Thursday, 14 April 2016

Re: [wanabidii] Ni Afadhali Mtu Mmoja Afe

Nikijikita kwwa maneno aliyoyatumia Kardinali mimi nitafikiri kuwa hawa wawili walikuwa wanaongea juu ya mtu fulani ambaye Rais anasita kumchukulia hatua. Kardinali akamshauri kuwa ''Heri kumtosa (kufa) huyo kuliko kulinyima (kuteketea) haki taifa.
Nani haoni yanayotokea? mathalan: Polisi kusita kuleta mkataba unaoonyesha mabilioni yameliwa. Nani anajua kama mkataba ukiletwa mbele kuna mtu ataumbuka? kama wawili hawa waliona kuumbuka huko ni 'kufa' kwa nini Kardinali asimshauri kumuumbua huyo kuliko bilioni 37 kuyeyuka kama pelemende kwenye ulimi? Kwa ufupi sijatafsiri 'kufa' na ''kuteketea' kama kifo hasa kama cha Sokoine. Au nimepotea?
Elisa
--------------------------------------------
On Thu, 4/14/16, 'Bart Mkinga' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] Ni Afadhali Mtu Mmoja Afe
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, April 14, 2016, 11:22 AM

Magazeti
leo yameandika kile alichokisema Mwadhama Polycarpo Kadinali
Pengo wakati wa ibada ya kumbukumbu ya Hayati Edward Moringe
Sokoine aliyefariki kwenye ajali ya gari 12 Aprili 1984. Kwa
wale ambao walikuwa hawajazaliwa, ni kwamba kifo cha Sokoine
ni kifo kilicholeta simanzi kubwa kwa karibia Watanzania
wote kuanzia tuliokuwa wadogo wakati huo mpaka kwa wakubwa.
Na watu wengi mpaka leo hawaelewi ilitokeaje gari ya Waziri
Mkuu kugongwa na gari nyingine, mbele kukiwa na magari,
nyuma kukiwa na magari, Waziri Mkuu akiwa amekaa kiti cha
nyuma, lakini akafariki yeye pekee yake. Lakini kwa sababu
ya heshima na imani kubwa ambayo Watanzania tulikuwa nayo
kwa kiongozi wetu mkuu, Mwalimu Nyerere ambaye naye msiba
huo ulimchanganya sana hadi kulia hadharani, hatukuhoji
zaidi maana katika hotuba yake ya simanzi kubwa alituambia,
'Watanzania tukubali kuwa Sokoine amefariki kwa ajali ya
gari', wote tuliyachukua maneno hayo kwa imani kubwa
mpaka leo. Mungu amjalie raha ya milele marehemu Sokoine
kutokana na mapenzi yake na matumizi ya vipawa vyake
alivyopewa na mwenyezi Mungu kwaajili ya faida ya watu
wanyonge na maskini.
Ni kwenye ibada hiyo ya Kumkumbuka Hayati Sokoine
ndipo Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo alipoeleza kuwa Rais
Magufuli akiwa Chato alimpigia simu, na kati ya mambo ambayo
Rais Magufuli alimwambia yeye Kadinali ni kuwa, 'Kama
ningejua Urais ndiyo hivi nisingegombea', naye Kadinali
akamwambia Rais, 'Ni afadhali mtu mmoja afe lakini Taifa
lisiteketee'.
Wengi tunaendelea kutafakari, ni nini hawa watu
wawili waliongea mpaka kufikia huko? Japo ni rahisi kusema
kuwa kwa mzalendo wa kweli, huwa yupo tayari kufa kwaajili
ya watu wengine lakini kifo ni kigumu na bahati nzuri
hutokea bila ya kuwa na taarifa ya kabla. Sisi wengine
tutaendelea kuomba kusiwepo na wa kufa na pia Taifa
lisiteketee.
Binafsi ningekataa tamaa kama ningesikia kuwa Rais
Magufuli alimwambia Kadinali kuwa anamshukuru Mungu
amemsaidia kuwa Rais na sasa anafurahia nafasi aliyopewa ya
kuwaongoza Watanzania. Tafsiri rahisi ingekuwa hajali shida
za wananchi. Nchi hii ina watu asilimia kubwa wanaoishi kwa
shida na kwa kubahatisha kuliko idadi ya wenye uhakika wa
maisha. Kuna watu wanakufa muda usio wao kwa sababu ya
kukosa matibabu, kupata matibabu duni au kutibiwa kwa dawa
zilizo chini ya viwango. Kuna watu wanakufa kila siku
kwaajili za magari, pikipiki, mitumbwi na basikeli kwa
sababu ya udini wa vyombo wanavyosafiria, barabara mbaya,
ukosefu wa wataalam na vyombo vya uokoaji, n.k. Lakini pia
kuna watu wasiopata chakula cha kutosha au chakula bora,
kuna watu wana makazi duni kabisa, kuna watu wanafikiria ni
kwa namna gani watanunua hata blanketi au shati. Kuna watoto
pia ambao Mungu kawajalia vipaji mbalimbali lakini kutokana
na umaskini wa wazazi wao kamwe vipaji vyao havitakuja
kuonekana.
Hayo yote yanatokea wakati tukiwa na rasilimali
ambazo kila mmoja anazijua. Hayo yote yanatokea Tanzania
ikiwa na uongozi wa kwake yenyewe kwa zaidi ya miaka 50.
Hayo yote yanatokea tukijidai kuwa tuna uongozi bora, sera
na mipango mizuri ya uchumi, tuna sheria na vyombo vya
kusimamia utawala wa sheria, vyombo vya kusimamia maadili ya
uongozi wa umma, tuna taasisi mbalimbali za kusimamia
mipango ya kuondoa umaskini usiondoka. n.k.
Kama miaka yote tumekuwa na hayo yote lakini nchi
haikupiga hatua, ina maana vyombo hivyo ama vyote au vilivyo
vingi vina matatizo makubwa. Na mahali pa kuanzia siyo
kuviboresha bali kuviunda upya vikiwa na maelekezo mapya,
sheria mpya za kuviendesha na za kuvisimamia. Ili kuweza
kuyafanya haya kuna watu wanatakiwa kuondolewa, na kuna watu
wapya wenye fikra mpya wanatakiwa kuingizwa. Na hapa ndipo
ugumu wa kazi ya Urais unapokuja.
Maana wanaotakiwa kuondolewa ni watu ambao nyuso
zao siyo ngeni kwa Rais Magufuli. Wengine ni makada wa Chama
aliowafahamu kwa miaka mingi. Wengine ni marafiki
aliowafahamu kwa miaka mingi. Wengine huenda waliwahi kuwa
wakubwa zake katika utumishi wa umma, wengine ndugu au
marafiki wa viongozi wenzake. Wengine ni watu aliowategemea
sana kuwa msaada katika uongozi wake lakini anagundua kuwa
siyo msaada bali ni 'majipu'. Kuweza kuwachukulia
watu wa karibu yako, ambao sura na sauti zao unazijua, kwa
faida ya watu ambao hata majina yao huyajui, inahitaji roho
ya pekee, na roho hiyo iwe ya Kimungu.
Mheshimiwa Membe aliwahi kudokeza ilivyo ngumu
kumchukulia hatua mtu unayemfahamu na uliyemteua
mwenyewe.
Lakini tunachoweza kumwambia Mheshimiwa Rais ni
kuwa utendaji bora hupimwa katika ugumu na siyo katika
urahisi. Ni aheri amegundua mapema kuwa kazi ya Urais ni
ngumu, hasa unapoongoza nchi ambayo mifumo mbalimbali
haifanyi kazi, sera zipo kwenye mafaili lakini hazifanyiwi
kazi, sheria zipo kwenye makabrasha lakini zinapindishwa kwa
namna watu wenye malaka wanavyotaka, n.k.
Jambo la kujiuliza, je watendaje wengine wote nao
wanatambua kuwa kazi zao ni ngumu? Mawaziri wote wanatambua
kuwa uwaziri ni kazi ngumu? Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa
Wilaya wanatambua kuwa kazi yao ni ngumu? Polisi wanatambua
kuwa kuwalinda wananchi, tena kwa haki bila upendeleo ni
kazi ngumu? Mahakama zinatambua kuwa kutoa hukumu kwa wakati
wake na kwa haki ni kazi ngumu? Mifuko ya kijamii wanajua
kuwahakikishia maisha mazuri wanachama wao badala ya
kuhangaika na majengo ya kifahari yasiyowasaidia moja kwa
moja wanachama wao ni kazi ngumu? Madaktari wanatambua kuwa
kuwahudumia watanzania kwa upendo na uadilifu ni kazi ngumu?
Au hawa wengine wanasali na kumshukuru Mungu kuwaweka mahali
walipo?






--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment