Monday, 11 April 2016

RE: [wanabidii] Rais Magufuli Urais ni Wako Chukua Hatua

Msambichaka,
Njia ipo, kama ulivyoonyesha katika mchango wako.
Kuna maamuzi yetu yanaweza kutunyima misaada ila yakawa na tija kwetu, tunapofikia hali hiyo inabidi tuwe wabunifu kama tunavyochangia wengi!

Hatuna maana ya kuwa na kiburi kiasi cha kuimbia dunia "we are on our own… ", wala hatuwezi kufukuza wawekezaji hovyo kama alivyofanya Grandpa Robby!!??  Tutakaa tupange kodi zetu, tuboreshe utaratibu wetu wa mikataba ya nchi na uwekezaji KWA kuangalia faida zetu na wao pia. KAMA watashindwa itabidi wawaachie wengine wanaoweza!! Hatuwezi kufanya makosa kama GrandPa.

Tuungane, tuwe kitu kimoja, inapotokea binadam wenzetu wa nje wakapinga maendeleo yetu kwa kukosoa taratibu, tamaduni au sera nzuri tulizojiwekea, tuhangaike mpaka tupate namna ya kusonga kama ulivyotoa ushauri bora.

Kuna mengi yanaendelea kati ya uliyotaja, mengine yamesemwa na Mzee Muhingo na wengineo, na pia leo;
1. Mkuu wa Mkoa amesimamishwa kazi baada ya kushindwa kubaini wafanyakazi hewa 45.
2. Kuna taarifa ya kodi ya wakulima wa korosho kupunguzwa huko kusini, sina chanzo cha taarifa hii ila ni hatua nzuri kama ina ukweli.

Na kuna mengi zaidi yanakuja, tusubiri.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment