Thursday, 11 August 2016

[wanabidii] Fw: Mtanzania asiye na ndugu Kafariki Denmark

UPDATES ZA MTANZANIA MWENZETU ALIYEFARIKI MPAKA SASA:

Tunawatafuta ndugu wa Samuel John Asheli aka Rasta TZ, aliyefariki Denmark tarehe 05.08.2016, baada ya kuugua kwa muda mrefu. Marehemu amekaa Denmark kwa miaka 10.

Marehemu hakuwa na ndugu hapa Denmark wala hakuwa na utaratibu wa kujumuika na watanzania wenzake. Hivyo, hatuna picha yake.

Taarifa tulizozipata kutoka kwa watu waliokuwa karibu na marehemu zinasema kuwa, marehemu alikuwa na mtoto wa miaka 20 huko Italy na ndugu zake wako Tanzania. Mara ya mwisho, marehemu alituma barua kwenda Tanzania miezi miwili kupitia S.L.P 70, Kisutu, Dar Es Salaam. Kama unamfahamu mtu anayemiliki/tumia S sanduku hili la Posta, tafadhali mwambie awasiliane na jumuia ya watanzania waishio Denmark kupitia:

Fortunatus Bundu +4528106145 (Mwenyekiti)
Tambwe Tumba +61283381 (Katibu)

NB: Manispaa aliyokuwa anaishi marehemu imepanga kufanya mazishi wiki ijayo. Tafadhali mara upatapo ujumbe huu, tunaomba uusambaze kwenye ma-group mengine ili ndugu zake wapate taarifa za msiba na ikiwezekana waweze kuhudhuria mazishi yake.0 comments:

Post a Comment