Tuesday, 12 April 2016

Re: [wanabidii] Rais Magufuli Wabadilishe Watanzania - Umaskini ni Hulka

Mkinga mawazo yako mali kweli kweli. Hongera.

Ananilea Nkya
 E-mail:ananilea_nkya@yahoo.com

--------------------------------------------
On Tue, 4/12/16, 'Bart Mkinga' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] Rais Magufuli Wabadilishe Watanzania - Umaskini ni Hulka
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Tuesday, April 12, 2016, 8:27 PM

Kuna
wakati niliwahi kusoma taarifa moja ya hulka ya mtu mweusi.
Hulka yake
kubwa ni kupenda kutumia kuliko kuzalisha. Kule Marekani
kulifanyika
utafiti juu ya mtu mweusi. Wamarekani weusi wanachangia 6%
ya GDP ya
Marekani lakini wanachangia 10% katiika matumizi. Matajiri
wakubwa weusi
Marekani ni wasanii, pesa yao nyingi wanayopata wanaenda
kutumia kwa
kununua magari ya kifahari, nguo za kifahari na majumba ya
kifahari
kwenye makampuni ya Wamarekani weupe.
Wazungu
tunaowalaumu kuwa wanatunyonya ni makini sana katika
matumizi, na wapo
sensitive sana kwa kila linalotokea. Mzungu anaweza kuwa na
akiba ya
U$500,000 bank lakini leo akisikia kuwa mataifa
yanayozalisha mafuta kwa
wingi Duniani yanakutana kupanga mbinu za kupandisha bei ya
mafuta,
kesho yake anaanza kubana matumizi kwenye maeneo mbalimbali,
Mzungu
akisikia kuwa kuna uwezekano wa kutokea upungufu wa chakula,
kama kila
siku jioni alikuwa anakula hotelini, anaanza kula sandwichi
(mkate
uliowekwa mboga za majani, nyanya na mayai). Kama alikuwa
amepanga
kufunga arusi, anaweza kuahirisha au kupunguza waalikwa
mpaka kufikia
watu wanne tu.

Lakini
Mtanzania anasikia kuwa mwaka huu kuna ukame, atasikia kuwa
mafuta
yamepanda bei, atasikia MCC wamesimamisha msaada, Magufuli
ameongeza
kodi kwenye kila aina ya mapato, n.k., maisha yake yapo pale
pale.
Mtanzania ataendelea kunwa bia 10 kila siku kama alivyozoea,
ataendelea
kufanya kitchen party, ataendelea kufanya send off na arusi
ya kifahari
yenye waalikwa wasiopungua 200, arusi ambayo maandalizi yake
yataanza
mwezi April wakati arusi ni mwezi Agosti. Mtanzania anakuja
kushtuka
wakati anapoona anataka kwenda hospitali lakini hana hela,
anatakiwa
kulipa ada ya mwanae lakini hela hakuna, anatakiwa kulipa
pango lakini
hana hela, hapo ndiyo anaanza kusema kuwa tubane matumizi,
unabana
matumizi gani wakati huna hela? Maana hata usipotaka kubana
matumizi,
ukweli ni kwamba huna hela ya kutumia.
Kinachomfanya
mtu kuwa tajiri siyo kile apatacho bali ni kile
anachokitunza. Huu ni
wakati wa makasisi na washekhe kuwaambia waumini umuhimu wa
kuwa
watunzaji wa mapato yao kwaajili ya manufaa ya familia zao.
Wawashawishi
waumini wao kuachana na sherehe kama za kitchen party na
send off maana
siyo hitaji la kiimani/kiibada. Wahamasishwe kutotaka
sherehe za
kifahari za arusi ambazo kimsingi haziongezi chochote.
Ubarikio,
ubatizo, kipaimara ni ibada zisizolazimisha sherehe. Wale
wanaotaka
kuyafanya hayo nao waambiwe wasiwachangishe watu wengine
maana kuna watu
hawana hela lakini hawana ujasiri wa kusema hawana uwezo wa
kuchanga.
Viongozi wa siasa nao wawahamasishe watu kuachana na sherehe
zisizo na
umuhimu.

Rais
Magufuli ameonesha njia kwa kutosherehekea sikukuu za
kiserikali,
nadhani anaogopa kufuta hizi za kijamii na kidini kwa hofu
tu ya
kuambiwa anaingilia mambo ya kiimani au kijamii. Kama hawezi
kuzifuta
basi aseme tu kuwa anashauri sikukuu hizi zisherehekewe kwa
kusali na
uzalishaji mali tu.

Wito wangu ni kwamba tutumie muda mwingi kuzalisha
kuliko kutumia.
Tunamwomba
Rais Magufuli serikali yake itumie muda mwingi kuwasaidia
Watanzania
kuwa wazalishaji kuliko kutumia muda mwingi kukusanya kodi.
Iwasaidie
Watanzania wawe wazalishaji na baadaye ipate kodi ya
kutosha. Ni wakati
wa wataalam wa biashara, wataalam wa uwekezaji, wataalam wa
kilimo,
wataalam wa madini, wataalam wa uvuvi, n.k.  kufanya
kazi kufa na kupona
kuwafanya Watanzania watengeneze faida katika shughuli zao
za kiuchumi
ili serikali iwe na uhalali wa kukusanya kodi. Shida kubwa
tuliyo nayo
tuna maafisa biashara wasiojua biashara, tuna maafisa kilimo
wasiojua
kilimo, tuna wataalam wa madini wasioyajua madini, tuna
maafisa
uwekezaji wasioujua uwekezaji, tuna maafisa uvuvi wasioujua
uvuvi, n,k.
Tuna
maafisa mifugo ambao akiachishwa kazi wanashindwa kufuga
hata kuku 500.
Tuna wahindisi ambao wakiachishwa kazi wanashindwa
kutengeneza hata
daraja la upana wa mita 3. Tuna wakuu wa mikoa wakiachishwa
kazi
wanashindwa kuwa na miradi ya kuwawezesha kupata japo
shilingi 500,000
kwa mwezi ingawa walipokuwa wakuu wa mikoa walihimiza vijana
wanaomaliza
vyuo vikuu wajiajiri.
Sasa
ni wakati wa serikali ya Magufuli kuwapima wataalam kwa
yale
wanayoyafanya na siyo kwa uwingi wa vyeti au miaka ya kukaa
ofisini.
Rais awaulize wataalam hawa ni kwa namna gani wamewasaidia
wazalishaji
wa sekta mbalimbali kuwa wazalishaji wenye tija. Kama
serikali haina
msaada kwa wazalishaji, inakosa uhalali wa kukusanya kodi.
Ifike mahali
serikali iwe na ujasiri wa kusema, 'wewe mkulima
tulikutoa kutoka
uzalishaji wa magunia 10 ya maharage mpaka magunia 100, kwa
nini hutaki
kulipa kodi? Wewe mfanyabishara tulikutoa kutoka kuwa
muagizaji wa
midoli kutoka China mpaka kuwa mmiliki wa kiwanda cha
mashati, kwa nini
hutaki kulipa kodi?, n.k.

Uhalali wa serikali kudai kodi utokane na
uwezeshaji kwa wananchi wake.
Nchi
hii inatakiwa kuanza upya maana hata mitazamo, fikra na
vitendo vya
viongozi na umma kwa ujumla, siyo vinavyotuelekeza kwenye
maendeleo.
Wakati Rais unapotumbua majipu, kazania pia elimu ya
kubadilisha hulka
ya watu kutoka kwenye jamii ya watumiaji na kuwa jamii ya
wazalishaji.
Hakuna moral right ya kutumia bila uzalishaji. Na serikali
pia iwe na
fikra hiyo. Serikali inapoenda kuwabana walipa kodi ijiulize
pia
imewasaidia kwa namna gani katika biashara zao. Halmashauri
zinapoweka
vizuizi barabarani vya ushuru wa mazao, zijiulize zimesaidia
nini katika
uzalishaji wao.
HUU NI WAKATI WA KUVUNA
ULICHOPANDA.
Mkinga Msambichaka



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment