Mhe. Keissy aweza kuwa sahihi - Zanzibar haijachangia gharama za Muungano.
SASA, Kwanza, mtoa hoja huyu na muandishi Hapns, watafute ni kiasi gani Zbar (SMZ) inaidai SMT fedha za faida ya kibiashara itokanayo na shughuli za taasisi za Muungano mfano ATC, TCAA, TPA, TPC/TPBank, TTCL, BoT. Hizo tu kwa miaka 20 (usiende mbali).
Pili, Waulizeni wakubwa wa SMT ni kwanini hawapo tayari kuweka bayana ugunduzi wa gharama za Muungano ili Zbar ijue mchango wake halali ni kiasi gani kwa mwaka. Mjue kuwa ugunduzi huu ulifanywa na kampuni za wataalamu wa kimataifa walioajiriwa na SMT/SMZ kwa ajili ya kazi hiyo ya kutafuta gharama halisi na mfumo wa ugawanyaji mapato ya shughuli za Muungano.
Mjue tu kwamba kazi hiyo ilifanywa mwaka 1997 (wakati huo utawala wa Ben Mkapa ulipounda kiitwacho Tume ya Rais ya Pamoja ya Fedha - Joint Presidential Commission) ambayo katibu wake ni Khamis Ame, aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi ndani ya Zanzibar Electoral Commission, ZEC), na ripoti yake ikatinga serikalini mwaka 2002 hivi.
(Hapa niwadokolee kitu kuwa kusubiri utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa na wataalamu, ilikubaliwa Zanzibar ipokee 4.5% ya misaada inayotolewa kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. This was agreed as a provisional amount pending the implementation of the proposals).
Tatu, hili kwa muandishi kipenzi changu Katabazi, peruzi kinachoitwa Articles of Union - hapa wala usijisumbue kuangalia ile aliyoitoa Balozi Sefue, achana nayo ile. Kwa uanasheria wako unaosomea, ipate kwenye vyanzo vya kuaminika - nakwambia usiende Serikalini utajisumbua bure - halafu rudi humu ukumbini ueleze kama ipo sehemu inayosema kwa makubaliano ya kuungana, serikali ya Tanganyika na Zanzibar zinafutwa.
Nne, nawasihi sana msiwe mnazishika hoja bila ya kutafakari kama zina hoja. Si hivyo nahofia mlio hivo mtakuwa mnajishusha kwa kujua. Ni afadhali mtu ujishushe kwa kutojua.
Kwaherini.
Jabir+
--------------------------------------------
On Wed, 6/4/14, 'Happiness Katabazi' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:
Subject: [wanabidii] KUJADILI MUUNGANO ISIWE DHAMBI,USALITI
To: "WANABIDII" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Wednesday, June 4, 2014, 1:58 AM
KUJADILI MUUNGANO ISIWE
DHAMBI,USALITI
Na Happiness Katabazi
KWA muda mrefu Watanzania walikuwa wameaminishwa kuwa
kuhoji, kukosoa au kujadili masuala yanayohusu muungano wa
Tanganyika na Zanzibar uliofanyika Aprili 26, mwaka 1964 ni
dhambi au usaliti.
Dhana hiyo kwa kiasi kikubwa ndiyo iliyosababisha baadhi ya
watu kuendelea kutoa manung'uniko ya chini chini yaliyozaa
kitu kinachoitwa kero za muungano zilizoanza kutishia uwepo
wake, hasa baada ya kusikia mapendekezo ya rasimu ya katiba
mpya inayopendekeza uwepo wa serikali tatu.
Kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele, kasumba hiyo ya
kuutukuza muungano bila kuhoji sababu za kuungana, matatizo
na faida zake, sasa imeanza kupotea, watu wanaoanza kuhoji
mambo hayo nao wameanza kuonekana si wasaliti au wenye nia
ya kuuvunja.
Watanzania wengi hasa wale wa Tanzania bara walikuwa
wakihofia kujitokeza hadharani kutoa hoja zinazokosoa baadhi
ya upungufu uliomo kwenye muungano na kinachofanywa na
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), lakini sasa hofu
yao inaanza kuyeyuka kama iyeyukavyo theluthi inapokutana na
joto.
Baadhi ya Wazanzibar kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamikia
muundo wa muungano uliopo hivi sasa kwamba umekuwa
ukiwanyonya na kukosa fursa ya kujikwamua kiuchumi ikiwemo
kujiunga kwenye mashirika mbalimbali ya kimataifa yenye
lengo la kuzikwamua kiuchumi nchi wanachama.
Malalamiko ya kuonewa, kunyonywa kutoka kwa viongozi au
wananchi wa Zanzibar ndivyo vilivyochangia baadhi ya
wanasiasa Tanzania bara kuogopa kuwakosoa wenzao kwa hofu ya
kupokea lugha chafu au kushambuliwa kwa kuitwa wabaguzi.
Miaka ya nyuma ilidaiwa kuna baadhi ya wanasiasa, waliwahi
kushughulikiwa kimya kimya, tena kikamilifu na dola au vyama
vyao kwa kisingizio tu walikuwa wanapinga Muungano.
Kimsingi waliokuwa wakikosoa, kuhoji na kujadili muungano
baadhi yao nilizungumza nao, hawakuwahi kufikiria kuvunja
Muungano, isipokuwa walikuwa na mtazamo tofauti kuhusu
baadhi ya mambo ndani ya Muungano na walikuwa wanataka
yarekebishwe kwa njia ya amani.
Mitazamo hiyo pengine ingeachiwa fursa ya kusikika, kero
nyingi za muungano zingetatuliwa, na Watanzania hivi sasa
wangekuwa wanazungumzia mambo mengine ya maendeleo.
Tunaona baadhi ya wanasiasa waliosulubiwa kule Zanzibar,
kimya kimya kwa fitna eti ni wapinga Muungano, Mungu
amewajalia kupata madaraka makubwa ndani ya Serikali ya
Umoja wa Kitaifa (SUK), ule uovu waliokuwa wakihusishwa nao
wa kuvunja muungano, umezikwa ingawa sijui ni katika
makaburi gani.
Mei 27, mwaka huu, Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy
(CCM), aliwashambulia Wazanzibar, kwamba hawana sababu
ya kulalamikia kutaka haki sawa kwenye kila jambo la
muungano wakati hawachangii kitu kwenye Serikali ya
Muungano.
Keissy alitoa kauli hiyo ndani ya Bunge, wakati akichangia
hoja ya Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa kwa mwaka wa fedha 2014/2015,
inayoongozwa na Waziri Bernard Membe.
Alichangia hoja hiyo akijibu hoja ya Kambi Rasmi ya Upinzani
iliyosema kuna upendeleo mkubwa na uwiano usio sawa kati ya
Tanzania Bara na Visiwani katika uteuzi wa mabalozi wa
Tanzania nje ya nchi.
Anasema kwa zaidi ya miaka 20 Zanzibar haichangii kitu
katika Serikali ya Muungano, lakini ndiyo vinara wa
Kulalamika na kutaka usawa kwenye kila jambo, hivyo kama
wanahitaji haki sawa basi waanze kuchangia fedha.
Wakati akiendelea kuchangia hoja hiyo, Mbunge wa Chakechake,
Mussa Haji Kombo (CUF), aliomba mwongozo wa Naibu Spika
dhidi ya kauli hiyo huku akitumia maneno yafuatayo:
"Mheshimiwa Spika, kuna mwendawazimu mwingine ni mtu
anayepiga piga mawe hovyo, mwingine anakuwa mtu wa
kuchekacheka, akipita anaweza kuwa anacheka tu
'kwekwekwe', na mwendwazimu mwingine ni yule anayeongea
ovyo mbele ya watu wenye heshima zao kama tulivyo humu
ndani."
Baada ya kauli hizo kulitokea malumbano ndani ya Bunge huku
baadhi ya wabunge wa Zanzibar kudai Keissy anafanya ubaguzi,
amewadhalilisha Wazanzibar kwa kuwaona ni masikini na pia
wakampiga marufuku asifike visiwani humo.
Malumbano hayo yalikatizwa na Naibu Spika Job Ndugai,
alipoamua kuahirisha Bunge, lakini mambo yaliendelea nje ya
Ukumbi wa Bunge ambapo wabunge kutoka Zanzibar waliwahi
kutoka nje kumkabili Keissy.
Kama si uwepo wa baadhi ya wabunge wa CCM walioamua kumuweka
kati Keissy, mbunge huyo angepigwa na wabunge kutoka
Zanzibar ambao walionyesha dhahiri kukerwa na kauli zake.
Ibara ya 17 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ya mwaka 1977, inasomeka hivi: "Kila raia wa Jamhuri
ya Muungano anayo haki ya kwenda kokote katika
Jamhuri ya Muungano na kuishi katika
sehemu yoyote, kutoka nje ya nchi na kuingia, na
pia haki ya kutoshurutishwa kuhama au kufukuzwa
kutoka katika Jamhuri ya Muungano.
Sasa kwa mujibu wa Ibara hiyo, tumuulize huyu Mbunge wa
Magogoni, Kombo Khamis Kombo, amepata wapi madaraka ya
kutaka Keissy azuiwe kwenda Zanzibar?
Hivi tukisema Kombo ndie kinara wa ubaguzi na amevunja
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka
1977 ya kutaka Keissy asiruhusiwe kwenda Zanzibar,
tutakuwa tumekosea?
Wale wabunge wa Zanzibar, walipaswa watuambie tena kwa njia
ya amani ni lini walichangia muungano. Mimi namuunga mkono
Keissy, kwamba baadhi ya Wazanzibar, kwa sababu wanazozijua
wao wamekuwa vinara wa kulalamika kila kukicha, kwamba
wanaonewa, mara Muungano uvunjwe, wananyonywa sana na
Tanzania Bara na hawaoni faida ya Muungano na kwamba Wabara
tuwaachie Zanzibar yao.
Sasa kosa la Keissy hapa liko wapi hadi wabunge hao
Wazanzibari watake kumshikisha adabu? Keissy amesema
ukweli kuwa baadhi ya Wazanzibar wamekuwa ni vinara wa
kulalamika na kutaka uwiano sawa katika kila jambo la
Muungano wakati Zanzibar inachangia kidogo.
Kwani si kweli Tanzania Bara inachangia pato kubwa
katika Muungano kuliko Zanzibar? Shida inatoka wapi? Mbona
nafasi nyingi za uongozi huko Zanzibar zimeshikwa na
Wazanzibar na Watanzania Bara hawalalamiki katika hilo?
Napata wasiwasi kuwa huenda wale wabunge waliozua tafrani
walikuwa na ajenda yao nyingine wakasingizia Keissy
amewakera. Maana haiingii akilini kabisa kilichosemwa
na Keissy, ndio kiwapandishe jazba na kutaka kumpiga wakati
aliyoyasema siyo mambo mapya na wabunge
hao walishindwa kutoa vielelezo vinavyoonyesha
aliyosema ni uongo.
Keissy amekuwa jasiri kati ya wanasiasa wachache wa Tanzania
Bara ambao wengi wao wamekuwa na mtazamo kama wake, lakini
wamekosa ujasiri wa kuuzungumza wazi kwa kisingizio
kuwa wanaogopa kutolewa lugha chafu kutoka kwa baadhi
ya Wazanzibar na kuambiwa kuwa wanataka kuvunja muungano.
Wengi wa wabunge walizoea kusikia kauli za kukosoa, kujadili
muungano kutoka kwa Tundu Lissu, ambaye kwa muda mrefu
alikuwa akionekana mstari wa mbele kugusa maeneo yaliyokuwa
yakionekana ni dhambi au usaliti kuyazungumzia.
Kauli ya Keissy haiwezi kuwa chanzo cha kuvunjika kwa
Muungano wetu, jambo la msingi linalopaswa kufanywa na
viongozi ni kuuzungumzia kwa uwazi ili kuuboresha zaidi
badala ya kuficha ficha mambo.
Hivi Zanzibar siku hizi wamegeuka kuwa miungu watu hadi
hawataki wasemwe au wakosolewe? Maana kila linapozungumzwa
jambo lao hata kama ni la ukweli wamekuwa wakali kama
pilipili na kuwashambulia wanaotoa kauli husika.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, aliwahi kusema Zanzibar si nchi,
baada ya hapo alishambuliwa kana kwamba alifanya uhaini
fulani.
Ibara ya 1 ya katiba ya nchi inasema hivi: "Tanzania ni
nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano."
Ibara ya 2 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
inasomeka hivi: "Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote
la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na
ni pamoja na sehemu yake ya bahari Tanzania inapakana
nayo."
Lakini kuna baadhi ya wanasiasa kutoka Zanzibar, kwa sababu
wanazozijua wamekuwa wakipotosha ukweli huo kwa kusema
Zanzibar ni nchi.
Wasomi wa sheria tunafahamu kuwa Zanzibar sio nchi kwa
sababu inakosa sifa ya kuwa na uwezo wa kuingia mikataba na
mataifa ya nje, tunapaswa kujadiliana matatizo ya muungano
bila jazba ili kuondoa mazonge yote yaliyomo la sivyo
tutaendelea kufuga matatizo.
Tuendelee kudumisha Muungano wetu.
0716 774494
www.katabazihappy.blogspot.com
Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la Jumapili, Juni 1 Mwaka
2014.
Sent from my iPad
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit
https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment