Nadhani tuige utekelezaji wake (kama ukifanyika) na sio maneno matupu,
Sisi ni wazuri sana wa propaganda ya maneno kuliko vitendo.
Mwanzo ni mwanzo tuone mwisho.
Mwananchi wa kawaida.
--
Sent from myMail app for Android
Tuesday, 03 June 2014, 07:59AM +0300 from "'julius mtatiro' via Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>:
MALAWI
WAMEANZA KUONESHA NJIA, NI TAIFA LINALOELEKEA KATIKA DEMOKRASIA YA KWELI (USIKOSE
KUSOMA NUKUU HIZI NILIZOZITAFSIRI)
HOTUBA YA RAIS PETER MUTHARIKA – BAADA YA KUAPISHWA KUWA
RAIS WA TANO WA MALAWI – 02 Juni 2014.
1. VYOMBO
VYA DOLA KUTOTUMIWA VIBAYA NA WATAWALA;
“Kuanzia leo jeshi la polisi, taasisi ya kuzuia rushwa,
ofisi ya mwendesha mashtaka wa serikali na vyombo vingine vya ulinzi na
vinavyolinda sheria vitafanya kazi zake kwa uhuru lakini kwa weledi. Tutaizatiti
Taasisi ya kupambana na rushwa kwa rasilimali watu na uwezo wa kifedha ifanye
kazi yake bila kuingiliwa na serikali”
2. MAWAZIRI
NA WATUMISHI WA UMMA WEZI NA WABADHIRIFU;
“Katika utumishi wa umma, sitaongeza hata siku moja ya
kumvumilia waziri wangu au mfanyakazi wa serikali ambaye anachukua mali za umma
au mali isiyo yake. Mtakapoona waziri wa serikali yangu amekwamatwa msishangae.
Baraza langu la mawaziri litaishi na msingi huu wa kuwatumikia wananchi.
Nataka ujumbe huu ueleweke kwa uwazi kabla sijateua baraza
la mawaziri. Kama matakwa yako ni kuwa tajiri badala ya kuwatumikia wananchi wa
Malawi, usijihangaishe kuja kwenye baraza langu. Nitakapokuteua jiambie moyoni
kuwa leo ninachora mstari mwekundu dhidi ya rushwa, wizi wa mali za umma na
najiandaa kuchora mstari huo kwa damu yangu”
3. VYOMBO
VYA HABARI NA MAWASILIANO YA UMMA;
Uongozi wetu utahakikisha kuna upatikanaji wa habari wa
kutosha na katika hili tutawasiliana na washika dau wote pamoja na vyombo vya
habari ili kupitisha na kutekeleza muswada wa haki ya mawasiliano kuwa sheria.
Tutaruhusu Shirika la Utangazaji la Malawi (Hapa Tanzania
TBC) kufanya kazi kwa uwazi, uhuru na utaratibu unaotenda haki, kufanya maamuzi
ya uhariri kwa uhuru na sitaki waziri wangu wa mawasiliano kuingilia kazi yao.
Hii ni ahadi nayoitoa kwa wananchi wa Malawi. Enzi za kutumia mashirika ya
utangazaji ya UMMA kwa ajili ya kupendelea utawala zimepitwa na wakati. Enzi za
kufanya makeke ya watawala kupitia vyombo vya habari vya umma zimepitwa na
wakati”
4. KUBANA
MATUMIZI YA SERIKALI;
“Tutatekeleza utaratibu wa kubana matumizi. Hii itajumuisha
Rais kufanya kazi Ofisini kuliko barabarani. Ndiyo, nitakuja kuwatembelea
katika shughuli za kijamii na kitaifa. Lakini msiniulize kuja kuwatembelea bila
sababu za msingi huku nikitumia gharama kubwa za taifa. Nitawawezesha maafisa
wote wanaohusika katika utumishi wa umma wafanye kazi zao karibu yenu kama
wanavyotakiwa”.
5. KASHFA YA
“CASHGATE”
Wana- Malawi wenzangu, katika miezi kumi na mbili iliyopita,
kulikuwa na jinai kadhaa zilizofanywa dhidi ya nchi yetu, kwa mfano KASHFA YA
“CASHGATE”. Ninapenda kuwaeleza kwamba uchunguzi wa kashfa hii ambao
ulianzishwa na Rais Joyce Banda utaeendelezwa na kukamilishwa kwa haki. Wana wa
Malawi wanasubiri kujua nani alifanya nini. Wana wa Malawi wanataka rasilimali
zao zilizoibiwa zirudishwe. Wana wa Malawi wanataka haki itendeke na hakuna
atakayeidanganya serikali kuwa eti inawawinda watu bila sababu.
6. UTANGAMANO
WA KITAIFA;
“Ndugu zangu wana wa Malawi, nimeapishwa kuilinda katiba ya
Malawi na kusimamia utawala wa sheria. Hili nitalitekeleza. Lakini naomba
niweke jambo moja wazi. Sheria lazima iachwe ifanye kazi peke yake inapotokea
makosa yametendwa. Lazima tukomeshe utaratibu wa kukamata mtu halafu tunatafuta
kosa lake baadaye. Lazima tukomeshe tabia ya kuwaadhibu wale tusiowapenda kwa
sababu wanafuata itikadi iliyo tofauti na ya kwetu. Nyakati za kutumia vyombo
vya dola na vya haki kwa ajili ya KUWASHUGHULIKIA wapinzani wetu kisiasa
zimeshapitwa na wakati. Tusichanganye utendaji na utafutaji wa haki na visasi
vya kisiasa”
MAONI YANGU!
Kwa vyovyote vile, Tanzania tuna kila jambo la kujifunza
kutoka kwa taifa hili masikini, Uvumilivu wa Kisiasa, Kauli za viongozi zenye
kuonesha matumaini na Dira sahihi na Nia njema inayotoka katika kauli za
viongozi. Hapa kwetu kauli za viongozi ni “JESHI LITACHUKUA NCHI”, “TUTAINGIA
MSTUNI”, “KULENI NYASI” “WANANCHI HAWANA AKILI” n.k. Hata kashfa zetu kubwa za
mabilioni ya fedha yaliyochotwa zimeishia hewani kwa sababu wakubwa wanalindana
na wanalindana huku taifa LINAKWISHA. Tuendelee kutafakari.
J. Mtatiro,
Dar Es Salaam,
+255 717 536 759.
Call
Send SMS
Add to Skype
You'll need Skype
Credit Free via Skype
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com .
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout .
0 comments:
Post a Comment