Kwa mara ya kwanza maneno: NGUVU YA UMMA niliyasikia yakisemwa na viongozi wa CHADEMA. Polepole wakawa wakiwahimiza wananchi kuikatalia serikali pale (Serikali) inapokuwa imewatendea kinyume na matarajio wananchi. Mwanzoni ilikuwa ni maandamano na yaliongozwa na CHADEMA. Baadaye wananchi walijiongoza kupinga wasichokitaka. Mifano hai ni Mbeya pale wamachinga walipokwaruzana na serikali mpaka Mkuu wa Mkoa akaomba msaada wa Mbunge wa Mbeya mjini ambaye ni mbunge wa CHADEMA. Mfano wa pili ni Mtwara na kwa kweli huko hakukuwa na harufu ya CHADEMA.
Baada ya hapo sasa tunashuhudia wafugaji na wakulima wanavyosuguana na majuzi wakulima walifunga barabara ya Morogoro Iringa. Nguvu ya umma.
Ghafla tulianza kushuhudia nchi mbali mbali zikikabiliwa na wananchi kupinga mambo Fulani. Hii si katika nchi za ulimwengu wa tatu tu. Hata nchi zilizoendelea kama Uingereza na Ufaransa. Nguvu ya umma imekuwa nguvu ya umma.
Nimeambatanisha picha ya video hapa (Download). Simba wawili waliamua kumuonea nyati mmoja. Kwa dakika arobaini na tano wamemzungusha mpaka akachoka. Kuna mahala nyati huyo anaonekana anawazungusha simba wote wawili na hii inaonekana ana nguvu kuliko wao. Lakini baada ya kumchosha alilazwa chini na simba mwenye njaa akawa anajipumzisha kidogo ili aje afurahie mawindo yake. Kwa kawaida simba anaweza kuliingia kundi la nyati hata mia. Akisha mnasa mmoja wengine wanajiondokea.
Zamu hii zivyo. Nyati wawili walikuwa karibu wakishuhudia mwenzao akinyanyaswa. Mwisho wakaamua kuingilia kati. Kwa ushirikiano jike akilinda mazingira dume likamvaa simba na kumrusha mara mbili hewani. Alipopata mwanya akatokomea. Hii ni nguvu ya umma. Umma wa nyati uliamua kutonyanyswa na simba.
Sasa hii sera ya Nguvu ya umma mwanzilishi wake nani? Ni CHADEMA kweli????
Elisa Muhingo
0767187507
0 comments:
Post a Comment