Elisa, nguvu ya umma ni sera au kauli mbiu au kibwagizo?
----------
Sent from my Nokia phone
------Original message------
From: ELISA MUHINGO <elisamuhingo@yahoo.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Tuesday, February 11, 2014 12:10:29 PM GMT-0800
Subject: [wanabidii] Sera ya nguvu ya umma mwanzilishi wake nani
Kwa
mara ya kwanza maneno: NGUVU YA UMMA niliyasikia yakisemwa na viongozi wa
CHADEMA. Polepole wakawa wakiwahimiza wananchi kuikatalia serikali pale
(Serikali) inapokuwa imewatendea kinyume na matarajio wananchi. Mwanzoni
ilikuwa ni maandamano na yaliongozwa na CHADEMA. Baadaye wananchi walijiongoza
kupinga wasichokitaka. Mifano hai ni Mbeya pale wamachinga walipokwaruzana na
serikali mpaka Mkuu wa Mkoa akaomba msaada wa Mbunge wa Mbeya mjini ambaye ni
mbunge wa CHADEMA. Mfano wa pili ni Mtwara na kwa kweli huko hakukuwa na harufu
ya CHADEMA.
Baada
ya hapo sasa tunashuhudia wafugaji na wakulima wanavyosuguana na majuzi
wakulima walifunga barabara ya Morogoro Iringa. Nguvu ya umma.
Ghafla
tulianza kushuhudia nchi mbali mbali zikikabiliwa na wananchi kupinga mambo Fulani.
Hii si katika nchi za ulimwengu wa tatu tu. Hata nchi zilizoendelea kama
Uingereza na Ufaransa. Nguvu ya umma imekuwa nguvu ya umma.
Nimeambatanisha
picha ya video hapa (Download). Simba wawili waliamua kumuonea nyati mmoja. Kwa dakika
arobaini na tano wamemzungusha mpaka akachoka. Kuna mahala nyati huyo
anaonekana anawazungusha simba wote wawili na hii inaonekana ana nguvu kuliko
wao. Lakini baada ya kumchosha alilazwa chini na simba mwenye njaa akawa
anajipumzisha kidogo ili aje afurahie mawindo yake. Kwa kawaida simba anaweza
kuliingia kundi la nyati hata mia. Akisha mnasa mmoja wengine wanajiondokea.
Zamu
hii zivyo. Nyati wawili walikuwa karibu wakishuhudia mwenzao akinyanyaswa.
Mwisho wakaamua kuingilia kati. Kwa ushirikiano jike akilinda mazingira dume
likamvaa simba na kumrusha mara mbili hewani. Alipopata mwanya akatokomea. Hii
ni nguvu ya umma. Umma wa nyati uliamua kutonyanyswa na simba.
Sasa
hii sera ya Nguvu ya umma mwanzilishi wake nani? Ni CHADEMA kweli????
Elisa Muhingo
0767187507
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:
Post a Comment