Thursday, 5 June 2014

Re: [wanabidii] MALAWI WANATHUBUTU HAYA - TANZANIA NA KENYA TUKO WAPI?

Mbegu, kumbuka huyu mama hakuwahi kupigiwa kura, alipata urais kutokana na kifo cha boss wake, hata uteuzi wake kuwa makamu wa rais ulipigiwa kelele na wananchi, tatizo sio mabadiliko, ni nani tumuweke? Tusijepata akina gagbo na idd amin wengine. Hata hivyo huo uchaguzi unaousifia umejaa porojo haiwezekani wajiandikishe elfu 35, wapige kura elfu 180 na daftari la wapiga kura lipo.

----------
Sent from my Nokia phone

------Original message------
From: Edgar Mbegu <embegu@hotmail.com>
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, June 5, 2014 9:05:53 PM GMT+0000
Subject: RE: [wanabidii] MALAWI WANATHUBUTU HAYA - TANZANIA NA KENYA TUKO WAPI?

Mimi nadhani kwetu Tz tatizo ni ujinga na umasikini wa walio wengi; woga, ubinafsi na unafiki miongoni mwa "wasomi" wachache. Nashawishika kusema, ingekuwa kwingineko Afrika, yule mama na chama chake wangebebwa kwa risasi za moto, mabomu ya machozi, maji ya kuwasha n.k. Lakini, katika miaka ya hivi karibuni, marais wangapi wamepita Malawi? Vyama vingapi vimeshika dola Malawi? Lakini Malawi ipo na itaendelea kuwapo! Tutafakari! Nimtakie kila la heri Mutharika. Hope he will be a man of his words!

Date: Wed, 4 Jun 2014 05:40:55 -0700
From: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] MALAWI WANATHUBUTU HAYA - TANZANIA NA KENYA TUKO WAPI?
To: wanabidii@googlegroups.com

Malaw wanaelewa sana......cc baado ndio maana hata mtu akikamata nafasi ni kuumiza wengine kwa kwenda mbele bila kujali chama gani....kuna haja ya kujifunza uzalendo.....mwone huyu prof rais mpya w a malaw ahadi zake.....zimenigusa sana , akizitekeleza, there will be a new Malawi really

On Wednesday, June 4, 2014 1:09 PM, 'Nico Eatlawe' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Good piece of information. Hata Tanzania tunao kama Mutharika ila Joyce amewazuia wasipate fursa kuingia ikulu. Siku moja ya ajabu inakuja ambapo Farao lazima atawaachia wana wa Mungu kwenda nchi yao ya ahadi wakati yeye na farasi zake wakiwa chakula cha samaki!

On Tuesday, 3
June 2014, 11:51, Telesphor Magobe <tmagobe@gmail.com> wrote:

Uzoefu wangu ni kwamba viongozi wengi wa Afrika wanafanya vizuri katika awamu ya kwanza ya utawala wao na awamu ya pili huwa wamechoka na wanaelekeza nguvu nyingi kwenye maslahi yao (kwa kujirundikia mali na kupambana na washindani wao).
2014-06-03 13:01 GMT+03:00 'Mike Zunzu' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>:

Mheshimiwa Mtatiro,Hivi unadhani viongozi wa nchi yetu hawaijui misingi ya haki na wajibu wao?
Wanafahamu sana, tatizo ni ukosefu wa hekima na utashi, matokeo yake ni nchi kuongozwa kwa msingi isiyofaa, hata kiranja mkuu wa shule ya msingi anaweza akawa na mtaratibu mzuri wa kupanga taratibu na kuongoza viranja wenzake kuwa ufanisi zaidi kuliko nchi yetu
inavyoongozwa.Kunaweza kuwa naserikari zinazofuata misingi ya haki kila upande wa nchi tunazopakana nazo, kama viongozi wet hawatakuwa na huluka ya kuongoza kwa misingi ya haki tutabaki hivyo hivyo tukiburuzwa hadi mbingu zitakaposhuka.
Tunawapongeza majirani kwa hatu hiyo ya mwanzo, iwapo yote yatafanika kama inavyosomeka, hapo ndipo unaweza kuropoka na kusema hili ni chaguo la Mungu.

On Tuesday, 3 June 2014, 6:05, 'julius mtatiro' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

MALAWI
WAMEANZA KUONESHA NJIA, NI TAIFA LINALOELEKEA KATIKA DEMOKRASIA YA KWELI (USIKOSE
KUSOMA NUKUU HIZI NILIZOZITAFSIRI)

HOTUBA YA RAIS PETER MUTHARIKA - BAADA YA KUAPISHWA KUWA
RAIS WA TANO WA MALAWI - 02 Juni 2014.

1. VYOMBO
VYA DOLA KUTOTUMIWA VIBAYA NA WATAWALA;

"Kuanzia leo jeshi la polisi, taasisi ya kuzuia rushwa,
ofisi ya mwendesha mashtaka wa serikali na vyombo vingine vya ulinzi na
vinavyolinda sheria vitafanya kazi zake kwa uhuru lakini kwa weledi. Tutaizatiti
Taasisi ya kupambana na rushwa kwa rasilimali watu na uwezo wa kifedha ifanye
kazi yake bila kuingiliwa na serikali"

2. MAWAZIRI
NA WATUMISHI WA UMMA WEZI NA WABADHIRIFU;

"Katika utumishi wa umma, sitaongeza hata siku moja ya
kumvumilia waziri wangu au mfanyakazi wa serikali ambaye anachukua mali za umma
au mali isiyo yake. Mtakapoona waziri wa serikali yangu amekwamatwa msishangae.
Baraza langu la mawaziri litaishi na msingi huu wa kuwatumikia wananchi.

Nataka ujumbe huu ueleweke kwa uwazi kabla sijateua baraza
la mawaziri. Kama matakwa yako ni kuwa tajiri badala ya kuwatumikia wananchi wa
Malawi, usijihangaishe kuja kwenye baraza langu. Nitakapokuteua jiambie moyoni
kuwa leo ninachora mstari mwekundu dhidi ya rushwa, wizi wa mali za umma na
najiandaa kuchora mstari huo kwa damu yangu"

3. VYOMBO
VYA HABARI NA MAWASILIANO YA UMMA;

Uongozi wetu utahakikisha kuna upatikanaji wa habari wa
kutosha na katika hili tutawasiliana na washika dau wote pamoja na vyombo vya
habari ili kupitisha na kutekeleza muswada wa haki ya mawasiliano kuwa sheria.

Tutaruhusu Shirika la Utangazaji la Malawi (Hapa Tanzania
TBC) kufanya kazi kwa uwazi, uhuru na utaratibu unaotenda haki, kufanya maamuzi
ya uhariri kwa uhuru na sitaki waziri wangu wa mawasiliano kuingilia kazi yao.
Hii ni ahadi nayoitoa kwa wananchi wa Malawi. Enzi za kutumia mashirika ya
utangazaji ya UMMA kwa ajili ya kupendelea utawala zimepitwa na wakati. Enzi za
kufanya makeke ya watawala kupitia vyombo vya habari vya umma zimepitwa na
wakati"

4. KUBANA
MATUMIZI YA SERIKALI;

"Tutatekeleza utaratibu wa kubana matumizi. Hii itajumuisha
Rais kufanya kazi Ofisini kuliko barabarani. Ndiyo, nitakuja kuwatembelea
katika shughuli za kijamii na kitaifa. Lakini msiniulize kuja kuwatembelea bila
sababu za msingi huku nikitumia gharama kubwa za taifa. Nitawawezesha maafisa
wote wanaohusika katika utumishi wa umma wafanye kazi zao karibu yenu kama
wanavyotakiwa".

5. KASHFA YA
"CASHGATE"

Wana- Malawi wenzangu, katika miezi kumi na mbili iliyopita,
kulikuwa na jinai kadhaa zilizofanywa dhidi ya nchi yetu, kwa mfano KASHFA YA
"CASHGATE". Ninapenda kuwaeleza kwamba uchunguzi wa kashfa hii ambao
ulianzishwa na Rais Joyce Banda utaeendelezwa na kukamilishwa kwa haki. Wana wa
Malawi wanasubiri kujua nani alifanya nini. Wana wa Malawi wanataka rasilimali
zao zilizoibiwa zirudishwe. Wana wa Malawi wanataka haki itendeke na hakuna
atakayeidanganya serikali kuwa eti inawawinda watu bila sababu.

6. UTANGAMANO
WA KITAIFA;

"Ndugu zangu wana wa Malawi, nimeapishwa kuilinda katiba ya
Malawi na kusimamia utawala wa sheria. Hili nitalitekeleza. Lakini naomba
niweke jambo moja wazi. Sheria lazima iachwe ifanye kazi peke yake inapotokea
makosa yametendwa. Lazima tukomeshe utaratibu wa kukamata mtu halafu tunatafuta
kosa lake baadaye. Lazima tukomeshe tabia ya kuwaadhibu wale tusiowapenda kwa
sababu wanafuata itikadi iliyo tofauti na ya kwetu. Nyakati za kutumia vyombo
vya dola na vya haki kwa ajili ya KUWASHUGHULIKIA wapinzani wetu kisiasa
zimeshapitwa na wakati. Tusichanganye utendaji na utafutaji wa haki na visasi
vya kisiasa"

MAONI YANGU!

Kwa vyovyote vile, Tanzania tuna kila jambo la kujifunza
kutoka kwa taifa hili masikini, Uvumilivu wa Kisiasa, Kauli za viongozi zenye
kuonesha matumaini na Dira sahihi na Nia njema inayotoka katika kauli za
viongozi. Hapa kwetu kauli za viongozi ni "JESHI LITACHUKUA NCHI", "TUTAINGIA
MSTUNI", "KULENI NYASI" "WANANCHI HAWANA AKILI" n.k. Hata kashfa zetu kubwa za
mabilioni ya fedha yaliyochotwa zimeishia hewani kwa sababu wakubwa wanalindana
na wanalindana huku taifa LINAKWISHA. Tuendelee kutafakari.

J. Mtatiro,

Dar Es Salaam,+255 717 536 759.

CallSend SMSAdd to SkypeYou'll need Skype
CreditFree via Skype

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
mailto:wanabidii%2Bunsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

0 comments:

Post a Comment