Tuesday, 17 June 2014

[wanabidii] KIGOGO WA NCCR MAGEUZI AJIVUA UANACHAMA

Kazi aliyopewa huko nccr, ama imemshinda ama ameimaliza ndiyo maana anashindwa kutoa sababu ya kujiondoa kwake. Hivi naye huyo alikuwa kigogo nccr?

From: wanabidii@googlegroups.com [mailto:wanabidii@googlegroups.com]
Sent: Wednesday, June 18, 2014 7:57 AM
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: RE: [wanabidii] KIGOGO WA NCCR MAGEUZI AJIVUA UANACHAMA

Huyu ndugu sijamwelewa. Kilichomtoa ni ajali, bajeti, Katiba, UKAWA au nini!
Mbona statement yenyewe kama vile ni ya kughushi.
Nahisi NCCR MAGEUZI watafanya sherehe kwa huyu ndugu kujiondoa kwenye chama maana naona kama ulikuwa mzigo usiobebeka.

From: 'Mollel' via Wanabidii
Sent: ‎6/‎18/‎2014 1:01
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] KIGOGO WA NCCR MAGEUZI AJIVUA UANACHAMA

Ni kweli Baha

'bahabp2003' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Kazi kwelikweli huu usanii huu,balaa

Sent from Samsung tablet

-------- Original message --------
From 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Date: 17/06/2014 23:57 (GMT+03:00)
To wanabidii@googlegroups.com
Subject Re: [wanabidii] KIGOGO WA NCCR MAGEUZI AJIVUA UANACHAMA

Ipo siku mtu ataita waandishi wa habari kuwaambia leo sili chakula.

On Tuesday, June 17, 2014 5:09 PM, Emma Kaaya <emmakaaya@gmail.com> wrote:

TAMKO LA KUJIVUA UANACHAMA WA CHAMA CHA

NCCR – MAGEUZI 17 Juni 2014.

1 :0    UTANGULIZI

Ndugu wana habari na ndugu Watanzania, kwa kutambua mchango wangu

mkubwa ambao nimkuwa nikiufanya katika ujenzi wa vyama vya siasa hasa

Upinzani hapa nchini, ni dhahiri nimekuwa mjenzi wa vyama kuliko

mafanikio ya wananchi.  Nimegundua mengi sana na kujifunza mengi sana

juu ya hivyo vyama vyetu vya Siasa, tunapotafuta demokrasia katika

nchi yetu sio tu kuwa huru kwa kila jambo bali kuwa na UTU kwa watu 

tunaowatafutia Demokrasia ya kweli, hatuwezi kusema nchi haina

demokrasia kama hatujatenda haki kwa wanachama au wananchi wetu.

SABABU ZA KUJIUDHURU UANACHAMA NA NYADIFA ZOTE ZA UONGOZI.

2 :0    AJALI YA GARI

Mwaka jana June 2013 kulikuwa na uchaguzi mdogo wa Udiwani Wilayani

sengerema Kata ya Nyampulukano na mimi nikiwa msimamizi wa Uchaguzi

huo mdogo wa marudio, jumamosi ya kuamkia uchaguzi tulipata ajali ya

gari tukitoka kukagua vituo vya kupigia kura na mimi nilikuwa kiti cha

mbele cha gari na nikapata maumivu makali sana, japo nilipewa huduma

ya kwanza lakini baada ya hapo sikupata matibabu stahiki kitu ambacho

mpaka sasa, nisingeweza kulaumu kama hawajui lakini wanajua fika

viongozi wenzangu, na ukizingatia wakati ule nilikuwa Katibu wa

Mahusiano na Uenezi Taifa kitengo cha Vijana.

Kutokana na hali kuwa si nzuri na kufikia kuona nalalamika ujue kabisa

hali si nzuri ki afya, jambo la msingi kwa wenzangu hata kama wanahisi

na makosa lakini jambo la Busara ni UTU kwanza wakumponya aliye

mgonjwa ndipo busara zingine zinafanyika, kiukweli nasikitika sana na

ninaumia sana kwa tukio hili maana ile ilikuwa ni kazi ya chama na

siya mtu, ina maana hata Elfu kumi tu nayo ni ngumu ?  kweli hapa

tujiulize sasa, na ndio maana naumia sana kwa hilo, kwa hili mimi

naona kama wamenitelekeza na kuniachia familia yangu mzigo.

Nashauri tu kuwa vijana wenzangu wa Kitanzania tunapo jiunga na vyama

vya Siasa  tuchunguze UTU kwanza kabla hatujafikia maamuzi na tusiwe

washabiki wasiasa bila kujua hatima yetu kimaisha, nashauri kama

vijana tuwe tunasapotiana kwenye matatizo maana leo limemkuta Kisandu

kesho linakuja kwako.  Nimejaribu hatakuomba msaada kwa baadhi ya

viongozi rafiki msaada wa aina yoyote bila mafanikio.

USHAURI WANGU kwa chama changu NCCR – Mageuzi naomba kama hili

limetokea kwangu basi lisijirudie kwa mwingine kwani hata Mungu

hapendi kuona hali kama hizo.

Kutokana na hili la matibabu ndugu na familia yangu wamenishauri

niachane na Siasa za vyama ili waweze kuona wananisaidia vipi,

kimsingi naungana na ndugu zangu na kukubali ombi lao kuliko kuumia

namna hii.  Naomba msamaha kwa viongozi wenzangu pale tulipo kwazana

na mimi na wasamehe pale walipo nikosea japo nabaki na maumivu ya

kiafya.

3 :0    KATIBA MPYA

Kwa upande wa swala la KATIBA MPYA, huu mchakato si wa mtu mmoja au

watu kadhaa bali ni mchakato wa Watanzania wote.  Swala la Muundo wa

Muungano si swala la CCM wala UKAWA bali ni letu sote, hapa

ningeshauri tu kuepuka mvutano baina ya serikali mbili au Serikali

tatu, wakakaa pamoja na kufikia maridhiano yenye Busara ili tupate

Katiba mpya inayoendana na mazingira ya Kitanzania.   Pia lazima

wawakilishi wetu Bunge la Katiba watambue kuwa maoni ya Serikai mbili

ni ya Wananchi na Maoni ya Serikali tatu nayo pia ni ya Wananchi hivyo

Busara ndio itumike kurejesha Umoja wetu wenye katiba ya pamoja.

4 :0    KUHUSU BAJETI YA SERIKALI MWAKA  HUU

Viongozi wetu watambue kuwa Bajeti hii ni ya Watanzania wote hivyo

badala ya kukosoa tunapaswa kuboresha na tusikosoe bila kuiboresha

maana kama tutakosoa tu mwisho wa siku tutakuwa hatuja tibu chochote

bali serikali ikosolewe kwa kupewa solution.

5:0     UKAWA

Hakuna dhambi mbaya kama dhambi ya ubaguzi,  Baba au Mama akibagua

baadhi ya watoto tena wadamu ni dhambi kali sana ya ubaguzi

inayohitaji kukemewa.  Ndugu zangu wanao jiita UKAWA hawa jamaa si

wazalendo kabisa wametawaliwa na dhambi ya ubaguzi wa vyama.  Vyama

vya Siasa vipo 23, vyama 22 vikawa ni vyama vya Upinzani, iweje leo

wote ni wapinzani eti UKAWA iwe ya vyama vitatu vya upinzani fikiria

kama ni uchaguzi Mkuu, vyama vitatu kugombea uchaguzi haisaidii maana

hata robo haijafika. Ubaguzi uliofanywa na hawa jamaa hauvumiliki

kabisa na si vitendo bali ni Umoja ndani ya Mtengano.  Wakiweza

kuungana vyote vyama 22 vikawa UKAWA basi nitakuwa tayari kuendelea na

siasa na hata Serikali 3 nitaunga mkono lakini dhambi ya kubaguana ya

vyama  itaendelea basi ni heri Serikali 2 au 1 maana UKAWA ni ya vyama

vitatu na si ya wananchi maana ya UKAWA ya wananchi ni ya vyama vyote

22 vya Upinzani dhambi ya ubaguzi iacheni ni Pepo mchafu.

6:0     FIKRA MBADALA

Vijana wenzangu tuache mihemko na jaziba katika ushabiki wa mambo ya

kisiasa na tuhamie katika uzalendo wa kujenga nchi yeye Amani na

Uzalendo bila kujali itikadi za vyama vyetu na tusijikite kuchagua

vyama bali tuchague viongozi wanaotufaa bila kujali Ushabiki wa vyama.

7:0     MAPUMZIKO

Kwa sasa nimeamua kupumzika siasa na kuangalia mstakabli wa maisha ya

kifamilia kwanza, pamoja na kupumzika huko nitapumzika na kwamba

nitakuwa naelekea chama gani hilo si swala la leo mpaka pale

nitakapooona inafaa na sijui ni lini.

Ndugu wanahabari nifikishieni taarifa hii kwa umma wa Watanzania na

Mungu atupe uzima wa maisha marefu.

0786 025 609

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA.

MWL. DEOGRATIUS KISANDU

ALIYEKUWA MJUMBE WA HALMASHAURI KUU TAIFA NCCR – MAGEUZI 17 / 06 / 2014

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Note:
This message is for the named person's use only.  It may contain confidential, proprietary or legally privileged information.  No confidentiality or privilege is waived or lost by any mistransmission.  If you receive this message in error, please immediately delete it and all copies of it from your system, destroy any hard copies of it and notify the sender.  You must not, directly or indirectly, use, disclose, distribute, print, or copy any part of this message if you are not the intended recipient. MWANANCHI COMMUNICATIONS LIMITED and any of its subsidiaries each reserve the right to monitor all e-mail communications through its networks.
Any views expressed in this message are those of the individual sender, except where the message states otherwise and the sender is authorized to state them to be the views of any such entity.

Thank You.

0 comments:

Post a Comment