Thursday, 1 January 2015

Re: [wanabidii] WILLIAM HAULE ATANGAZA RASMI NIA YA KUGOMBEA UBUNGE MWAKA HUU 2015

Kijana wa miaka 24 awe amefanya kitu tangiable?kwa mradi huu na mtizamo huu ni mafisadi tu ndio wataingia bungeni...Nyerere alipopewa nchi hii aliaminiwa tu na watanzania..na wakampa. Talenti ya mtu ya uongozi inaonekana tu ali mradi watazamaji watake kutazama. Kuanza kujipitisha na kutoa vimisaada vya mipira..vimfuko vya cement nk ni mbinu za kuwahadaa wananchi kwa kuwa tu unataka kitu fulani kwao. Juzijuzi tu Godfrey Mgimwa amepewa ubunge alikuwa amefanya kitu gani tangiable?...Mtu wa kuulizwa amefanya ninj ndio achaguliwe ni aliye madarakani na sio kijana huyu...Ngupula

'Reuben Mwandumbya' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Haule;
Sikukatishi tamaa lkn wewe binafsi inatakiwa ujipe moyo mkuu kwanza,mana mlango unaotaka kuingilia upo imara huwezi kuuvunja kwa jiwe la fatuma,hii ni kwa maono yangu.
Kumbuka wewe ndo unaanza,sina hakika km umeshafanya llt tangible kwa Wana ludewa,Watz sasa ni welevu wanapima utendaji sio maneno.
Kazi mbele yako ni ya ukweli,usiwe mwoga na kukata tamaa mapema,hata usipopata mwaka huu uwe unaendelea kupambana for future mana Deo sio wa milele,tupo pamoja na kila la kheri.


Sent from Huawei Mobile

'ngupula' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Jimbo la ludewa ndio linakaliwa na deo filikunjombe? kama ni hivyo jitie moyo na ukajaribu....Deo ni moja ya wabunge wazur sana wa bunge la 2010...2014...kwa mtazamo wa wengi..Ngupula

'amon mkoga' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Una hela ya kampeni watakuchuja asubuhi tu.
 
AMON MKOGA



On Thursday, January 1, 2015 1:20 AM, Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com> wrote:


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
WILLIAM HAULE ATANGAZA RASMI NIA YA KUGOMBEA UBUNGE MWAKA HUU 2015
Mimi William Haule, kijana wa miaka 24, mhitimu wa Chuo Kikuu Dar es Salaam katika fani ya Sayansi ya Siasa na Utawala, mwanadiplomasiamchambuzi wa masuala ya siasa, leo tarehe 01/01/2015, nachukua fursa hii kutangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Ludewa katika mwaka huu wa uchaguzi 2015.
Hii ni mara yangu ya kwanza kutangaza kuwa nitagombea ubunge Jimbo la Ludewa, kwa kuwa nimeombwa sana na vijana, wazee wa vijiji mbalimbali vya jimbo la Ludewa, na ni mara nyingi nimekuwa nikiwaambia bado muda, lakini sasa umebaki muda mfupi hivyo niseme tu na kuwahakikishia kuwa nitagombea. 
Kwa kuwa uongozi ni mbio za kupokezana vijiti. Naaamini katika kutoa mchango wangu juu ya maendeleo ya jamii kuliko kusubiri kufanyiwa nini na Taifa langu. (kama alivyowahi kusema raisi wa zamani wa marekani Bw. John F. Kennedy).
Kasi ya maendeleo ya Ludewa hairidhishi na matatizo mengi ya msingi hayapatiwi ufumbuzi. Kero zinazowakabili watu wa Ludewa ni nyingi na zinahitaji mtu mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri na kubuni miradi mbalimbali itakayoweza kuharakisha maendeleo ya Ludewa. Wananchi wa Ludewa wanahitaji kuwa na kiongozi mwenye kupenda maendeleo, mwenye fikra mbadala na mwenye uwezo wa kuanzisha msukumo mpya wa kasi ya maendeleo kulingana na kero zao na vipaumbele vya kisera na kimikakati vya kiwilaya na kitaifa. Kuna mambo mengi hayajakamilika na utekelezaji wake unalegalega.
Kwa kuyaangalia yote haya, nimetafakari kwa umakini na kujipima uwezo wangu, na nimeonelea nianze kwa vitendo ili niwe chachu ya mabadiliko kwa watu wa Ludewa, ambako ndipo nilipozaliwa. Charity begins at home, na ndo maana nimeamua kuwania ubunge wa Ludewa ili nishiriki kikamilifu na kwa ukaribu zaidi pamoja na wana Ludewa wenzangu katika kuzikabili changamoto za maendeleo katika jimbo la Ludewa kwa spidi na kwa ubunifu wa hali ya juu, maana mimi kila nikiiangalia Ludewa, sioni matatizo au vikwazo vya maendeleo, bali naona fursa tu za kuleta mabadiliko. Japokuwa Ludewa ina fursa nyingi, na ni mojawapo ya wilaya kongwe, kasi yake ya maendeleo haiendani na fursa zilizopo.
Ni matarajio yangu kuwa wananchi wa Ludewa tutaungana pamoja kupata mtu stahiki anaye tambua kero na matatizo yetu lakini pia mwenye mikakati madhubuti ya kukabiriana nayo. 
Kuna umuhimu mkubwa kwa viongozi mahiri na wenye nia thabiti ya kuwatumikia watu wajitokeze popote walipo na waje kuongeza nguvu kwa taifa letu ili tuweze kupamban

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment