Sunday 1 June 2014

[wanabidii] Re: [Mabadiliko] Profesa Muhongo anapata wapi jeuri hii?

Jeuri ya Prof. Muhongo inatokana na.
1. Yeye anajiona ni mtu msomi na kuwa ni mtu muhimu kuliko maprofesa wengine kwa kuwa aliteuliwa na rais kuwa Mbunge na kuwa Waziri.
2. Yeye akiwa Profesa hajui kuitumia elimu yake kulingana na mazingira na jamii inayomzunguka.
3.Yeye limbukeni wa nafasi ya uwaziri na hakutegemea kuwa atakuwa waziri ngawa ni msomi.
4. Zarau ni asili yake ndio maana hukuweza kuchukuwa jukumu la kuomba ridhaa ya uongozi kutoka kwa wananchi, mtu mwenye kueshimu taaluma yake hawezi akafuatilia taaluma za watu wengine, na kufanya hivyo hajiamini na usomi wake.
5, Uchanga wake katika nyanja ya kisiasa ni tatizo .
6. Hana washauri na anaamini kuwa hakuna mtu wa kumshauri.
7. Anachokifanya si kwamba hakifahamu bali ni utetezi na ni miungoni mwa walewale.
8. Kuwa prof. kisiwe ndio kigezo kuwa chochote atakacho kisema na kutenda ni sahihi na hakitakiwi kuhojiwa hata kama kuna utata au mkanganyiko.
8.Yeye kalewa sifa kwa machache aliyoyafanya .
9. Si muungana kikauli
10.Ni mtu mpenda sifa nk


2014-05-31 23:22 GMT+03:00 'Gikaro Ryoba' via Mabadiliko Forum <mabadilikotanzania@googlegroups.com>:
Ndugu Mhariri,
Wakati anasoma bajeti ya Wizara yake, Profesa Muhongo akimchana Dr Ole Sendeka bungeni kwa kumkejeli na kumdhalilisha hadharani huku akifikia hatua ya kutaka kuweka hadharani matokeo yake (Ole Sendeka) ya mtihani wa kidato cha nne aliokaa mwaka 1984 katika Shule ya Sekondari Monduli.

Isingekuwa busara za Spika Makinda ni dhahiri kwamba Muhongo angeanika matokeo ya Ole Sendeka hadharani.

Badala ya kujibu tuhuma za ufisadi wa fedha za umma unaomkabili yeye (Profesa Muhongo) na mshirika wake (Maswi), Muhongo alitumia muda wa umma vibaya kwa kumshambulia Ole Sendeka kama mtu binafsi na kumdhalilisha vya kutosha.

Kwa jinsi ninavyofahamu mimi, ushahidi ukishatolewa bungeni, kama alivyofanya Dr Kafulila na Dr Ole Sendeka, ni jukumu la tume ya maadili ya bunge kuuchunguza na kuona kama unakidhi haja na kisha kuwapelekea TAKUKURU na mahakama waufanyie kazi.

Sasa inakuwaje Madam Spika akamruhusu Prof Muhongo apoteze muda wa umma kwa kumshambulia Ole Sendeka kama mtu binafsi huku akikwepa tuhuma za ufisadi zinazomwandama yeye na Maswi? Hili suala sio sawawa hata kidogo.

Aidha, inaonekana kwamba Prof Muhongo ni mtu wa ajabu sana kwa jinsi anavyojisifu kwa usomi wake bila kuzingatia kwamba sisi watanzania tumemtuma akatuwashie umeme sio kututangazia usomi wake! Mh Mbowe aliomba muda uongezwe ili kila mbunge apate nafasi ya kuhoji namna mambo yanavyokwenda ovyo kwenye wizara hii lakini Prof Muhongo akambeza na kumdharau.

Majisifu ya kila siku ya profesa Muhongo na kuringia usomi wake sio tija kwa watanzania. Watanzania tunataka umeme na tunataka mafisadi wanaokula fedha za umma washughulikiwe.

Sisi hatuna haja na usomi wa Muhongo. Hata kama Wizara hii ikiongozwa na mtu aisiyekwenda shule kama vile Kapteni Komba au Prof Majimarefu, sisi hatuna shida na hilo. Shida na taabu yetu ni kuona kila mtanzania anapata huduma ya umeme wa uhakika.

Profesa Muhongo anatakiwa ajiandikishe kwenye chuo siasa cha CCM Kivukoni, akajifunze taaluma ya siasa na namna ya kuheshimu watu na mawazo yao, tofauti na jinsi anavyotenda mambo kwa sasa. Kutaja matokeo ya mtihani ya Ole Sendeka bungeni haikuwa hoja ya msingi. Hoja ya msingi ilikuwa ajibu tuhuma zinazomkabili yeye na msaidizi wake wa karibu (Maswi). Vitendo vya kifisadi vinavyofanywa na watu wa chama na serikali haviwafurahishi wananchi hata kidogo. Wananchi wanataka mawaziri wachapakazi watakaowaletea maendeleao endelevu. Hawataki mawaziri domo kaya wanaoringia usomi wao wakati wanashindwa kutumia usomi huo kuwaletea wananchi maendeleo. Kutamba kwamba amewahi kuwa Rais wa wanajioljia Afrika hakutuongezei shibe na wala hakutupunguzii njaa. Muhongo anapaswa kupima kila neno linalotoka kinywani mwake na kutathimini madhara yake kabla ya kuropoka.

Kutaja hadharani matokeo ya mtihani ya mtu anayetetea wananchi, ni utovu wa maadili ya uongozi na nidhamu kwa kiongozi mkubwa kama Muhongo ambaye anategemewa kuwaletea watanzania maendeleo. Matokeo ya mtihani ya mtu ni SIRI, hayatakiwi kutajwa hadharani—hii ni NYARA ya serikali. Muhongo na hao watumishi kengeufu wa Baraza la Mitihani (NECTA) waliomchapia matokeo ya Ole Sendeka yafaa wachukuliwe hatua za kisheria kwa kukiuka miiko ya utumishi wa umma.
 
Thobias Odhiambo,
Dar es Salaam,
Simu: 0719 786 226

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/1401567765.28623.YahooMailNeo%40web125303.mail.ne1.yahoo.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment