Tuesday, 12 April 2016

Re: [wanabidii] Rais Magufuli Wabadilishe Watanzania - Umaskini ni Hulka

Well said. I should share this

Sent from my HTC Phone

----- Reply message -----
From: "'ananilea nkya' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Subject: [wanabidii] Rais Magufuli Wabadilishe Watanzania - Umaskini ni Hulka
Date: Tue, Apr 12, 2016 22:42

Mkinga mawazo yako mali kweli kweli. Hongera.    Ananilea Nkya   E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com    --------------------------------------------  On Tue, 4/12/16, 'Bart Mkinga' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:     Subject: [wanabidii] Rais Magufuli Wabadilishe Watanzania - Umaskini ni Hulka   To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>   Date: Tuesday, April 12, 2016, 8:27 PM      Kuna    wakati niliwahi kusoma taarifa moja ya hulka ya mtu mweusi.   Hulka yake    kubwa ni kupenda kutumia kuliko kuzalisha. Kule Marekani   kulifanyika    utafiti juu ya mtu mweusi. Wamarekani weusi wanachangia 6%   ya GDP ya    Marekani lakini wanachangia 10% katiika matumizi. Matajiri   wakubwa weusi    Marekani ni wasanii, pesa yao nyingi wanayopata wanaenda   kutumia kwa    kununua magari ya kifahari, nguo za kifahari na majumba ya   kifahari    kwenye makampuni ya Wamarekani weupe.   Wazungu    tunaowalaumu kuwa wanatunyonya ni makini sana katika   matumizi, na wapo    sensitive sana kwa kila linalotokea. Mzungu anaweza kuwa na   akiba ya    U$500,000 bank lakini leo akisikia kuwa mataifa   yanayozalisha mafuta kwa    wingi Duniani yanakutana kupanga mbinu za kupandisha bei ya   mafuta,    kesho yake anaanza kubana matumizi kwenye maeneo mbalimbali,   Mzungu    akisikia kuwa kuna uwezekano wa kutokea upungufu wa chakula,   kama kila    siku jioni alikuwa anakula hotelini, anaanza kula sandwichi   (mkate    uliowekwa mboga za majani, nyanya na mayai). Kama alikuwa   amepanga    kufunga arusi, anaweza kuahirisha au kupunguza waalikwa   mpaka kufikia    watu wanne tu.      Lakini    Mtanzania anasikia kuwa mwaka huu kuna ukame, atasikia kuwa   mafuta    yamepanda bei, atasikia MCC wamesimamisha msaada, Magufuli   ameongeza    kodi kwenye kila aina ya mapato, n.k., maisha yake yapo pale   pale.    Mtanzania ataendelea kunwa bia 10 kila siku kama alivyozoea,   ataendelea    kufanya kitchen party, ataendelea kufanya send off na arusi   ya kifahari    yenye waalikwa wasiopungua 200, arusi ambayo maandalizi yake   yataanza    mwezi April wakati arusi ni mwezi Agosti. Mtanzania anakuja   kushtuka    wakati anapoona anataka kwenda hospitali lakini hana hela,   anatakiwa    kulipa ada ya mwanae lakini hela hakuna, anatakiwa kulipa   pango lakini    hana hela, hapo ndiyo anaanza kusema kuwa tubane matumizi,   unabana    matumizi gani wakati huna hela? Maana hata usipotaka kubana   matumizi,    ukweli ni kwamba huna hela ya kutumia.   Kinachomfanya    mtu kuwa tajiri siyo kile apatacho bali ni kile   anachokitunza. Huu ni    wakati wa makasisi na washekhe kuwaambia waumini umuhimu wa   kuwa    watunzaji wa mapato yao kwaajili ya manufaa ya familia zao.   Wawashawishi    waumini wao kuachana na sherehe kama za kitchen party na   send off maana    siyo hitaji la kiimani/kiibada. Wahamasishwe kutotaka   sherehe za    kifahari za arusi ambazo kimsingi haziongezi chochote.   Ubarikio,    ubatizo, kipaimara ni ibada zisizolazimisha sherehe. Wale   wanaotaka    kuyafanya hayo nao waambiwe wasiwachangishe watu wengine   maana kuna watu    hawana hela lakini hawana ujasiri wa kusema hawana uwezo wa   kuchanga.    Viongozi wa siasa nao wawahamasishe watu kuachana na sherehe   zisizo na    umuhimu.       Rais    Magufuli ameonesha njia kwa kutosherehekea sikukuu za   kiserikali,    nadhani anaogopa kufuta hizi za kijamii na kidini kwa hofu   tu ya    kuambiwa anaingilia mambo ya kiimani au kijamii. Kama hawezi   kuzifuta    basi aseme tu kuwa anashauri sikukuu hizi zisherehekewe kwa   kusali na    uzalishaji mali tu.      Wito wangu ni kwamba tutumie muda mwingi kuzalisha   kuliko kutumia.   Tunamwomba    Rais Magufuli serikali yake itumie muda mwingi kuwasaidia   Watanzania    kuwa wazalishaji kuliko kutumia muda mwingi kukusanya kodi.   Iwasaidie    Watanzania wawe wazalishaji na baadaye ipate kodi ya   kutosha. Ni wakati    wa wataalam wa biashara, wataalam wa uwekezaji, wataalam wa   kilimo,    wataalam wa madini, wataalam wa uvuvi, n.k.  kufanya   kazi kufa na kupona    kuwafanya Watanzania watengeneze faida katika shughuli zao   za kiuchumi    ili serikali iwe na uhalali wa kukusanya kodi. Shida kubwa   tuliyo nayo    tuna maafisa biashara wasiojua biashara, tuna maafisa kilimo   wasiojua    kilimo, tuna wataalam wa madini wasioyajua madini, tuna   maafisa    uwekezaji wasioujua uwekezaji, tuna maafisa uvuvi wasioujua   uvuvi, n,k.   Tuna    maafisa mifugo ambao akiachishwa kazi wanashindwa kufuga   hata kuku 500.    Tuna wahindisi ambao wakiachishwa kazi wanashindwa   kutengeneza hata    daraja la upana wa mita 3. Tuna wakuu wa mikoa wakiachishwa   kazi    wanashindwa kuwa na miradi ya kuwawezesha kupata japo   shilingi 500,000    kwa mwezi ingawa walipokuwa wakuu wa mikoa walihimiza vijana   wanaomaliza    vyuo vikuu wajiajiri.   Sasa    ni wakati wa serikali ya Magufuli kuwapima wataalam kwa   yale    wanayoyafanya na siyo kwa uwingi wa vyeti au miaka ya kukaa   ofisini.    Rais awaulize wataalam hawa ni kwa namna gani wamewasaidia   wazalishaji    wa sekta mbalimbali kuwa wazalishaji wenye tija. Kama   serikali haina    msaada kwa wazalishaji, inakosa uhalali wa kukusanya kodi.   Ifike mahali    serikali iwe na ujasiri wa kusema, 'wewe mkulima   tulikutoa kutoka    uzalishaji wa magunia 10 ya maharage mpaka magunia 100, kwa   nini hutaki    kulipa kodi? Wewe mfanyabishara tulikutoa kutoka kuwa   muagizaji wa    midoli kutoka China mpaka kuwa mmiliki wa kiwanda cha   mashati, kwa nini    hutaki kulipa kodi?, n.k.      Uhalali wa serikali kudai kodi utokane na   uwezeshaji kwa wananchi wake.   Nchi    hii inatakiwa kuanza upya maana hata mitazamo, fikra na   vitendo vya    viongozi na umma kwa ujumla, siyo vinavyotuelekeza kwenye   maendeleo.    Wakati Rais unapotumbua majipu, kazania pia elimu ya   kubadilisha hulka    ya watu kutoka kwenye jamii ya watumiaji na kuwa jamii ya   wazalishaji.    Hakuna moral right ya kutumia bila uzalishaji. Na serikali   pia iwe na    fikra hiyo. Serikali inapoenda kuwabana walipa kodi ijiulize   pia    imewasaidia kwa namna gani katika biashara zao. Halmashauri   zinapoweka    vizuizi barabarani vya ushuru wa mazao, zijiulize zimesaidia   nini katika    uzalishaji wao.   HUU NI WAKATI WA KUVUNA   ULICHOPANDA.   Mkinga Msambichaka            --       Send Emails to wanabidii@googlegroups.com             Kujiondoa Tuma Email kwenda       wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya   kudhibitisha ukishatuma             Disclaimer:      Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility   for any legal consequences of his or her postings, and hence   statements and facts must be presented responsibly. Your   continued membership signifies that you agree to this   disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.      ---       You received this message because you are subscribed to the   Google Groups "Wanabidii" group.      To unsubscribe from this group and stop receiving emails   from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.      For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.    --   Send Emails to wanabidii@googlegroups.com    Kujiondoa Tuma Email kwenda   wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma    Disclaimer:  Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.  ---   You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.  To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.  For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.  

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment