Sunday, 22 June 2014

Re: [wanabidii] Re: AJALI YAUA 7 LUGALO , DAR ES SALAAM

Poleni sana mliopotelewa na ndugu na waliojeruhiwa. Tunahitaji kuwabana zaidi wanaotoa leseni za udereva. Ziwe za halali. Pili tutumie magari mapya. Daladala nyingi ni mbovu sana. na ni chakavu hazistahili kubeba abiria kabisa. Anyway najihangaisha. Wacha tufe tu hakuna jinsi.

2014-06-22 14:49 GMT+03:00 'Aldin Mutembei' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:
Poleni jamani.

Nayaunga mkono mawazo ya Hildegarda.

Tofauti na kwetu, huku Ulaya na Marekani barabara zao ni PANA. Ni Pana hasa!!!! Zikiruhusu nafasi kwa watembea kwa miguu, na baiskeli. Mliokaa nchi za Scandinavia mnajua kuwa nafasi za baiskeli huwa na rangi za kibluu pembeni, na ni tofauti na njia ya watembea kwa miguu. Hapa Berlin nafasi za baisikeli zina rangi ya damu ya mzee. Kwa hiyo utakuta barabara ya kawaida (sio zile kuu Highway) ina ruhusu magari manne au 6 na kwenda na kurudi, na bado kuna barabara ya baisikeli na nyingine ya watembea kwa miguu. BAADA YA HAPO kuna nafasi kabla hujafikia nyumba. Yawe ni maduka au nyumba za makazi. 
Kwa hiyo, wale wanaopanga meza pembeni na kukaa kunywa au kula (kama sasa wakati wa Summer), wala hawana wasiwasi wa gari kuwakaribia.
Nenda Sinza, gari likikosa mwelekeo tu, wanywaji pombe zitawatoka vichwani, ikiwa watawahi kutoka hai.
Upanuzi wa barabara ya Ali Hassan Mwinyi bado ni MDOGO. Upanuzi wa barabara ya Morogoro ndio kabisaa!!! Usiniambie barabara nyingine ndogo ndogo za ndani ya jiji.

Miji inayojengwa miaka hii (kama ilivyojengwa sasa Dodoma) ingekuwa na sura hii, maana ni kupanga miaka 50 au 100 ijayo.

Kwa kifupi, sisi watu wa fasihi, habari hii ya ufinyu wa barabara inatukumbusha hadithi ya Shabaan Robert KUSADIKIKA.
Mjumbe aliyeleta habari kuwa nchi aliyotembelea, watu wake wana barabara pana na vyombo vinapita humo, aliambiwa: "mwongo na mzushi. unyayo wa binadamu hauzidi sintimeta XX sasa barabara pana ni za nini.
Mawazo ya kusadikika na kufikirika, kumbe kwetu ni ya kutendeka na kujionea.

Aldin

Aldin K. Mutembei   (PhD)                         Aldin K. Mutembei (PhD)
Taasisi ya Taaluma za Kiswahili                  Institute of Kiswahili Studies
Kampasi ya Mwalimu J.K. Nyerere             Mwalimu J.K. Nyerere Campus
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam                   University of Dar es Salaam, TANZANIA
+255 715 426 162      [Kiganjani]                +255 715 426 162  (Cell)

b-pepe: kaimutembei@gmail.com    
            Alternative e-mail: <kaimutembei@gmail.com>

On Sunday, 22 June 2014, 3:30, 'lesian mollel' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Nilikuwepo maeneo haya
Nawapongeza sana wanajeshi wetu wa kambi ya chi brigade na Lugalo wamesaidia sana kuokoa majeruhi
Kwa kweli tatizo ni speed kali ya dereva wa dala dala lililokua likienda Ubungo likitokea mtongani, nadhani gari lilikata labda break na kupoteza mwelekeo na kuhamia upande wa magar yaliokua yakielekea Tegeta na kulifyeka hiyo coaster....kiukweli maafa ni makubwa na yalikua ya kutisha hata sikuweza kutoa simu kupoga picha nilijikuta nabubujikwa na machozi......Madereva  wasioa na busara au wavuta bangi wasipewe kuendesha abiria jamani
Kwa haraka niliona maiti zaidi ya kumi though nasikia imetangaza 6 mmmmmh
Hali ilikua inatisha jamaniiiiii, acheni

On Saturday, June 21, 2014 4:22 PM, Oksana Spice <worldngojobs@gmail.com> wrote:

On Saturday, June 21, 2014 4:19:08 PM UTC+3, Oksana Spice wrote:
Ajali mbaya ya gari imetokea mchana huu, katika maeneo ya Lugalo jijini Dar es Salaam. Katika ajali hiyo, inakadiriwa zaidi ya watu saba wamefariki dunia.
Mashuhuda wanasema, ajali hiyo imesababishwa na gari aina ya dalala iliyokuwa ikitokea maeneo ya Tegeta kuja Mwenge. Gari hiyo ililigonga dalala nyingine kabla ya kulivamia roli na baadaye gari nyingine aina ya Toyota Discover.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment