Friday, 14 February 2014

Fwd: Re: [wanabidii] Maoni ya Waislamu kuhusu mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba ya Tanzania

-------- Original Message --------
Subject: Re: [wanabidii] Maoni ya Waislamu kuhusu mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba ya Tanzania
From: ngupula <ngupula@yahoo.co.uk>
To: Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com>
CC:

Ni mapendekezo mazuri...lakini binafsi siafiki hata kidogo serikali kuanza kupendelea kundi fulani na kuliacha kundi fulani...mtindo kama huo tayari umeonyesha kuleta mgogoro haswa katika utoaji wa mikopo elimu ya juu. Watu fulani hupewa 100 percent ya mkopo wakati watu fulani hupewa asilimia tu fulani kama 30 au 40..ndio lengo linaweza likawa ni zuri tu lakini msingi huo unawaumiza sana watu wa aina fulani ya kipato na kimsingi ni kuwataifisha kwa namna fulani kama kwa jinsi tu ulivyokuwa utaifishaji wakati wa ujamaa. Na izingatiwe kuwa watu hao ndio walipa kodi kwa serikali na wangestahili kuhudumiwa..kamwe hatuwezi kuwa na tabaka la walipa kodi huku hawapewi huduma na tabaka la wahudumiwa. Mi nafikiri serikali itoe huduma zote kwa usawa..katika jamii kubwa kama yetu ni lazima watakuwepo waliotangulia na walionyuma. ..tatizo hili pia linajidhihilisha katika bima ya afya ya taifa. Haiwezekani aliyechangia laki moja apewe huduma sawa na aliyechangia alfu 10..huku ni kuwatweza baadhi ya watu fulani katika nchi na kuwabebesha mizigo isiyo yao..

Juma Mzuri <jumamzuri@gmail.com> wrote:

Maoni ya Halmashauri Kuu ya Waislamu kuhusu mapendekezo ya mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
1.0 Utangulizi:
MAONI haya yanalenga katika maeneo matatu makubwa. Kwanza yanalenga katika kuainisha haja na namna ya kutanua demokrasia (kwa kuiwajibisha zaidi serikali). Kama ilivyo sasa katika Katiba, serikali, na hasa Rais, wana madaraka na majukumu mengi na makubwa. Pamoja na mambo mengine, Rais ni Mkuu wa Dola, Mkuu wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu.
Kulingana na madaraka na majukumu hayo, Rais na serikali hawawajibiki ipasavyo. Rais ni Sehemu ya Bunge, lakini si Mbunge na hawajibiki Bungeni. Aidha, Rais ni Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri, lakini si Mjumbe wa Baraza hilo. Hata ikabidi Baraza la Mawaziri kujiuzulu, Rais anabaki madarakani. Pia Rais huteuwa Mawaziri ambao wanawajibika kwake na siyo kwa Bunge. Mfumo wa serikali mchanganyiko kati ya mfumo wa Urais (Presidential System) na ule wa Kibunge (Parliamentary System) na umejenga Urais wa Kifalme (Imperial Presidency) ambao hauisihi baada ya uhuru.
Pili, maoni haya yanalenga katika kuainisha haja na namna ya kuimarisha muundo wa serikali na, hasa, Muungano. Katiba ya Muungano ilijengwa juu ya nguzo kuu tatu, yaani: Chama Dola (State Party), Urais wa Utendaji (Executive Presidency) na Serikali mbili za Muungano. Baadhi ya nguzo hizi sasa hazipo. Mfumo wa chama Dola umeondoka. Aidha, Rais wa Zanzibar siyo tena Makamu wa Rais na kiungo muhimu cha Muungano. Kwa hiyo, ni dhahiri kwamba, tangu kuondoka kwa nguzo hizi na kuja kwa mfumo wa vyama vingi. Msingi wa muungano katika Katiba na msingi wa Katiba ya Muungano umedhoofika. Nguzo iliyobaki ya Serikali mbili pekee haiwezi kuisimamisha katiba ya sasa. Hali ambayo imeleta haja ya kubadili muundo wa serikali na katiba.
Tatu, maoni haya yanalenga katika kuainisha haja na njia za kuinua wanyonge. Katiba ya sasa inachukulia kuwa watu wote ni sawa; au ina dhana kuwa usawa utakuja kutokana na nia nzuri (good will) ya watu wa juu. Ukweli ni kwamba watu ni tofauti. Kuna watu (wa baadhi ya mikoa, makabila, maumbile, jinsia na itikadi) ambao kwa sababu za kihistoria na nyinginezo wamekuwa na hali duni. Kuwachukulia watu hawa kuwa wako sawa na wale wenye hali bora ni kutowajali na kutotambua hali halisi ya jamii yetu.
Isitoshe, Katiba ya sasa inadaiwa kuwa haina dini (Secular). Kama ni hivyo, inalinda vipi haki za jamii ambayo ina dini? Masuala haya ni muhimu kwa vile, kama dini, Secularism ni itikadi na ina wafuasi wake. Inawezekana kwamba Secularism ni itikadi dhidi ya dini. Si makosa pia kusema kuwa katiba isiyo na dini ni katiba ya watu wasio na dini (Secularists); au katiba ya watu ambao dini zao hazina mifumo ya kikatiba. Katiba hiyo inaweza isijali haki za watu ambao dini zao zina mifumo kamili ya maisha. Kuwatendea haki waumini wa itikadi zote, Katiba isiyo na DINI haitoshi. Inayotakiwa ni Katiba isiyo na ITIKADI yoyote (hata ya ujamaa); au katiba yenye mchanganyiko muafaka wa itikadi zote. Kwa maneno mingine, katiba inayotakiwa ni ile isiyopendelea itikadi yeyote, lakini inayolinda itikadi zote.
2.0 Mapendekezo:
2.1 Muundo wa Dola:
2.1.1 Serikali:
(a) Urais:
Rais aendelee kuchaguliwa moja kwa moja na wananchi kwa zaidi ya asilimia 50 ya wapiga kura wote. Na iwapo hatapatikana yeyote mwenye kupata zaidi ya asilimia 50, itabidi mshindi wa kwanza na pili wapigiwe tena kura ili kuweza kumpata mshindi wa zaidi ya asilimia 50 za wapiga kura wote.
Rais ni lazima athibitishwe na Mahakama katika kipindi cha mwezi mmoja baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa.
Kuwepo na uwezekano wa kuhoji matokeo ya uchaguzi wa Rais kupitia Mahakama, ikiwa kuna sababu za msingi za kufanya hivyo (kama vile vitendo vya rushwa au ubadhilifu wa kura), kabla matokeo hayo kuthibitishwa na Mahakama.
Wagombea binafsi wa Urais waruhusiwe.
Rais asiwe sehemu ya Bunge. Sheria zipitishwe na Bunge bila ya kuwa na haja ya Rais kuidhinis

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment