Mambo mengine mawili yanayoweza kumsumbua au kumkwamisha kabisa Lowasa ni 1) Kukataliwa na Baba wa Taifa 1995
2) kuwa na wapange wengi jambo linalodhibitisha uwezekano wa kuwa na mali nyingi na pia kuashilia uwezekano wa kuwa na liserikali likubwa kupita kawaida maana wote hao inabidi awashukuru 'kwa kazi kubwa' wanayofanya.
Namsubiri salimu Ahmed salim maana naye anatajwa
--------------------------------------------
On Thu, 9/25/14, mngonge franco <mngonge@gmail.com> wrote:
Subject: Re: [wanabidii] Edward Ngoyai Lowassa: Mchapa kazi mwenye nakisi ya uadilifu na falsafa
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thursday, September 25, 2014, 9:48 AM
Kama CCM watampitisha
basi kawa rais moja kwa moja na pengine hakuna sababu ya
kupiga kura tusipompigia jeshi litachukua nchi. Maana
tumekwishatishwa na wakubwa
2014-09-25 9:28
GMT+03:00 Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com>:
KATIKA
makala mbili nilizoandika na kuchapishwa katika gazeti hili
wiki mbili zilizopita, nilijaribu kuanisha sifa za kihaiba
na kikazi za mwananchi anayefaa kuwa Rais wetu wa
tano.Nashukuru
kwa mrejesho niliopokea kutoka kwa wasomaji wengi na
walionitia shime niendelee na makala hizi. Nawashukuru pia
waandishi wenzangu wa makala, akiwemo mwandishi mahiri na
mkongwe, Johnson Mbwambo, kwa kurejea maudhui ya makala
yangu katika andiko lake lililochapishwa katika gazeti hili
toleo Na. 370 la Septemba 10-16, 2014.Nakubaliana
kwa kiasi kikubwa na hofu aliyoonyesha juu ya uwezekano wa
wagombea kukidhi sifa nilizozianisha, pamoja na hitimisho
lake kwamba wagombea waliokwishajitokeza hadi sasa wana
ombwe kubwa la kifalsafa.Nilisitisha
kwa muda makala hizi kutokana na uzito wa maoni niliyopokea
kutoka kwa watu mbalimbali, wakiwemo viongozi waliojijengea
heshima kubwa katika nchi yetu. Wengi wa waliotoa maoni
walienda mbali na kunishauri niandike kitabu kuhusu wasifu
wa wagombea.Wengine
waligutuka nilipohitimisha makala yangu kwa ahadi ya kuanza
kuwajadili wagombea mmoja baada ya mwingine, wakidhani
kwamba nitakuwa nakwenda mbali mno! Aidha, wapambe wa
wagombea nao wamekuwa na wasiwasi kwamba nitawabeba baadhi
ya wagombea na kuwaharibia wagombea wao.Baadhi
ya wasomaji na wapambe wa wagombea wamenishauri kwamba
niache kuwajadili wagombea na niwaachie wananchi waamue
wenyewe. Nimekataa ushauri wao huu wa kuwachia wananchi
waamue wenyewe, na hivyo naendelea na uchambuzi wangu wa
wagombea wote waliojitokeza na watakaojitokeza.Nimeamua
kujitwika jukumu hili hatarishi kama sehemu ya wajibu wangu
wa kijamii katika kuchangia kuiepusha nchi kupata kiongozi
atakayetushtukiza bila kumjua sawasawa kabla hajaingia
madarakani. Ukimwacha Mwalimu Nyerere, marais wetu waliopita
na aliyepo walitushtukiza.Hatukumjua
vizuri Mzee Mwinyi kabla hajawa Rais, na vivyo hivyo kwa
Mzee Mkapa. Wote hawa walipatikana kwa mtindo unaofanana:
waliibuliwa bila kujitutumua wao wenyewe kuutaka urais kwa
udi na uvumba kama ilivyo kwa wagombea wa leo.Mzee
Mwinyi aliibuliwa na Kamati Kuu ya CCM, wakati Mzee Mkapa
aliibuliwa na Mwalimu Nyerere pasipo kutarajiwa. Bahati
nzuri waliibuliwa katika mtindo usiotia shaka sana kwa
sababu ni uzao wa taasisi za kueleweka kwa wakti ule, ambazo
ni Mwalimu mwenyewe na Kamati Kuu ya CCM ya wakati huo
ambayo isingekuwa rahisi kuitilia shaka katika maamuzi
yake.Pengine
tulimjua kidogo Rais Kikwete kabla ya kuingia madarakani kwa
sababu alijinadi vya kutosha kabla hajaingia ikulu mwaka
2005. Jina la Rais Kikwete lilianza kuwika kwa upana wake
kwa mara ya kwanza mwaka 1995 alipochukua na kurudisha fomu
ya kugombea urais kwa mbwembwe, sambamba na swahiba wake
mkuu wa wakati huo, Ndugu Edward Lowasa.Tangu
wakati huo tuliendelea kumwagiwa sifa kemkem juu ya Rais
Kikwete hadi anaingia madarakani mwaka 2005. Kwa hiyo,
hatukujua upande wa pili wa Rais Kikwete kwa maana ya
udhaifu wake kihaiba na kiutendaji kabla hajaingia
madarakani. Ndiyo kusema naye kwa kiasi fulani
alitushtukiza.Yote
hii ni kwa sababu tumekuwa hatuna utamaduni wa kuwadodosa
vya kutosha watu wanaotaka kuwa viongozi wetu. Maandishi
mengi kuwahusu wagombea huandikwa wakati wa kampeni
yakilenga kuwasifu wagombea fulani na 'kuwakandia'
wagombea wengine. Hatupati uchambuzi unaotuwezesha kuwajua
wagombea wote kwa ukamilifu wake katika kutusaidia kufanya
maamuzi ya maana. Hili ndilo ombwe la ufahamu ambalo
najaribu kuliziba katika mfululizo wa makala zangu.Katika
uchambuzi wangu nitajitahidi kuwa mkweli na kuzingatia
maadili na weledi wa kitaaluma ili kuepuka kupendelea au
kuonea. Hata hivyo, kama yalivyo maandishi yote katika
sayansi ya jamii, sitarajii kwamba makala hizi hazitaibua
hisia kali, shutuma, lawama na hata vitisho kutoka kwa
miongoni mwa wapambe wa wagombea ambao wamejiaminisha kwamba
wagombea wao ndio hasa wanaofaa kuongoza nchi hii na hakuna
mwingine.Niwatahadharishe
wasomaji na hasa wapambe wa wagombea kwamba ninachokiandika
hapa ni wasifu wa wagombea, kwa maana ya "biography" na
sio wasifu kwa maana ya "hagiography". Katika kuandika
hagiography, mwandishi hujikita katika kuanisha mazuri ya
mtu anayemwandika huku akifumbia macho udhaifu au upungufu
wake.Katika
kuandika biography mwandishi hujikita katika kuanisha pande
mbili za mhusika ikiwa ni mazuri na mapungufu yake. Kimsingi
hagiography huandikwa kwa ajili ya kuwatukuza na kuwasifu
'watakatifu' wanaoishi. Bahati mbaya au nzuri hatuna
hata mtakatifu mmoja kati ya wagombea wetu.Hivyo,
tutachambua nguvu na mazuri yao kwa upande mmoja, na
madhaifu na mapungufu yao kwa upande mwingine. Ni matumaini
yangu kwamba uchambuzi huu utawasaidia wagombea na wapambe
wao katika kujiimarisha kwa kukazia nguvu na mazuri yao na
kuchukua hatua stahiki katika kurekebisha au kujiandaa
kujibu mapigo kuhusu madhaifu na mapungufu yatakayojitokeza
katika makala hizi.Tunaanza
na Ndugu Edward Ngoyai Lowasa. Huyu alipata kuwa Waziri Mkuu
katika Awamu ya Kwanza ya utawala wa Rais Kikwete aliyedumu
kwa takribani miaka mitatu kutoka 2005 hadi 2008.Ndugu
Lowasa ndiye mwanasiasa pekee mwenye uwezekano wa kugombea
tena urais kati ya wanachama 17 wa CCM waliojitokeza
kugombea urais mwaka 1995. Wengine waliobaki ama wamefariki
dunia (wakiwemo Horace Kolimba, Tuntemeke Sanga, Kighoma
Malima), au wamezeeka na kuishiwa nguvu za kukabiliana na
mikiki ya kisiasa (wakiwemo John Malecela, Cleopa Msuya,
Pius Msekwa, Joseph Warioba), au 'wamepotea' katika
ulingo wa siasa (wakiwemo Rose Lugembe, Solomon Ole Saibul,
Aggrey Mwasagah, Omari Mwariko na Balozi Frederick
Rutakyamirwa).Wana
CCM wawili kati ya wale waliojitokeza mwaka 1995
walifanikiwa kuukwaa urais katika vipindi tofauti, ambao ni
Mzee Benjamin Mkapa (1995-2005) na Rais Jakaya Kikwete
(2005-2015). Jaji Mark Bomani aliyegombea pia mwaka 1995
naye bado yumo katika ulingo wa siasa lakini hajaweka wazi
kama atagombea au la hadi ninapoandika makala haya, lakini
kuna watu kadhaa wanamtajataja.Edward
Lowasa alijitokeza mwaka 1995 akiwa na mika 42 tu mbele
kidogo ya January Makamba (miaka 40), ambaye naye
amejitokeza kugombea akitembelea kete ya ujana.Aidha,
pamoja na kwamba hajawahi kutangaza rasmi na moja kwa moja,
Lowasa ni mwanasiasa ambaye anatajwa kwa uhakika zaidi
kwamba anautaka urais 2015, na pengine amejiandaa zaidi
kisaikolojia kuwa Rais kuliko mgombea mwingine. Kwa hivyo,
Lowasa ni moja ya wagombea wenye nguvu za kisiasa za kuweza
kushinda uteuzi ndani ya CCM na pengine kushinda kiti cha
urais.Kikazi,
Ndugu Edward Ngoyai Ngoyai Lowasa ni mwanasiasa ambaye
tunaweza kumuelezea kama kiongozi anayebebwa na taswira
chanya ya uchapa kazi katika sehemu mbalimbali alizofanya
kazi, ikiwemo alipokuwa Waziri Mkuu. Kihaiba, Ndugu Lowasa
anazungukwa na taswira hasi katika eneo la uadilifu,
kutokana na kuhusishwa na tuhuma na hisia nyingi kuhusu
rushwa na ufisadi hapa nchini.Pengine,
hiki ndicho kitakuwa kikwazo kikubwa zaidi katika mbio zake
za urais kwa sababu uadilifu itakuwa moja ya agenda kubwa
katika kampeni za 2015. Akifanikiwa kupenya uteuzi wa CCM
atakuwa na kazi ya kutosha kujibu maswali mengi kuhusu
tuhuma za ufisadi. Tutachambua taswira hizi pamoja na sifa
zingine za Ndugu Lowasa katika makala ijayo.-
See more at: http://www.raiamwema.co.tz/edward-ngoyai-lowassa-mchapa-kazi-mwenye-nakisi-ya-uadilifu-na-falsafa#sthash.v5xtqqn9.dpuf
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment