Friday 14 October 2016

Re: [wanabidii] JANGA LIKIJA JUU YA JANGA: NANI ATASIMAMA KUELEZA?

Elisa, 

kwa mara nyingine nauona umuhimu wa kukutana na wewe ili nipate mahojiano zaid juu ya kazi ninazozifanya hivi sasa za kuripot na kuchambua juu ya tetemeko. yaani Matokeo yake madhara yake na nini kifanyike kusaidia watu. 

Jana nilikuwa Minziro ambako niko epicenter ya tetemeko, nilitembelea wananchi na wanafunzi shuleni, nimegundua kitu kingine, kuna hali ya taharuki kwa wanafunzi, walimu na wananchi kwa ujumla. Sijui hili umeliona mzee Elisa?

Je umerudi Bukoba ili tufanye miadi kwa ajili ya maongezi juu ya hili? 

2016-10-14 10:18 GMT+03:00 'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Muhimu cha kufanya Elisa ni kwanza:
i) Kutumia wataalamu wa Ecology na wa masuala ya matetemeko ya ardhi kuangalia kama hilo eneo wanakoishi ni hatarishi kwa matetemeko na mafuriko.

2) Ikiwa ni hatarishi ni wazilikitokea tena litabomoa nyumba na kuingiza jamii ktk hasara. Hivyo budi watafute eneo la kuwajengea nyumba kwa kutumia NHC kwa kujenga nyumba ambazo hela zitatosha na kulingana na wingi wa watu katika familia kwa standard space kwani building regulation zipo. Kusiwe na mbanano. Hivyo itabidi kutafuta eneo na kufanya participatory land use planninh na kuwapa hati miliki ya makapo. Budi watoe fidia kwa ardhi ya kufaa watakayochukua kama sio ya serikali.

3) Afanyavyo kiongozi kuwajengea nyumba ni muhimu ila anajenga wapi panapofaa kuishi ukiangalia mazingira yasiyo hatarishi. Ukiwapa pesa hao baadhi wataanza kunywa Lubisi na baadhi ya walezi au watoto makanjanja wataanza kutaka kuzitumia vibaya. Ukiwapa vifaa baadhi watauza na kusepa mjini na kuacha vizee vikiteseka. Vibaka wapo pia ktk familia na ndiko kunakotoka akina scorpion, panya road na fisi na wengineo.

4) Mahali ambako palitokea tetemeko watakuwa wana mashamba yao wapewe Hati Miliki ya Kimila. Kule wanakopimiwa wapewe Hati Miliki ya Serikali na ipigwe muhuri-Haihamishiki bila ya kibali cha Waziri wa Ardhi. Hii itakomesha uuzaji wa ardhi hovyo kwa matajiri na wageni. Hati miliki itakomesha wavamizi wa ardhi na uuzaji hovyo ufanywao na familia na viongozi wa kijiji/Mtaa. Watu wa Kagera wana ardhi ambayo ina nyumba na mashamba ya midizi na miti ya matumizi ya familia. Kila mmoja anakata ,miti yake kwa kuni au mkaa. Hivyo mashamba yao waachiwe waendelee kulima ila pale watakapopimiwa serikali iangalie kuwa kila mmoja anayepewa ardhi ajenge kama sheria ya ardhi inavyosema yaani 60% ya plot na kubakiza 40% kwa mahitaji mengine ya choo, jiko, mabanda ya uwani na bustani sio kujenga 100% halafu hata pa kulima mbogambona  mtu hana kisha anabananisha feeder road anaweka kiosk cha biashara. Moto ukiwaka hakuna pa gari kupita au watu kupita kuuzima. Umefika hata vijijini kulazimishe ustaarabu uwepo hasa katika mipango miji na vijiji. Tuwache kuwa na majengo bananishi na squatters vijijini. Tuwe wastaarabu. Inapofika shule-kila shule iwe na space kubwa pamoja na mashamba kama ilivyokuwa wakati wa JK Nyerere. Mashamba ya waanfunzi kujifunza kilimo, kupanda miti kuzunguka shule na viwanja vya michezo sio Kiosk za biashara kila kona ya shule na mabada ya mambo mengi yanayoathiri elimu na mazingira ya shule.

5) Kamati ya kuhusisha wataalamu wa ardhi, mazingira, majengo na kuangalia ramani nzima na matumizi ya pesa muhimu sana kupunguza ufisadi ili kieleweke. Baada ay upimaji ardhi na ujenzi evaluation ifanyike kuona kipi kilipangwa na kimefanyika kipi at what cost na auditing muhimu. Zinazobakia kama ni hela au vifaa vitumike vipi. Pia kujenga makao ya wazee na vilema wasio na ndugu huko kijijini walelewe naUstawi wa Jamii.

6)Kama ni hela za kuwapa taslimu-kuepuka matumizi mabaya budi kupeleka NBC, NMB, CRDB kuwafungulia accounta hapo hapo kijijini na kuziingiza ktk account. Tumia vitambulisho vya Raia, Mpiga kura na vya vyama na kadi za kuzaliwa kwa walionavyo uonfdoe urasimu wa wao kwenda bank mbali kufungua account. Mpe kadi yake hapo hapo kijijini. Hufanyika hivyo katika Valuation and Resettlement Tanzania. Ukimpa hela taslimu-utata lipa kwa cheque na weka mashine za kuchukua hela ofisi mojawapo ya Kata na Tarafa ili banks hizo ziwe karibu. Ulizi wa mashine hizo muhimu viobaka wengi. Ukiwapa cash-watavamiwa na majambazi mpaka wageni wahamiaji ambao nao wameanza kupokea pesa za TASAF. Tujifunze kutokana na makosa yatokeayo maeneo mengine.

Kama Kawa
--------------------------------------------
On Thu, 13/10/16, 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

 Subject: [wanabidii] JANGA LIKIJA JUU YA JANGA: NANI ATASIMAMA KUELEZA?
 To: wanabidii@googlegroups.com
 Date: Thursday, 13 October, 2016, 22:22

 Mwezi mmoja uliopita tarehe 10
 September kulitokea tetemeko la ardhi na kuleta maafa katika
 Mkoa wa Kagera. Watu wasiozidi 19 walikufa, nyumba kadhaa
 zikaanguka na nyingine nyingi zikapata nyufa. Nyufa nyingine
 ni hatarishi kiasi nyumba hizo ni hatari kuzitumia na nyufa
 nyingine si hatarishi. Katika dharura hiyo miyndombinuu
 kadhaa iliharibika. Mfano ni shule kadhaa zilianguka,
 barabara zilipasuka, makanisa yalianguka na kadhalika.
 Nchi, serikali, balozi za nchi za nje, vyama vya siasa;
 mashirika mbalimbali na watu binafsi waliitikia kwa kutoa
 michango mbalimbali kwa lengo la kusaidia waathirika wa
 tetemeko hilo

 Niliwahi kufanya hesabu wakati huo nyumba zikiwa elfu sita
 zilizoathirika nikahesabu kama sh. Million 10 zingetumika
 kwa kila nyumba basi zingehitajika bilioni 60. Hazipo.
 Kati ya waathirika wapo waliokwisha maliza kurekebisha au
 kujenga upya nyumba zao kiasi athari za tetemeko kwao si
 hoja. Hii ni nafuu kwa kamati ya maafa.
 Wapo ambao wamejaribu na kukwama kwa sababu uwezo wao wa
 kujenga ni mdogo. Wapo ambao ni haki yao kukaa kimya na
 kusubiri msaada maaqna hawawezi kuzijenga.
 Misaada ambayo imetolewa hadi sasa si ile ya kurejesha
 majengo ya kuishi.
 Ninapopita maeneo yaliyoathirika nayaona yote ninayoyaeleza.
 Ninaona pia watu wanaoishi kwenye nyumba ambazo ni hatari
 kutokana na nyufa zilizotokea.
 Ninaamini halitakuwa jambo la kushangaza kama mvua zitakuja
 na upepo mkali mkoani Kagera. Lakini najiuliza mvua hiyo
 ikinyesha na kuzipiga na kuziangusha nyumba zilizopasuliwa
 na tetemeko na watu zaidi ya waliokufa kwa tetemeko wakafa;
 ni kiongozi gani atasimama kutoa maelezo? Rais, makamu wake,
 Waziri Mkuu au Mkuu wa Mkoa? Atawalaumu watu kwa kutumia
 nyumba hizo kwa sababu serikali ilishazitangaza kuwa
 mipasuko iliyotokea ni hatarishi? Jambo hili si la kucheza
 nalo. Kuna miundo mbinu inayowezesha kufika walipo
 waathirika. Nani ataelewa kuwa serikali ilitangulia
 kutengeneza miundo mbinu? Misaada iliyotolewa ilikuwa
 inatangazwa kuwa ni kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa
 Tetemeko. Ni sawa, Na shule kujengwa ni kuwasaidia
 waathirika. Lakini kweli baada ya wanafunzi kusambazwa shule
 nyingine inaeleweka kuwa watu waendelee kuishi kwenye mahema
 au nyumba mbovu kwa sababu kwanza tunajenga shule? Nani
 ataelewa? Nani ataelewesha? Serikali ilipotangaza kutoa
 sementi na mabati waathitika waliandaa mazingira kuanza
 kujenga. Nani kasema kila aliyevunjikiwa nyumba ana uwezo wa
 kujenga? Ninafikiri hili jambo si la kuchezea. Mvua inakuja
 na ipo itakayonyesha kwa vurugu. Ni kawaida. Lazima
 itazivuruga nyumba ninazozipitia kila mara. Kati ya wote
 wanaowajibika na kadhia iwezayo kutokea, Mkuu wa mkoa
 namuona akiwa hatarini. Ndiye aliye karibu. Kama wote
 wakibanwa watasema hatukujua. Yeye atasemaje. Lakini pia ni
 garama ndogo yeye kuwajibika/kuwajibishwa. Nyumba zikianguka
 na kuua watu mia rais atatangaza tu kuwa 'amemtumbua'
 kwa uzembe maana hakuweza kutumia misaada vizuri. Ndiye
 mwenyekiti wa kamati ya maafa. Baada ya hapo atachaguliwa
 mwingine mambo kwisha. Si kama kumuwajibisha waziri Mkuu
 ambaye baraza lote litafumuliwa. Lakini heri Mkuu wa Mkoa
 kutumbuliwa kwa sababu aliamua kutumia misaada kuwajengea
 nyumba badala ya kuacha wao kujijengea kuliko kutumbuliwa
 kwa sababu watu walifia kwenye nyumba zilizobomolewa na
 tetemeko huku akiwa na misaada chini yake. Ataeleweka kwa
 dhamira yake na kwa umma, Tusipuuze tahadhali kama hizi.
 Elisa Muhingo



  --

  Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

   

  Kujiondoa Tuma Email kwenda

  wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
 Utapata Email ya
  kudhibitisha ukishatuma

   

  Disclaimer:

  Everyone posting to this Forum bears the sole
 responsibility
  for any legal consequences of his or her postings, and
 hence
  statements and facts must be presented responsibly. Your
  continued membership signifies that you agree to this
  disclaimer and pledge to abide by our Rules and
  Guidelines.

  ---

  You received this message because you are subscribed to
 the
  Google Groups "Wanabidii" group.

  To unsubscribe from this group and stop receiving emails
  from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

  For more options, visit
 https://groups.google.com/d/optout.


  
    

  --

  Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

   

  Kujiondoa Tuma Email kwenda

  wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
 Utapata Email ya
  kudhibitisha ukishatuma

   

  Disclaimer:

  Everyone posting to this Forum bears the sole
 responsibility
  for any legal consequences of his or her postings, and
 hence
  statements and facts must be presented responsibly. Your
  continued membership signifies that you agree to this
  disclaimer and pledge to abide by our Rules and
  Guidelines.

  ---

  You received this message because you are subscribed to
 the
  Google Groups "Wanabidii" group.

  To unsubscribe from this group and stop receiving emails
  from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

  For more options, visit
 https://groups.google.com/d/optout.


 --
 Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 Kujiondoa Tuma Email kwenda
 wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
 Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

 Disclaimer:
 Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
 for any legal consequences of his or her postings, and hence
 statements and facts must be presented responsibly. Your
 continued membership signifies that you agree to this
 disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 ---
 You received this message because you are subscribed to the
 Google Groups "Wanabidii" group.
 To unsubscribe from this group and stop receiving emails
 from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
 For more options, visit
 https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.



--
J L Kamala

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment