Thursday, 20 October 2016

[wanabidii] Ukatili majumbani wawapeleka watoto kuishi mitaani Mwanza

Ukatili majumbani wawapeleka watoto kuishi mitaani Mwanza


[caption id="attachment_75810" align="aligncenter" width="600"]<img class="size-full wp-image-75810" src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2016/10/IMG_1447.jpg" alt="Mkurugenzi wa shirika la Railway Children, Kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Pete Kent akizungumza na waandishi wa habari kuzungumzia utafiti wa watoto wa mitaani walioufanya mwaka 2015 mkoani Mwanza. " width="600" height="765" /> Mkurugenzi wa shirika la Railway Children, Kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Pete Kent akizungumza na waandishi wa habari kuzungumzia utafiti wa watoto wa mitaani walioufanya mwaka 2015 mkoani Mwanza.[/caption]

&nbsp;

[caption id="attachment_75812" align="aligncenter" width="800"]<img class="size-full wp-image-75812" src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2016/10/IMG_1463.jpg" alt="Mkurugenzi wa shirika la Railway Children, Kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Pete Kent akizungumza na waandishi wa habari kuzungumzia utafiti wa watoto wa mitaani walioufanya mwaka 2015 mkoani Mwanza. Kulia ni Ofisa Maendeleo na Miradi wa Railway Children, Jo De Lamar akifuatilia mkutano huo." width="800" height="571" /> Mkurugenzi wa shirika la Railway Children, Kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Pete Kent akizungumza na waandishi wa habari kuzungumzia utafiti wa watoto wa mitaani walioufanya mwaka 2015 mkoani Mwanza. Kulia ni Ofisa Maendeleo na Miradi wa Railway Children, Jo De Lamar akifuatilia mkutano huo.[/caption]

&nbsp;

[caption id="attachment_75811" align="aligncenter" width="800"]<img class="size-full wp-image-75811" src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2016/10/IMG_1455.jpg" alt="Mkurugenzi wa shirika la Railway Children, Kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Pete Kent akizungumza na waandishi wa habari kuzungumzia utafiti wa watoto wa mitaani walioufanya mwaka 2015 mkoani Mwanza. Kushoto ni Afisa Mradi wa Railway Children Africa, Adam Kaombwa na Ofisa Maendeleo na Miradi wa Railway Children, Jo De Lamar (kulia)." width="800" height="484" /> Mkurugenzi wa shirika la Railway Children, Kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Pete Kent akizungumza na waandishi wa habari kuzungumzia utafiti wa watoto wa mitaani walioufanya mwaka 2015 mkoani Mwanza. Kushoto ni Afisa Mradi wa Railway Children Africa, Adam Kaombwa na Ofisa Maendeleo na Miradi wa Railway Children, Jo De Lamar (kulia).[/caption]

&nbsp;

[caption id="attachment_75808" align="aligncenter" width="800"]<img class="size-full wp-image-75808" src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2016/10/IMG_1403.jpg" alt="Meneja Habari na Utetezi wa HakiElimu, Elisante Kitulo (kushoto) akizungumza kuwakaribisha viongozi wa Railway Children kabla ya kuzungumzia matokeo ya utafiti wa watoto wa mitaani uliofanyika Mkoa wa Mwanza mwaka jana." width="800" height="485" /> Meneja Habari na Utetezi wa HakiElimu, Elisante Kitulo (kushoto) akizungumza kuwakaribisha viongozi wa Railway Children kabla ya kuzungumzia matokeo ya utafiti wa watoto wa mitaani uliofanyika Mkoa wa Mwanza mwaka jana.[/caption]

&nbsp;

[caption id="attachment_75814" align="aligncenter" width="800"]<img class="size-full wp-image-75814" src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2016/10/IMG_1474.jpg" alt="Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa katika mkutano na viongozi wa Shirika la Railway Children katika ofisi za taasisi ya HakiElimu jijini Dar es Salaam leo." width="800" height="542" /> Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa katika mkutano na viongozi wa Shirika la Railway Children katika ofisi za taasisi ya HakiElimu jijini Dar es Salaam leo.[/caption]

&nbsp;

<strong>UTAFITI</strong> uliofanywa na shirika la Railway Children Africa mkoani mwaka jana umebaini kuwa idadi kubwa ya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi mitaani wamenyanyaswa kingono, huku miongoni mwa sababu zinazochangia kukimbia nyumbani na kuishi mitaani ni ukatili.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Shirika la Railway Children, Bw. Pete Kent alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kubainisha matokeo ya utafiti juu ya watoto wa mitaani mkoani Mwanza.

Alisema utafiti umebaini kuwa, asilimia 100 ya watoto wa mitaani wamewahi kunyanyaswa kimwili kwa vitendo au hata kwa maneno, huku ukionesha asilimia100 ya wasichana na 25 ya wavulana wakidhalilishwa kijinsia.

"Watoto na familia zilizoathiriwa na ukatili mara nyingi hutengwa na kunauwezekano wa kutonufaika na mipango endelevu na badala yake wanahitaji huduma zaidi za kiushauri ili kutibu majeraha yaliyotokana na ukatili katika familia zao," alisema Mkurugenzi Kent.

Aidha Afisa Mradi wa Shirika la Railway Children Africa, Adam Kaombwa aliongeza kuwa utafiti huo ulibaini jumla ya watoto 1940 wanaishi na kufanya kazi mitaani katika Jiji la Mwanza, ikiwa ni ongezeko la asilimia 25 ukilinganisha na tafiti za nyuma.

&nbsp;

[caption id="attachment_75809" align="aligncenter" width="663"]<img class="size-full wp-image-75809" src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2016/10/IMG_1427.jpg" alt="Afisa Mradi wa Shirika la Railway Children Africa, Adam Kaombwa aliongeza akizungumza na waandishi wa habari kufafanua juu ya matokeo ya utafiti wa watoto wa mitaani walioufanya mwaka 2015 mkoani Mwanza. Kushoto ni Mkurugenzi wa shirika la Railway Children, Kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Pete Kent akifuatilia." width="663" height="600" /> Afisa Mradi wa Shirika la Railway Children Africa, Adam Kaombwa aliongeza akizungumza na waandishi wa habari kufafanua juu ya matokeo ya utafiti wa watoto wa mitaani walioufanya mwaka 2015 mkoani Mwanza. Kushoto ni Mkurugenzi wa shirika la Railway Children, Kanda ya Afrika Mashariki, Bw. Pete Kent akifuatilia.[/caption]

&nbsp;

Alisema utafiti umebaini ndani ya miezi 12, idadi ya wasichana wanaofanya biashara ya ngono imeongezeka kwa asilimis 229, huku ongezeko kubwa likiwa ni la wasichana wenye umri wa kati ya miaka 11 hadi 14.
"Idadi ya wasichana wanaofanya biashara ya ngono ni 418, na kati ya hao 218 ni wenye umri chini ya miaka 18. Pia kuna hali ya kupungua kwa asilimia 40 ya watoto wa mitaani wenye umri kati ya miaka 0-14 kwa kipindi cha ya miaka mitatu – kwa walengwa wetu wakuu," alieleza Kaombwa.

Alisema pamoja na hayo shirika linatambua juhudi za serikali ya Tanzania katika kutoa huduma, msaada na ulinzi kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu na kuwepo kwa Mpango wa Taifa wa Kukomesha Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto na hadhi ya Tanzania kama nchi ya mfano katika Ubia wa Kimataifa wa Kukomesha Ukatili dhidi ya Watoto.

&nbsp;

[caption id="attachment_75813" align="aligncenter" width="800"]<img class="size-full wp-image-75813" src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2016/10/IMG_1468.jpg" alt="Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa katika mkutano na viongozi wa Shirika la Railway Children katika ofisi za taasisi ya HakiElimu jijini Dar es Salaam leo." width="800" height="475" /> Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa katika mkutano na viongozi wa Shirika la Railway Children katika ofisi za taasisi ya HakiElimu jijini Dar es Salaam leo.[/caption]

&nbsp;

Hata hivyo ameipongeza kwa jitihada dhahiri za kuwepo kwa dhamira ya kweli ya kisiasa katika kubadili hali ya watoto wote wanaoishi katika mazingira magumu, wakiwemo watoto mitaani.

Pamoja na hayo ili kukabiliana na ongezeko la watoto wanaoishi katika mazingira magumu, hatarishi na wapweke mitaani shirika la Railway Children Africa limeandaa kongamano la kimataifa la 'Kuvunja mzunguko' linalotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Benki kuu ya Tanzania Novemba 17- 18 mwaka huu.

Kongamano la kuvunja mzunguko ni kwa mtu yeyote anayeweza kufanya kazi ili kubadilisha maisha ya watoto wa mitaani-kushikamana popote duniani, ikiwa ni pamoja na wale wanaofanya kazi katika jamii moja kwa moja, kubuni mipango ya mashirika yasiyo ya kiserikali, watunga sera, bajeti au watafiti.

Bw. Kent aliongeza kuwa kongamano hilo litatoa fursa kwa wajumbe zaidi ya 250 kushirikiana, kujifunza na kupata uelewa mkubwa wa mikakati iliyothibitika ya kuvunja mzunguko wa ukatili kwa familia dhidi ya watoto wanaoishi mitaani.

--
___________________________________________________________________________________
Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com.
Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com
Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470
Web:- www.thehabari.com  
          http://joemushi.blogspot.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment