Tuesday, 4 February 2014

Re: [wanabidii] JESHI LA POLISI LASAKA JAMBAZI LILILOUA WATU WANANE HUKO RORYA, TARIME

Njia nyingi za kumpata huyu mtu. hata kujiuliza maswali mengine. Mfano:
Huyu si afisa wa polisi? hana uhusiano wowote na Polisi? Hafahamiki Polisi?
Kwa nini alifanya uhalifu kwa kipindi kirefu bila kuingiliwa?
Maswali kama haya yanaweza kusaidia sana kuisaidia polisi. La sivyo overtime litasahaulika na mtu huyu atadunnda tu mitaani



On Friday, January 31, 2014 1:36 PM, "hosea.ndaki@gmail.com" <hosea.ndaki@gmail.com> wrote:
Wasifu wa huyo jambazi ukoje? Ni mrefu au mfupi? Mnene au mwembamba? Anakadiriwa kuwa na umri gani?

----------
Sent from my Nokia phone

------Original message------
From: Emma Kaaya <emmakaaya@gmail.com>
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Wednesday, January 29, 2014 1:20:15 AM GMT-0800
Subject: [wanabidii] JESHI LA POLISI LASAKA JAMBAZI LILILOUA WATU WANANE HUKO RORYA, TARIME

Ndugu zangu waandishi wa habari, nimewaiteni hapa kwa dharura, ili kuweza
kuwafahamisha hali halisi ya mauaji yaliyotokea katika siku za hivi
karibuni katika mkoa wa Kipolisi wa Tarime Rorya.

Mnamo tarehe 26 Januari, 2014 majira ya saa 12.00 asubuhi huko katika
kijiji cha Mogabiri
katika mkoa wa kipolisi Tarime Rorya, jambazi asiyefahamika kwa jina
aliwaua kwa risasi Zakaria Mwita Marwa miaka 28 na Erick Lucas Maranya
miaka 24 baada ya kukutana nao njiani. Siku hiyohiyo, majira ya saa 4:00
usiku, katika kijiji hichohicho cha Mogabiri, jambazi huyo alimuua Robert
Kisiri miaka 45 baada ya kuvamia Grocery inayomilikiwa na Chacha Ryoba na
kumjeruhi mtu mwingine mmoja. Tarehe 27 Januari, 2014 majira ya 11:30
alfajiri katika kijiji cha Mugabiri, jambazi huyo alifanya mauaji tena kwa
kumpiga risasi David Mwasi Matiko miaka 39 na kumpora simu yake aina ya
Nokia. Katika tukio hilo, pia, alimjeruhi Machungu Nyamahemba miaka 19
ambaye bado amelazwa katika hospitali ya Tarime kwa Matibabu.

Siku hiyohiyo ya tarehe 27 Januari, 2014 majira ya saa 2:00 usiku katika
kijiji cha Nkende, jambazi huyo alimuua kwa kumpiga risasi Juma Marwa
Nyaitara miaka 30. Baada ya kufanya mauaji hayo, jambazi huyo aliwapora
simu zao za mkononi Chacha Magige na Masero Marigiri wote wa kijiji cha
Nkende. Usiku wa kuamkia tarehe 28 Januari, 2014, jambazi huyo aliendelea
kuua watu wengine watatu ambao bado majina yao hayajafahamika. Mtu mmoja
alipigwa risasi wakati akiendesha pikipiki
katika kijiji cha Nkende na wengine wawili waliuawa baada ya kukutwa na
jambazi huyo wakiwa wanatengeneza gari lililokuwa limewaharibikia katika
kijiji cha Mogabiri.

Hadi sasa juhudi kubwa za kumsaka jambazi huyo zinaendelea kufanyika na
Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama
pamoja na wananchi.  Aidha, mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernesti
Mangu, ametuma timu maalum kutoka makao makuu ya jeshi la Polisi
inayohusisha kamisheni ya Oparesheni, Upelelezi na Intelijensia kwenda
kuongeza nguvu katika juhudi zinazofanyika na ngazi ya mkoa kuhakikisha
kwamba, jambazi huyo anakamatwa upesi ili kuondoa hofu kwa wananchi.

Jeshi la Polisi nchini, linatoa wito kwa wananchi wote kutoa ushirikiano
ili jambazi huyo aweze kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria
haraka. Mwananchi mwenye taarifa za mhalifu huyo anaweza kutumia namba ya
simu ifuatayo 0754 785557.

Mkuu wa Oparesheni wa Jeshi la Polisi,
Kamishna Paul Chagonja

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment