Friday 14 October 2016

Re: [wanabidii] JANGA LIKIJA JUU YA JANGA: NANI ATASIMAMA KUELEZA?

Muhimu cha kufanya Elisa ni kwanza:
i) Kutumia wataalamu wa Ecology na wa masuala ya matetemeko ya ardhi kuangalia kama hilo eneo wanakoishi ni hatarishi kwa matetemeko na mafuriko.

2) Ikiwa ni hatarishi ni wazilikitokea tena litabomoa nyumba na kuingiza jamii ktk hasara. Hivyo budi watafute eneo la kuwajengea nyumba kwa kutumia NHC kwa kujenga nyumba ambazo hela zitatosha na kulingana na wingi wa watu katika familia kwa standard space kwani building regulation zipo. Kusiwe na mbanano. Hivyo itabidi kutafuta eneo na kufanya participatory land use planninh na kuwapa hati miliki ya makapo. Budi watoe fidia kwa ardhi ya kufaa watakayochukua kama sio ya serikali.

3) Afanyavyo kiongozi kuwajengea nyumba ni muhimu ila anajenga wapi panapofaa kuishi ukiangalia mazingira yasiyo hatarishi. Ukiwapa pesa hao baadhi wataanza kunywa Lubisi na baadhi ya walezi au watoto makanjanja wataanza kutaka kuzitumia vibaya. Ukiwapa vifaa baadhi watauza na kusepa mjini na kuacha vizee vikiteseka. Vibaka wapo pia ktk familia na ndiko kunakotoka akina scorpion, panya road na fisi na wengineo.

4) Mahali ambako palitokea tetemeko watakuwa wana mashamba yao wapewe Hati Miliki ya Kimila. Kule wanakopimiwa wapewe Hati Miliki ya Serikali na ipigwe muhuri-Haihamishiki bila ya kibali cha Waziri wa Ardhi. Hii itakomesha uuzaji wa ardhi hovyo kwa matajiri na wageni. Hati miliki itakomesha wavamizi wa ardhi na uuzaji hovyo ufanywao na familia na viongozi wa kijiji/Mtaa. Watu wa Kagera wana ardhi ambayo ina nyumba na mashamba ya midizi na miti ya matumizi ya familia. Kila mmoja anakata ,miti yake kwa kuni au mkaa. Hivyo mashamba yao waachiwe waendelee kulima ila pale watakapopimiwa serikali iangalie kuwa kila mmoja anayepewa ardhi ajenge kama sheria ya ardhi inavyosema yaani 60% ya plot na kubakiza 40% kwa mahitaji mengine ya choo, jiko, mabanda ya uwani na bustani sio kujenga 100% halafu hata pa kulima mbogambona mtu hana kisha anabananisha feeder road anaweka kiosk cha biashara. Moto ukiwaka hakuna pa gari kupita au watu kupita kuuzima. Umefika hata vijijini kulazimishe ustaarabu uwepo hasa katika mipango miji na vijiji. Tuwache kuwa na majengo bananishi na squatters vijijini. Tuwe wastaarabu. Inapofika shule-kila shule iwe na space kubwa pamoja na mashamba kama ilivyokuwa wakati wa JK Nyerere. Mashamba ya waanfunzi kujifunza kilimo, kupanda miti kuzunguka shule na viwanja vya michezo sio Kiosk za biashara kila kona ya shule na mabada ya mambo mengi yanayoathiri elimu na mazingira ya shule.

5) Kamati ya kuhusisha wataalamu wa ardhi, mazingira, majengo na kuangalia ramani nzima na matumizi ya pesa muhimu sana kupunguza ufisadi ili kieleweke. Baada ay upimaji ardhi na ujenzi evaluation ifanyike kuona kipi kilipangwa na kimefanyika kipi at what cost na auditing muhimu. Zinazobakia kama ni hela au vifaa vitumike vipi. Pia kujenga makao ya wazee na vilema wasio na ndugu huko kijijini walelewe naUstawi wa Jamii.

6)Kama ni hela za kuwapa taslimu-kuepuka matumizi mabaya budi kupeleka NBC, NMB, CRDB kuwafungulia accounta hapo hapo kijijini na kuziingiza ktk account. Tumia vitambulisho vya Raia, Mpiga kura na vya vyama na kadi za kuzaliwa kwa walionavyo uonfdoe urasimu wa wao kwenda bank mbali kufungua account. Mpe kadi yake hapo hapo kijijini. Hufanyika hivyo katika Valuation and Resettlement Tanzania. Ukimpa hela taslimu-utata lipa kwa cheque na weka mashine za kuchukua hela ofisi mojawapo ya Kata na Tarafa ili banks hizo ziwe karibu. Ulizi wa mashine hizo muhimu viobaka wengi. Ukiwapa cash-watavamiwa na majambazi mpaka wageni wahamiaji ambao nao wameanza kupokea pesa za TASAF. Tujifunze kutokana na makosa yatokeayo maeneo mengine.

Kama Kawa
--------------------------------------------
On Thu, 13/10/16, 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] JANGA LIKIJA JUU YA JANGA: NANI ATASIMAMA KUELEZA?
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thursday, 13 October, 2016, 22:22

Mwezi mmoja uliopita tarehe 10
September kulitokea tetemeko la ardhi na kuleta maafa katika
Mkoa wa Kagera. Watu wasiozidi 19 walikufa, nyumba kadhaa
zikaanguka na nyingine nyingi zikapata nyufa. Nyufa nyingine
ni hatarishi kiasi nyumba hizo ni hatari kuzitumia na nyufa
nyingine si hatarishi. Katika dharura hiyo miyndombinuu
kadhaa iliharibika. Mfano ni shule kadhaa zilianguka,
barabara zilipasuka, makanisa yalianguka na kadhalika.
Nchi, serikali, balozi za nchi za nje, vyama vya siasa;
mashirika mbalimbali na watu binafsi waliitikia kwa kutoa
michango mbalimbali kwa lengo la kusaidia waathirika wa
tetemeko hilo

Niliwahi kufanya hesabu wakati huo nyumba zikiwa elfu sita
zilizoathirika nikahesabu kama sh. Million 10 zingetumika
kwa kila nyumba basi zingehitajika bilioni 60. Hazipo.
Kati ya waathirika wapo waliokwisha maliza kurekebisha au
kujenga upya nyumba zao kiasi athari za tetemeko kwao si
hoja. Hii ni nafuu kwa kamati ya maafa.
Wapo ambao wamejaribu na kukwama kwa sababu uwezo wao wa
kujenga ni mdogo. Wapo ambao ni haki yao kukaa kimya na
kusubiri msaada maaqna hawawezi kuzijenga.
Misaada ambayo imetolewa hadi sasa si ile ya kurejesha
majengo ya kuishi.
Ninapopita maeneo yaliyoathirika nayaona yote ninayoyaeleza.
Ninaona pia watu wanaoishi kwenye nyumba ambazo ni hatari
kutokana na nyufa zilizotokea.
Ninaamini halitakuwa jambo la kushangaza kama mvua zitakuja
na upepo mkali mkoani Kagera. Lakini najiuliza mvua hiyo
ikinyesha na kuzipiga na kuziangusha nyumba zilizopasuliwa
na tetemeko na watu zaidi ya waliokufa kwa tetemeko wakafa;
ni kiongozi gani atasimama kutoa maelezo? Rais, makamu wake,
Waziri Mkuu au Mkuu wa Mkoa? Atawalaumu watu kwa kutumia
nyumba hizo kwa sababu serikali ilishazitangaza kuwa
mipasuko iliyotokea ni hatarishi? Jambo hili si la kucheza
nalo. Kuna miundo mbinu inayowezesha kufika walipo
waathirika. Nani ataelewa kuwa serikali ilitangulia
kutengeneza miundo mbinu? Misaada iliyotolewa ilikuwa
inatangazwa kuwa ni kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa
Tetemeko. Ni sawa, Na shule kujengwa ni kuwasaidia
waathirika. Lakini kweli baada ya wanafunzi kusambazwa shule
nyingine inaeleweka kuwa watu waendelee kuishi kwenye mahema
au nyumba mbovu kwa sababu kwanza tunajenga shule? Nani
ataelewa? Nani ataelewesha? Serikali ilipotangaza kutoa
sementi na mabati waathitika waliandaa mazingira kuanza
kujenga. Nani kasema kila aliyevunjikiwa nyumba ana uwezo wa
kujenga? Ninafikiri hili jambo si la kuchezea. Mvua inakuja
na ipo itakayonyesha kwa vurugu. Ni kawaida. Lazima
itazivuruga nyumba ninazozipitia kila mara. Kati ya wote
wanaowajibika na kadhia iwezayo kutokea, Mkuu wa mkoa
namuona akiwa hatarini. Ndiye aliye karibu. Kama wote
wakibanwa watasema hatukujua. Yeye atasemaje. Lakini pia ni
garama ndogo yeye kuwajibika/kuwajibishwa. Nyumba zikianguka
na kuua watu mia rais atatangaza tu kuwa 'amemtumbua'
kwa uzembe maana hakuweza kutumia misaada vizuri. Ndiye
mwenyekiti wa kamati ya maafa. Baada ya hapo atachaguliwa
mwingine mambo kwisha. Si kama kumuwajibisha waziri Mkuu
ambaye baraza lote litafumuliwa. Lakini heri Mkuu wa Mkoa
kutumbuliwa kwa sababu aliamua kutumia misaada kuwajengea
nyumba badala ya kuacha wao kujijengea kuliko kutumbuliwa
kwa sababu watu walifia kwenye nyumba zilizobomolewa na
tetemeko huku akiwa na misaada chini yake. Ataeleweka kwa
dhamira yake na kwa umma, Tusipuuze tahadhali kama hizi.
Elisa Muhingo



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and
hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to
the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.


 
   

--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole
responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and
hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to
the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com 
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment