Sunday, 8 June 2014

Re: [wanabidii] WAZIRI MKUU ACHARUKA, AKATAA KUKAGUA JENGO LA ZAHANATI

Kwanza, kituo cha afya cha Mkonze kimejengwa kwa ufadhili wa Ubalozi wa nchi gani? Hakutaja hapa Abdallah.

Pili na kubwa zaidi, sasa huyu Premier ndo ameamua nini? Kwa kutokagua mradi amemkomoa nani? Naona amewakomoa wananchi. Na amewatenda nini watendaji wa HLM ambao wamemkaidi amri aliyoitoa? Huyu naye anakuwa Premier lame duck!

Anachoweza ni kuamuru watu wapigwe tu na polisi. basi pia wanaamua kuua. Na mahkama imempa benefit. Kichekesho kwelikweli halafu tunawasikia watawala wakiimba, Mizaha mitupu dunia ya leo hasa Afrika.

Jabir+
--------------------------------------------
On Sun, 6/8/14, Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com> wrote:

Subject: [wanabidii] WAZIRI MKUU ACHARUKA, AKATAA KUKAGUA JENGO LA ZAHANATI
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sunday, June 8, 2014, 12:06 AM

TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
WAZIRI MKUU ACHARUKA, AKATAA KUKAGUA JENGO LA
ZAHANATI*Ni baada ya wataalam kukiuka maagizo
yake aliyotoa Machi mwaka huu
ILE HALI ya kufanya kazi kwa mazoea (business as
usual) iliyojengeka kwa baadhi ya watendaji wa Serikali leo
imewatokea puani watendaji wa Manispaa ya Dodoma wakati
Waziri Mkuu alipoamua kufanya ziara kukagua miradi ya
maendeleo.
Akiwa katika eneo la kwanza ambalo alipangiwa
kukagua ujenzi wa kituo cha afya cha Mkonze leo asubuhi
(Jumamosi, Juni 7, 2014) Waziri Mkuu alipokea taarifa ya
ujenzi wa kituo na kubaini kuwa hawajafanya chochote ili
kutekeleza maagizo yake aliyoyatoa Machi 22,
2014.
Katika taarifa yake, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa
ya Dodoma, Mhandisi Lusako Kilembe alimweleza Waziri Mkuu
kwamba walifanya tathmini ya ujenzi wa kituo hicho na
kubaini kuwa zinahitajika sh. Milioni 24.15 na kwamba maombi
ya matumizi hayo yamepangwa kujadiliwa kwenye kikao cha
kamati ya fedha na uongozi kitakachofanyika Juni 10, mwaka
huu.
Akiwa katika maadhimisho ya kilele cha wiki ya
maji ambayo Kitaifa yalifanyika mkoani Dodoma, Waziri Mkuu
alizindua mradi wa maji jirani na kituo cha afya cha Mkonze
na kubaini kuwa kuna hitilafu za ujenzi. Ndipo akaagiza
kwamba ufanyike ukarabati na yeye akaahidi kuja kukagua
ukarabati huo mwezi Juni, 2014.
Mara baada ya kusomewa taarifa ya mradi, Waziri
Mkuu akahoji ni kwa nini hawajafanya chochote tangu alipotoa
maelekezo Machi, mwaka huu. Hakupata jibu la kueleweka
kutoka kwa viongozi wa wilaya na mkoa.
Waziri Mkuu aliwasalimia wananchi waliokuwepo
kwenye eneo hilo na kuwaeleza kwamba hawezi kukagua kituo
hicho ilhali hakuna kilichotekelezwa tangu afike hapo Machi
mwaka huu.
Alisema haiwezekani yeye atoe maagizo katika
kipindi chote hicho halafu kisifanyike kitu chochote.
Akaondoka na kuendelea na ziara hadi kijiji cha Manzase
ambako alikagua mradi wa kisima cha maji.Mapema,
katika taarifa yake, Mhandisi Kilembe alisema kituo hicho
cha afya kilijengwa chini ya ufadhili wa ubalozi katika
makubaliano yaliyofikiwa Novemba 11, 2009 kwamba ingetoa
dola za marekani 84,307 sawa na sh. Milioni
152.86.
Hata hivyo, mara baada ya ujenzi kukamilika
Agosti 29, 2012, kituo hicho kilipata nyufa nyingi hali
iliyosababisha kifungwe na wananchi walitoa malalamiko yao
kwa Waziri Mkuu Machi mwaka huu wakati alipokwenda kuzindua
mradi wa maji kwenye kijiji cha Mkonze jirani na kituo
hicho.
Akiwa katika kijiji cha Manzase Waziri Mkuu
aliridhishwa na ujenzi wa mradi wa maji kwa ajili ya wakazi
9,000 wa eneo ambapo alielezwa kwamba utakamilika Julai 16,
2014.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:OFISI YA WAZIRI
MKUU,S. L. P.
980,DODOMA.JUMAMOSI, JUNI 7,
2014



--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment