu nyingine. Maana hawa wateule katika baadhi ya maeneo
wamekuwa ni kikwazo kwa maendeleo ya wananchi au kutokana na
maadili yao au uwezo wao mdogo. Ndani ya katiba hatuambiwi
ni wapi tumedhibiti kikatiba kuhakikisha watu hawapati
madaraka kwa kutumia pesa au vyeo vya wazazi na ndugu zao.
Ndani ya katiba hatuambiwi ni wapi tumedhibiti uwezekano wa
mikataba mibovu, n.k.
MTU
SAFI
UKIGUNDUA MWENZIO AMEFANYA KOSA AU HILA KWA MAKUSUDI NA
WEWE UKAUNGANA NAYE, WEWE NI MHALIFU ZAIDI. MTU MWADILIFU
ANATAKIWA KUSIMAMA KIDETE NA KUSEMA KUWA ULICHOFANYA SIYO
SAHIHI. TUNAPOFANYA HIVYO KWA DHAMIRA SAFI NA SIYO KWA
MASLAHI YAKO AU KIKUNDI FIULANI, KAULI HIYO ITAKUWA NI
TAKATIFU.
Napenda
kuwaambia watanzania wenzangu kuwa ni aheri katiba
isipatikane kuliko kukubali watu wengine kutumia sheria
zisizo halali kuhalalisha katiba isiyo halali.
WABUNGE WA CCM
WANAELEWA UTOFAUTI WA KUPATA KATIBA YA WOTE NA USHINDANI WA
UCHAGUZI?
Ukifuatilia
toka mwanzo wakati wa utengenezaji wa sheria ya kusimamia
mchakato wa kupata katiba mpya, ni dhahiri kuwa mchakato
uligeuzwa kuwa ni ushindani kati ya CCM na CHADEMA, na
baadaye kati ya CCM na UKAWA. Hili lilikuwa ni kosa kubwa
sana. Ni ukweli huo ndiyo uliowafanya wabunge wa CCM
kushangilia sana baada
ya kuelezwa kuwa kura zilizopigwa kwa fax, email na sms
zimefanya akidi ya theluthi mbili kufikiwa. Furaha ile
ilikuwa ni kushangilia kuwa CCM imewashinda UKAWA kama vile
kulikuwa na kiti kinachogombaniwa kati ya CCM na
UKAWA.
Ni
fikra hizo ndizo zilizomfanya Mwenyekiti wa Bunge Maalum la
Katiba hata kubuni upigaji kura ambao haujawahi kutokea nchi
yoyote katika sayari hii. Yote hiyo ilifanyika ili CCM ipate
ushindi dhidi ya UKAWA. Wajumbe hawa na Mwenyekiti wao
hawakujua kuwa ilistahili Watanzania wote tufurahie kuwa
tumepata katiba mpya
ambayo ina 'ownership' ya watanzania wote kama
mchakato wake ungekuwa umelenga kuwashirikisha wananchi wote
na siyo wanasiasa kuhodhi mchakato mzima. Leo tuna katiba
inayopendekezwa na CCM ambayo ownership yake ipo kwa CCM.
Hawa ndiyo watakaohitajika kuwashawishi wananchi waikubali
na huku UKAWA na sisi wengine tunaoamini kuwa haitakuwa
katiba halali tukiwashawishi wananchi waikatae kwa kuwa
katiba iliyotengenezwa imehusisha kundi dogo ambalo lina
msimamo unaofana kisera. KWENYE JAMBO HILI NI LAZIMA
WATANZANIA TUSIMAME NA TUTAMKE KUWA TUNATAKA KATIBA YETU
AMBAYO SISI WENYEWE TUTAIPIGIE DEBE, TUTAIFANYIA KAMPENI KWA
WATANZANIA WENZETU. HATUTAKI UUNDWAJI WA KATIBA MPYA
UBADILIKE NA KUWA NI MASHINDANO KATI YA CCM NA
UKAWA.
KWA NINI MATAIFA MBALIMBALI HUWEKA
HITAJI LA THELUTHI MBILI KWENYE KATIBA?
Katiba
husimamia masuala yote kwa ujumla ya kila mwananchi na ndiyo
msingi wa sheria zote za nchi. Msingi huu ni lazima uwe
imara, mzuri lakini muhimu zaidi uwe halali. Katika nchi
ambazo watu hutanguliza dhamira njema, viongozi
wanaosimamia upatikanaji wa katiba huwa hawataki washinde
bali huwa wanataka kujiridhisha kuwa angalao watu walio
wengi kabisa kama si wote, wanaafiki katiba walioitengeneza
ili wailinde, waitetee na wajivunie. Na ili hayo yafanyike
ni lazima kuwe na 'ownership'. Hii katiba
inayopendekezwa ikipitishwa ni lazima kutakuwa na kundi
kubwa (significant number) ambalo haliwezi kujivunia na
huenda wasiilinde katiba ambayo imetengenezwa na wajumbe wa
CCM na kisha kupelekwa kwa wananchi. Katiba hailindwi na
Polisi, Usalama wa Taifa, mahakama au Jeshi bali hulindwa na
wananchi wenyewe. Katiba mbovu na isyopendwa itazaa sheria
mbovu na zisizopendwa. WATANZANIA TUSIKUBALI KUWA SEHEMU YA
KUWEZESHA UTENGENEZAJI WA SHERIA MBOVU KWA KUPITISHA MSINGI
AMBAO HATUAMINI KUWA MCHAKATO WAKO UMEBEBA UHALALI WA
DHAMIRA SAFI.
NINI CHA KUFANYA
KWA
MTU MWADILIFU KABISA KABISA, KUUNGA MKONO KITU UNACHOJUA
WAZI SIYO SAHIHI NI UHAINI DHIDI YA NAFSI YAKO MWENYEWE.
Kama wananchi tunaamini kwa dhati ya mioyo yetu kwa kadiri
ya utashi wetu, kuwa katiba hii
haikukidhi vigezo vya uhalali wa kimaadili na uhalisia
(siyo kisheria), tutakuwa tumelisaidia sana Taifa letu la
leo na vizazi vyetu vingi vijavyo kwa KUIKATAA. Na tufanyapo
hivyo, isiwe kwa nia ya kushindana, isiwe kwa nia ya
kuishinda CCM au kumshinda Mwenyekiti wa Bunge au kwa nia ya
kukomoana, bali tufanye hivyo kwa dhamira safi kwaajili ya
faida ya watu wetu wote. Kuna watu ni wanaCCM, wengine CUF,
CHADEMA, n.k. lakini ninyi nyote mtambue kuwa katiba yetu ya
nchi ni moja tu. Tunataka katiba ambayo itatoa uhakika wa
kila mtu kuishi katika Taifa letu kwa kujivunia Uraia wake
na wala siyo fedha, cheo, kabila, dini, ukoo au familia
yake. Tunataka katiba ambayo itamfanya kila mmoja akimwona
Mtanzania mwenzake aone ni mtu wa karibu kwake kuliko mtu wa
Taifa jingine lolote. Tunataka katiba itakayoyaweka mamlaka
ya umma juu ya kitu chochote.
Kuna
siku nilikuwa nasafiri, nilikuwa na haraka sana. Nilipokuwa
naondoka nilihisi gari yangu haikuwa vizuri sana, kwanza
nilifikiria niahirishe safari yangu kwa siku moja ili
niifanyie matengenezo. Lakini kwa kufikiria umuhimu wa
safari ile niliamua kusafiri bila hata ya kujua kwa undani
tatizo la gari langu, nia ilikuwa moja tu kuwa nisichelewe
kwenye program niliyoipanga. Siku ya pili ya safari yangu,
gari iliharibika kabisa, chombo kilichoharibika sikukipata
duka lolote, nilikokuwa nawahi sikufika. Siku ya tatu
nilitarajia nifike Mbeya nipande ndege. Nilikopanga kwenda
sikufika, mbeya nilichelewa ndege
iliyotakiwa kunichukua kwenda Dar ili nikapande ndege
nyingine, Tiketi zote za ndege zilipotea.
Nimeelezea
kisa hiki kwa sababu wapo watakaosema kuwa gharama ambayo
Taifa limeingia kwenye uandaaji wa katiba inayopendekezwa ni
kubwa mno na hivyo kitendo chochote cha kuufuta au
kuurekebisha mchakato mzima ni upotevu wa fedha na muda.
Ukweli ni kwamba, kwa Taifa letu kuwa na katiba ambayo haina
uhalali wa kimaadili ni gharama ambayo haiwezi kupimika.
Tusipoliona hili sasa, tunaweza kulipia maradufu huko
mbeleni. KWA
KUUJUA UKWELI HUO NAPENDEKEZA YAFUATAYO:
Wananchi WAIKATAE katiba
inayopendekezwa lakini iwe ni kwa dhamira safi na siyo
ushindani au kukomoana Baada ya katiba inayopendekezwa
kukataliwa, mchakato urudi nyumaSheria ya
mabadiliko ya katiba iangaliwe upya ili kuhakikisha sheria
hiyo inalenga kuhakikisha hakuna mtu au kundi linalohodhi
mchakato wa upatikanaji wa katibaMchakato wa katiba
uanze na uteuzi wa wajumbe wa Bunge la Katiba kwa
kuhakikisha hakuna kundi au taasisi ambayo inakuwa na
wawakilishi zaidi ya 10% ya wajumbe wa Bunge la Katiba
(Bunge la Jamhuri lichukuliwe kama taasisi ambayo
itawakilishwa na wajumbe wachache)Wajumbe wa Bunge
la Katiba
wachaguliwe na makundi yao moja kwa moja na idadi yao
iongezweKwenye Bunge la Katiba wawepo pia wataalam
huru wa mambo ya katiba ambao kazi yao itakuwa ni kushauri
na kuandika katiba kwa muundo unaokubalikaMuundo wa
Mwungano upigiwe kuraBart
Mkinga
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment