Friday, 6 June 2014

RE: [wanabidii] Sakata la Mume wa mwimbaji FLORA MBASHA kumbaka shemeji yake mapya yaibuka

JINI MAHABA AT WORK - HII INAONESHA DHAHIRI JINSI WATUMISHI WA MUNGU NA WATU WENGINE WA BWANA WANAVYOANDAMWA NA ROHO CHAFU ILI KUWAHARIBIA NDOA, UCHUMI NA AFYA ZAO. WATU WA MUNGU  TUCHUKUE TAHADHARI KWA KUKESHA KATIKA MAOMBI NA KUTOTOA MLANGO WA ADUI KUPITIA NA KUTUHARIBU.

From: wanabidii@googlegroups.com [mailto:wanabidii@googlegroups.com] On Behalf Of Emma Kaaya
Sent: 05/Jun/2014 3:03 PM
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Sakata la Mume wa mwimbaji FLORA MBASHA kumbaka shemeji yake mapya yaibuka

BAADA ya kudumu kwa zaidi ya miaka 10, imebainika kuwa ndoa ya mwanamuziki mahiri wa muziki wa Injili Bongo, Flora na mumewe Emmanuel Mbasha ipo chali kwa maana ya kuanguka huku ikidaiwa kuwa, kusimama imara tena inawezekana lakini ni kazi kubwa, Amani limefukunyua mazito.

Hilo limejitokeza wiki moja baada ya madai ya mwanaume huyo kudaiwa kumbaka shemeji yake na kesi ipo polisi.

Imeelezwa Flora na mumewe ambao walifunga ndoa Agosti 22, 2002 wamepita katika migogoro mizito lakini wawili hao walikuwa wakiyamaliza kifamilia hadi kufikia hili la hivi karibuni ndilo lililoziba mataumaini ya wawili hao kuishi kama mume na mke.

Chanzo kilicho karibu na wawili hao kimeeleza kuwa, mzizi wa wawili hao kugombana ulichochewa na mwanamke mmoja (jina tunalo) ambaye alikuwa akikinzana na ushauri wa Mbasha mara kwa mara.
"Kuna vitu Mbasha alikuwa akimshauri huyo mama lakini walikuwa wakipishana Kiswahili  na hapo ndipo tatizo lilipokua hadi kufikia hatua ya kumwagana," kilisema chanzo.

TUJIUNGE NA MBASHA
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Emmanuel alizungumza na mwandishi wetu ambapo alikiri ndoa yake haina uhai tena na si rahisi kurejea katika hali ya kawaida licha ya kudai kuwa bado anampenda mkewe.
"Tulikuwa tunagombana sana na Flora lakini tulikuwa tukipatana ila mama… (anamtaja jina) alichangia ugomvi,

Flora naye alikuwa na nyendo zake mbaya, kuna wakati alikuwa anatoka kwenda gym (sehemu ya mazoezi) anachelewa kurudi ikafika wakati na nguvu ya ndugu wa mke ikawa kubwa kiasi cha kunizidi mimi na hapo ndipo mambo yalipofikia pabaya kabisa."

FLORA ATIMKA NYUMBANI
Mbasha anaendelea: "Ugomvi ulizidi, ilifika wakati tulipishana kiasi cha yeye kuondoka nyumbani na kwenda kuishi katika nyumba ya wageni kwa miezi kadhaa wakati huo.

"Ndani ya ugomvi huo nilisikia mengi, baadhi ya watu wananiambia mke wangu anaonekana na Prado na mwanaume mwingine mwenye pesa, iliniuma sana ingawa sijawahi kumuona moja kwa moja," alisema Emmanuel.

Kuhusu ugomvi huo, hivi karibuni Flora alikaririwa katika vyombo vya habari akisema hana tatizo na mumewe na ameshasamehe na kusahau yote yaliyopita hivyo ajitokeze tu ili akajibu mashitaka ya kudaiwa kubaka binti wa miaka 17 yaliyofunguliwa.

"Mimi sina tatizo kabisa na mume wangu, nimeshasamehe yote yaliyopita, kuhusu mashitaka ningeweza kuyafuta kama ningekuwa mimi ndiye niliyemshitaki," alisema Flora.

FLORA ADAIWA KUHAMIA KWA GWAJIMA
Wakati gazeti hili likiendelea kusaka undani juu ya sakata hili, kuna chanzo kingine kilipenyeza data kuwa baada ya ugomvi kuwa mzito, Flora alihamia kwa Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Dar, Josephat Gwajima ambako ndiko alikuwa akisali kila Jumapili.

"Kwani nyinyi Global hamna habari? Flora amehamia kwa Gwajima Jumapili iliyopita, kwanza alihudhuria ibada jioni akaenda kuishi maana Gwajima ni mchungaji wake kwa sasa," kilisema chanzo.

GWAJIMA ACHOMOA
Ili kupata mizani ya madai hayo, juzi Amani lilimpigia simu Mchungaji Gwajima na kumuuliza kama kweli Flora amehamia kwake kufuatia ugomvi kati yake na mumewe ambapo alikataa katakata.
"Flora hayupo hapa…mnataka niwaambiwe yuko hapa  halafu vyombo vya habari muanze kuandika vibaya? Hakuna kitu kama hicho," alisema Gwajima.

KWA NINI CHALI?
Ndoa kuwa chali ni ile ambayo imeanguka lakini inaweza kusimama tena tofauti na ndoa kuvunjika. Global iliwahi kuandika NDOA YA THEA CHALI baadaye ikasimama tena. Thea ni msanii wa filamu alifunga ndoa na Michael Sangu 'Mike' ambaye pia ni mwigizaji.

Wakati Emmanuel akizungumza na mwandishi wetu, alikiri kuwa Flora ameshamgeuka na nguvu kubwa imemuingia ndani ya moyo wake hivyo kuna ugumu sana wa kurudiana.

"Flora ambaye nilitegemea awe msaada katika hili lakini amefikia steji ya kuacha kunisikiliza, anasema haniamini, kwamba ninaweza kumfanyia lolote, sasa si bora kama anataka tuachane kwa heri kuliko kuniundia zengwe ambalo linataka kunipeleka mimi jela?" alihoji Mbasha.

Kutokana na mvutano huo pamoja na kesi hiyo ya kudaiwa kubaka inayomwandana Mbasha ni dhahiri kwamba kila mmoja hana imani na mwenzake tena hivyo suala la wawili hao kuishi kama zamani linakuwa gumu kuliko ngamia kupenya kwenye  tundu la sindano.

Emmanuel Mbasha alishitakiwa katika Kituo cha Polisi cha Tabata Shule, Mei 30, mwaka huu kwa madai ya kumbaka shemejie.Uchunguzi juu ya tukio hilo unaendelea hadi sasa shitaka ambalo mwenyewe amelikanusha.

On Monday, June 2, 2014 9:42:46 PM UTC+3, paul lawala wrote:

Miaka 17 kisheria hawezi kuhiari kufanya ngono,Law of child act 2009

2014-06-02 19:33 GMT+03:00 Jovias Mwesiga <ngo...@gmail.com>:

Hivi ubakaji kwa sheria ya tazania unasomekaje? Kwa hili ni ngumu kuhukumu kwa kusoma yaliyoandikwa labda tusubiri likianza kushugulikiwa kisheria

2014-06-01 17:11 GMT-05:00 Nicomedes Kajungu <nicom...@gmail.com>:

Hapa kuna maswali mengi kuliko majibi.

Wengine wanapenda kuharibiana tu.

On Jun 2, 2014 12:18 AM, "'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii" <wana...@googlegroups.com> wrote:

Kwa nini alipotaka kumbaka kwa mara ya kwanza sebureni asikimbie kupiga kelele na kutoka ndani. Miaka kumi na saba ana nguvu ya kupambana naye. Pili tena ndani ya gari ana nafasi gani ya kukuzuia ukashindwa kupiga dirisha hata kupasua kioo na kitu. Gari ni mbanano mapaka akufuate kitini akubake na iwezekane umelala au upo macho. Mengine nayo ni ya kuuliza. Asiikamate hiyo dudu na kuivuta why-age 17???? ama kweli!

On Thursday, 29 May 2014, 9:02, Emma Kaaya <emma...@gmail.com> wrote:

JESHI la Polisi Mkoa wa Ilala jijini Dar es Salaam linamsaka kwa udi na uvumba Emmanuel Mbasha (pichani) ambaye ni mume wa mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini, Flora Mbasha kwa madai ya kumbaka shemeji yake mwenye miaka 17 (jina tunalo) ambaye ni yatima.

Error! Filename not specified.

Flora Mbasha akiwa na mumewe Emmanuel Mbasha anayetuhumiwa kwa ubakaji.

Taarifa zilizopatikana  ndani  ya  jeshi hilo kupitia vyanzo vyetu makini zinadai kwamba mlalamikaji huyo alifika kituoni hapo Jumatatu iliyopita muda wa mchana na kufungua kesi  yenye Kumbukumbu Na. TBT/RB/3191/2014 na ya Jalada  la  Uchunguzi  Na. TBT/IR/1865/2014 akidai  kufanyiwa  unyama  huo kwa siku mbili (Ijumaa na Jumapili)  wiki iliyopita nyumbani kwa Mbasha, Tabata-Kimanga, Dar.

Ilidaiwa  kuwa, Ijumaa iliyopita mlalamikiwa alifanya kitendo hicho sebuleni nyumbani na Jumapili ilidaiwa  alitekeleza ukatili wake huo ndani ya  gari lake  hali ambayo  ilimfanya mlalamikaji kutoa  taarifa  Kituo cha Polisi, Tabara-Aroma jijini Dar.

Error! Filename not specified.

Mume wa mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini, Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha anayetafutwa na polisi kwa kosa la ubakaji.

Iliendelea kudaiwa kuwa, kufuatia maumivu  makali  aliyoyapata mlalamikaji huyo ilibidi  aende  Hospitali ya Amana  na  kugundulika  kuwa aliingiliwa  kimapenzi na kumsababishia michubuko  sehemu za  siri.

HISTORIA YA MLALAMIKAJI

Mlalamikaji ni  kati  ya  watoto  mapacha  waliozaliwa  jijini Mwanza  na mama  ambaye  jina lake  halikupatikana mara moja.

Mama wa mtoto huyo (kwa sasa ni marehemu pamoja na mume wake) akiwa muumini wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God (EAGT) aliamua  kumtoa mtoto mmoja kwa mama  mzazi wa Flora Mbasha kwa lengo la kumlea,  wakati huo mtoto  huyo alikuwa na miezi  mitatu.

Error! Filename not specified.

Flora Mbasha akiwa na mumewe Emmanuel Mbasha.

Ikaelezwa kuwa, mama wa  Flora alikaa  na  mtoto huyo akimsomesha hadi alipofika darasa la saba ambapo alimkabidhi kwa Flora na kuishi naye hadi  alipofikwa na janga hilo.

Maelezo zaidi yanasema Mbasha aliweza  kufanya  kitendo  hicho  kwa sababu mkewe (Flora)  ameondoka  nyumbani na kwenda kuishi hotelini kwa kile  kilichodaiwa  kwamba kuna ugomvi  mkubwa ndani ya ndoa yao.

Taarifa  zaidi  zinadai kwa sasa Mbasha naye hayupo  nyumbani kwake huku mlalamikaji yuko  Hospitali  ya Amana akiendelea kufanyiwa  uchunguzi  wa  kiafya ili kubaini kama ana maambukizi ya magonjwa ya zinaa au la!

Error! Filename not specified.

Wanandoa hao katika pozi.

Kwa  upande  wake  mlalamikaji huyo alipopigiwa  simu  juzi kwa  lengo  la  kuthibitisha  kuhusiana  na sakata  hilo  alikiri na kusema  amekwishatoa  taarifa  polisi   kwa  kitendo alichofanyiwa na mwenye nyumba huyo huyo.

--
Send Emails to wana...@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+...@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+...@googlegroups.com.

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment