Tuesday, 11 February 2014

[wanabidii] TGNP - UTEUZI BUNGE LA KATIBA UNA MAPUNGUFU

11/02/2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ijumaa Februari 8, 2014 Rais Jakaya Kikwete alitangaza majina ya wajumbe 201 wa Bunge la Katiba, watakaoshirikiana na wajumbe wengine ambao ni wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wapatao 357, wajumbe wa Baraza la wawakilishi Zanzibar wapatao 81  Jumla kuu inalifanya Bunge la katiba kuwa na wajumbe 639.

Kwa mujibu wa sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka namba 81 ya 2013, rais amepewa mamlaka ya kuteua  wajumbe wa Bunge hili kwa kushauriana na rais wa Zanzibar baada ya kupelekewa  mapendekezo ya majina kutoka kwa makundi yote ya wananchi.

Sisi  wanaharakati wa masuala ya Kijinsia, haki za binadamu, demokrasia na utawala bora tumefuatilia kwa makini mchakato huu  tukiwa pamoja na wenzetu wa mashirika mengine ya kiraia na baadhi ya makundi  na kupendekeza  majina ya wataalamu wa masuala ya kijinsia na haki za binadamu ambao wangeweza kutoa uchambuzi wa kina na kushiriki kutetea baadhi ya vifungu vya rasimu ambavyo vinabeba sauti za wananchi kwa mustakabali wa taifa letu.
Mchakato huu wa uteuzi  umekuwa na mapungufu na sura tofauti kama ilivyokuwa katika kipindi cha kujadili Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba 2013.

Kukosekana kwa ushiriki mpana wa uwakilishi wa makundi halisi yaliyoko pembezoni na kuchomeka majina ya watu wasiostahili kwenye nafasi za makundi mengine kutasababisha mapungufu makubwa ya uwakilishi katika mchakato huu.

Tumesikitishwa na kuingizwa kwa majina ya wanasiasa kwenye  kundi la NGO na kuwaacha wawakilishi wa asasi za kiraia wakati wanasiasa walikuwa na uwakilishi mkubwa kwenye kundi lao la watu 40. Aidha kundi la watu wenye mlengo unaofanana  nalo hatukupewea tafsiri  halisi kuwa ni watu kuitoka kundi gani au ni kina nani badala yake wameingia wanasiasa na kulifanya Bunge hili la katiba kuwa na wanasiasa wengi zaidi ya makundi mengine.
Wanaharakati tunahoji nini ilikuwa tafsiri ya watu wenye malengo yanayofanana? Baada ya wanasiasa kuteuliwa kupitia kundi lao la wajumbe 40 hawakutakiwa kuingia tena kupitia kundi hili la pili badala yake wangezingatia  makundi yaliyokuwa yamebaki.

Tunajiuliza kwa hali hii ya kujaza wanasiasa kwenye haya makundi ya wananchi tutapata katiba mpya tunayostahili kuwa nayo? Tunadai uwakilishi zaidi wa makundi mengine kwenye hili Bunge kwa sababu:-
(i)Wabunge wa sasa hawakuchaguliwa kwa kuzingatia uwiano wa kijinsia na makundi yaliyoko pembezoni
(ii)  Wabunge wa sasa wamechaguliwa kwa kuzingatia mfumo na ushawishi na itikadi za vyama vyao vya siasa; na sifa  zilizopelekea kuchaguliwa kwao na hadidu zao za rejea zimejikita katika kusimamia na kutetea katiba iliyopo na siyo kitunga Katiba;

Tunaendelea kudai usawa wa Kijinsia katika mchakato huu kwani msingi wa kijinsia haujazingatiwa kama vile Itifaki ya Maputo, AU Constituent Act, AU Shared Values na CEDAW na Mkataba wa Watoto (CRC)zinavyotamka.

Mwisho tunataka masuala muhimu ya wanawake ambayo yameonekana kwenye rasimu ya pili ya Katiba yaheshimiwe na wajumbe wa Bunge hili na yasitolewe bali yaboreshwe ili kutoa nafasi ya ushiriki kamili wa wanawake na wanaume  katika mgawanyo wa rasilimali za Taifa na kwenye fursa za uongozi.

Imetolewa na:
Signed
Lilian Liundi
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
TGNP Mtandao

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment