Thursday 13 October 2016

[wanabidii] JANGA LIKIJA JUU YA JANGA: NANI ATASIMAMA KUELEZA?

Mwezi mmoja uliopita tarehe 10 September kulitokea tetemeko la ardhi na kuleta maafa katika Mkoa wa Kagera. Watu wasiozidi 19 walikufa, nyumba kadhaa zikaanguka na nyingine nyingi zikapata nyufa. Nyufa nyingine ni hatarishi kiasi nyumba hizo ni hatari kuzitumia na nyufa nyingine si hatarishi. Katika dharura hiyo miyndombinuu kadhaa iliharibika. Mfano ni shule kadhaa zilianguka, barabara zilipasuka, makanisa yalianguka na kadhalika.
Nchi, serikali, balozi za nchi za nje, vyama vya siasa; mashirika mbalimbali na watu binafsi waliitikia kwa kutoa michango mbalimbali kwa lengo la kusaidia waathirika wa tetemeko hilo

Niliwahi kufanya hesabu wakati huo nyumba zikiwa elfu sita zilizoathirika nikahesabu kama sh. Million 10 zingetumika kwa kila nyumba basi zingehitajika bilioni 60. Hazipo.
Kati ya waathirika wapo waliokwisha maliza kurekebisha au kujenga upya nyumba zao kiasi athari za tetemeko kwao si hoja. Hii ni nafuu kwa kamati ya maafa.
Wapo ambao wamejaribu na kukwama kwa sababu uwezo wao wa kujenga ni mdogo. Wapo ambao ni haki yao kukaa kimya na kusubiri msaada maaqna hawawezi kuzijenga.
Misaada ambayo imetolewa hadi sasa si ile ya kurejesha majengo ya kuishi.
Ninapopita maeneo yaliyoathirika nayaona yote ninayoyaeleza. Ninaona pia watu wanaoishi kwenye nyumba ambazo ni hatari kutokana na nyufa zilizotokea.
Ninaamini halitakuwa jambo la kushangaza kama mvua zitakuja na upepo mkali mkoani Kagera. Lakini najiuliza mvua hiyo ikinyesha na kuzipiga na kuziangusha nyumba zilizopasuliwa na tetemeko na watu zaidi ya waliokufa kwa tetemeko wakafa; ni kiongozi gani atasimama kutoa maelezo? Rais, makamu wake, Waziri Mkuu au Mkuu wa Mkoa? Atawalaumu watu kwa kutumia nyumba hizo kwa sababu serikali ilishazitangaza kuwa mipasuko iliyotokea ni hatarishi? Jambo hili si la kucheza nalo. Kuna miundo mbinu inayowezesha kufika walipo waathirika. Nani ataelewa kuwa serikali ilitangulia kutengeneza miundo mbinu? Misaada iliyotolewa ilikuwa inatangazwa kuwa ni kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa Tetemeko. Ni sawa, Na shule kujengwa ni kuwasaidia waathirika. Lakini kweli baada ya wanafunzi kusambazwa shule nyingine inaeleweka kuwa watu waendelee kuishi kwenye mahema au nyumba mbovu kwa sababu kwanza tunajenga shule? Nani ataelewa? Nani ataelewesha? Serikali ilipotangaza kutoa sementi na mabati waathitika waliandaa mazingira kuanza kujenga. Nani kasema kila aliyevunjikiwa nyumba ana uwezo wa kujenga? Ninafikiri hili jambo si la kuchezea. Mvua inakuja na ipo itakayonyesha kwa vurugu. Ni kawaida. Lazima itazivuruga nyumba ninazozipitia kila mara. Kati ya wote wanaowajibika na kadhia iwezayo kutokea, Mkuu wa mkoa namuona akiwa hatarini. Ndiye aliye karibu. Kama wote wakibanwa watasema hatukujua. Yeye atasemaje. Lakini pia ni garama ndogo yeye kuwajibika/kuwajibishwa. Nyumba zikianguka na kuua watu mia rais atatangaza tu kuwa 'amemtumbua' kwa uzembe maana hakuweza kutumia misaada vizuri. Ndiye mwenyekiti wa kamati ya maafa. Baada ya hapo atachaguliwa mwingine mambo kwisha. Si kama kumuwajibisha waziri Mkuu ambaye baraza lote litafumuliwa. Lakini heri Mkuu wa Mkoa kutumbuliwa kwa sababu aliamua kutumia misaada kuwajengea nyumba badala ya kuacha wao kujijengea kuliko kutumbuliwa kwa sababu watu walifia kwenye nyumba zilizobomolewa na tetemeko huku akiwa na misaada chini yake. Ataeleweka kwa dhamira yake na kwa umma, Tusipuuze tahadhali kama hizi.
Elisa Muhingo



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.





--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment