Sunday 2 February 2014

Re: [wanabidii] MAELEZO YA Mwl Lwaitama baada ya Kushushwa kwenye Ndege ya PrecisionAir

Ludovick Simon, umeupotosha umma!!!!!!!!!!!!

Kama tatizo lilikuwa kweli ni lugha na juu ya unyet wa kile kiti cha mlango dharura, alistahili kuamishwa kiti ili mtu mwingine akae pale.

Kumshusha haikuwa sawa, labda kama mzee alitishia kulipua ndege.

Lakini, je kumshusha imesaidia nini?

Nchi za wenzetu wakiwa na shaka juu ya abiria fulani, huwafanyia ukaguzi na safari huendelea, hata kama ni chini ya uangalizi maalumu.

Hicho kiti hakiepukiki, kinaweza kukukuta wewe.

Mimi nilishakataa kukaa hapo. Walinipa kiti kingine.

Nyongeza, wakinipaga kiti ambacho kipo usawa wa yale mapanga (kw anje) huwa nakataa. Sipendi ATR, huwa nasafiri basi. Sina jinsi.


2014-01-29 Ludovick Simon Mwijage <bugabo18@hotmail.com>:
PrecisionAir ilimkubali Dk Lwaitama kama mteja wao ilipomuuzia tiketi na kukubali kumsafirisha hadi mwisho wa safari yake.
 
Lakini wakati huo huo, kwa kununua tiketi ya PrecisionAir, Dk Lwaitama naye aliingia makubaliano nao kwamba angefuata utaratibu wanaoutumia wao kuwasafirisha abiria kwa njia ya anga.
 
Inaweza kudaiwa kwamba Dk Lwaitama alivunja makubaliano hayo alipokataa kufuata utaratibu wao, baada ya kupanda ndege yao. 
 
Kama Dk Lwaitama hakuridhika na utaratibu wanaoutumia PrecisionAir, basi angetuma malalamiko yake, na mapendekezo, kwenye mamlaka yanayohusika na pengine akafuatilia malalamiko yake kwa kuvihusisha vyombo vya habari. Kufanya hivi, huenda kungeepusha rabsha kwa abiria wenzake na kadhia yote hii.
 
Suala la lugha aliloliibua ni muhimu sana. Ndio maana wengi tuko upande wake. Lakini inaelekea aliibua suala hili kwenye jukwaa lisilo sahihi na bila kuelewa chanzo cha PrecisionAir kutumia Kingereza kwa abiria wenye kiti karibu na mlango wa dharura.
 
Ingekuwa vizuri zaidi kama tatizo hili lingemalizikia nje ya vyombo vya kukazia sheria na mahakama. Kwamba, Dk Lwaitama anafahamu Kingereza, inaweza kutumiwa na mawakili wa PrecisionAir kutaka kujua nia yake ilikuwa nini alipokataa kupokea maelekezo kwa lugha anayoifahamu. Ingekuwa jambo jingine kama Dk Lwaitama angekuwa hafahamu Kingereza.
 
Kwa upande mwingine, huenda PrecisionAir wasimuombe radhi kama baadhi yetu tunavyofikiri. Kwani, wakifanya hivi, watakuwa wanamkaribisha Dk Lwaitama kuwafungulia kesi ya madai. Haya labda ndio mambo tunayopashwa kuyatafakari kwa faida ya Dk Lwaitama badala ya kulaani tu mwenendo na utaratibu unaotumiwa na PrecisionAir.


 

 
> Date: Tue, 28 Jan 2014 20:04:58 +0000

> Subject: Re: [wanabidii] MAELEZO YA Mwl Lwaitama baada ya Kushushwa kwenye Ndege ya PrecisionAir
> From: hosea.ndaki@gmail.com
> To: wanabidii@googlegroups.com

>
> Yeye ndo kachelewesha ndege kusafiri na kusumbua abiria wengine, kwanza alikuwa amekaa mlango wa dharura sasa kuambiwa uhame kiti ndo azue timbwili lote hilo kweli?
>
> ----------
> Sent from my Nokia phone
>
> ------Original message------
> From: <bonnyluv84@hotmail.com>
> To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
> Date: Tuesday, January 28, 2014 9:02:11 PM GMT+0400
> Subject: Re: [wanabidii] MAELEZO YA Mwl Lwaitama baada ya Kushushwa kwenye Ndege ya PrecisionAir
>
>
> Pole sana, itakuwa imekusumbua hii hali.Muda wako, pesa uliyolipa na hukusafiri, usumbufu uliupata, hukufika Bukoba, mambo ulipanga kuyanya huko Bukoba yamekwama, umedhalilika, umesingiziwa kuwa umefanya fujo, umelazimishwa kutojua kiingereza while wa ni mwalimu wa lugha na unakifahamu zaidi yao na zaidi wamesababisha uwasababishiye wengine usumbufu.
> Zaidi ya kukuomba radhi hawa precision inatakiwa wakulipe pesa kufidia vyote hivyo ili hiwe fundisho tosha.
> Pole tena.
> --
> Sent from myMail app for Android
> Tuesday, 28 January 2014, 03:17PM +0300 from Tracy John Kimambo <tracykwetu@gmail.com>:
> Ndugu wanazuoni maelezo niliyotoa mtandao wa wanamabadiliko juzi Jumapili haya hapa chini.  Kesho Jumatano kwenye The Citizen , kama wataichapisha makala  ya column yangu, ninajadili  hoja kuu ya kisanga hiki ambayo ni swala la kutumia Kiswahili  kutoa maelezo kwa abiria anayekaa karibu na mlango wa dharura. Yule mhudumu alikuwa jeuri na mwenye kutoelewa maana ya kuwa mhudumu wa ndege lakini nadhani hoja kuu ni kwanini wahudumu wanaelekezwa eti lazima kutoa maelezo ya kufungua mlango wa dharura lazima kutolewa  kwa Kiingereza wakati maelezo mengine kwa abiria wote ni kwa Kingereza na Kiswahili?
> Tena MIMI NIMEWAHI KUTOA USHAURI  kama HUU HUU KWA MHUDUMU MWINGINE safari nyingine na yule mhudumu
> alinijibu kwa ukarimu kuwa yeye alikuwa anafuata maelekezo tu na mimi nikampa pole yakaisha. Huyu wa juzi alikuwa apendi kupewa maoni na mtu aliyedhani mtu wa hadhi ya chini sana kwake ...maana nilikuwa kama kawaida yangu naonekana kibabu tu kisichozoea mambo ya usafiri wa ndege.
> Kama wahudumu wasingekuwa wamefundishwa kikasuku eti lazima kutoa maelekezo ya kufungua mlango wa dharura kwa Kiingereza hakuna tatitizo sakata llote lisingetokea. Pia rubani naye angetumiabusara na kumtuma  afisa wa juu ndani ya ndege  kuhoji majirani wa nilikokaa angegundua yule mhudumu alikuwa mwongo tu maana hakukuwepo hata majibizano ya kupaza sauti kabisa... mimi nilibaki mdomo wazi aliponiambia yule mhudumu wa kwanza ninaweza kusimamisha ndege ukatolewa nje kama tishio na mimi nikamjibu kwa upole ya nini yote hayo ndugu yangu maana mimi najua Kiingereza na wewe endelea na maelezo yako kwa Kiingereza... lakini nadhani siku hiyo labda aliamuka vibaya ..Bado sijaamini angeweza kutunga uongo wa eti kuna mtu anafanya fujo vile tu nilitoa maoni yangu tu tena kwa tabasamu langu la kwaida ninapokuwa na huzuni juu ya mambo yasiyo na mantiki yanayotendeka duniani. MAELEZO YANGU YA JUMAPILI HAYA HAPA CHINI.
> "Yaliyonikuta Mwanza
> Nawashukuru wote kwa kunipa pole. Wanasheria wa  rafiki yangu binafsi Dr Antony Diallo, mmiliki wa Star Tv  na Radio Free Africa,  na wanasheria waliotumwa na Nd. Sungusia wa  Kituo cha Sheria  na  Haki za Binadamu ( Legal and Human Rights Centre, LHRC) chenye makao makuu Dar es Salaam   walifika kituo cha polisi cha kiwanja cha ndege Mwanza  na wakafanikiwa kuniwekea dhamana   na hivyo niko nje kwa dhamana vinginevyo ningelala selo ndugu zangu _Kesho nitaripoti polisi kufuatilia juu ya kesi iliyofunguliwa dhidi yangu na Precision  kama itaenda mahakamani au vipi.
> Kilichotokea kifupi ni hivi. Nilipanda ndege  Flight PW 0492 iliyotarajiwa kuondoka Mwanza saa 3  dakika 50 asubuhi  kuelekea Bukoba. Nilikuwa nimekaa kiti namba 2B na mtafiti mmoja anayefanya kazi Maruku Tea Estate huko Bukoba  alikaa kiti na. 2A kwenye dirisha kushoto kwangu. Wakati ndege inaanza kukuelekea inakoruka alikuja mhudumu wa kike akatuuliza na yule mwenzangu kama tunajua Kiingereza na mimi nikasema kwa utani huku nikicheka  kuwa tunajua kidogo. Yule muhudumu  gafla akatahamaki akasema kama sijui kiingereza aniamishe kiti.
> Mimi nikamjibu kuwa hakukuwa na haja maana mimi najua kiingereza  maana ni mwalimu wa siku nyingi wa Kiingereza lakini nilichokuwa nashangaa ni kwa nini nyie wahudumu mnapenda kutoa maelezo kwa Kiingereza wakati mgeyatoa maelezo hayahayo kwa Kiswahili mara baada ya kujua kuwa sisi ni Watanzania na tunajua Kiswahili vizuri zaidi kuliko Kiingereza. Binti huyo nikaona ametaamaki na kuanza kusema lazima niteremshwe.
> Mimi nilidhani masihala maana niliwahi kutoa ushauri huu hapo nyuma kwa mhudumu mwingine wa Precision Air  na yeye alinijibu kwa heshima kabisa kuwa wao maelezo wameambaiwa lazima wayatoe kwa Kiingereza.  Mara  yule mhudumu wa kwanza akaondoka akaja mhudumu mwingine wa kike akasema kama sijui Kiingereza niamishwe nikamjibu wa taratibu na tabasamu langu la kawaida ninalolitoa katika mazingira kama haya ya dalili za kukosekana busara  na  mtoa huduma kukimbilia  kwenye mambo ya kugombana bila sababu kuwa hakukuwa na tatizo jamani kwani Kiingereza nakijua  na nilichokuwa nimempa mwenzake ni ushauri tu.
> Yeye wala hata hakuzungumza na mimi tena aliondoka ndipo nikasikia rubani akitangaza eti kuna tatizo la kiusalama na ndege itachelewa kuruka ili litatuliwe. Mara polisi wane hivi  na muhudumu wa Precision wa kiume mmoja  wakaingia ndani ya ndege na kusimama mbele yangu nilipokuwa nimekaa na kufunga mkanda.  Mhudumu akaniambia inabidi au nikuamishwe kiti  au ni ushushwe. Wakati huo huo wale  polisi  wakang'angania eti lazima nishuke.  Nikauliza nitii amri ya nanai sasa?  Polisi mmoja aliyeonekana kama mwenye  kuwaongoza wale polisi wenziwe akainama akanifungua mkanda  wa kwenye ndge akaninyanyua  mkuku mkuku na  kunitoa nje ya ndege.Hata begi zangu mbili za mkononi ilibidi niombe nikiwa chini nipewe.
> Abiria waliokuwa karibi na nilipokuwa walishangaa na kusema kwani amefanya nini huyu baba . Lakini waliokuwa nyumba mabali hawakujua kilichotokea zaidi ya manaeno waliokuwa wamelishwa na rubani na wlae wahudu kuwa kuna baba kule mbele amnaleta fujo inabidi ateremshwe. Nikapelekwa kituo cha polisi hapo uwajani huku nikisikia wakinongonezana kuwa  lazima kuniweka  selo (lockup ).
> Nikafanikiwa kumpigia Dr Antony Dialo simu akazungumza nao wale askari na wakaanza kuchukua maelezo yangu nikiwa nimeketi ofisini kwao kwenye kochi walau badala ya kuwekwa lockup... Baadaye nilipigia Ndugu Sungusia wa LHRC  na Dr Antony Diallo wote wakanitumia wanasheria  walionisaidia kuandika na kutia saini maelezo yangu. Wale wanasheria wakaniombea dhamana nikapata nikaruhusiwa kutoka pale kituoni lakini nikaamriwa kuripoti kituoni pale asubuhi kesho Jumatatu kwa maelekezo zaidi.
> Wakati huo ndege ile ya Precision iliondoka ikaenda Bukoba na ikarudi tena baadaye kutoka Bukoba na ndipo nikamuona yule muhudumu wa kike wa pili eti ndiye anatoa maelezo juu ya eti mimi kufanya fujo. Yule muhudumu aliyewadanganya wenzake wote pamoja na rubani kuwa eti mimi nimefanya fujo wala hakutoka nje ya ndege iliporudi kutoka Bukoba kutoa maelezo.
> Katika sakata lote ili yule abiria aliyeketi kushoto kwangu siti namba 2A wala hakuhojiwa na  rubani wa ndege ile  kujiahakikishia kama madai ya eti mimi kufanya fujo yalikuwa ya kweli  na  wala hata polisi waliotekereza maelekezo ya rubani  yakuniondoa ndani ya ndege mkuku mkuku hawakujiangaisha kuuliza yule abiria jirani yangu aliye kuwa siti 2A  kama ni kweli mimi nilifanya fujo yoyote au nilitoa maoni tu juu ya matumizi ya Kiswahili katika  kutoa maelezo ya  juu ya kipi cha kufanywa wakati wa dharura.
> Hadi sasa bado sijaelewa kisa kilichomfanya yule mhudumu atahamaki na kunibambikizia tuhuma ya kufanya fujo yarabi... maana hakukuwepo hata na kubadirishana maneno kwa ukali kwa upande wake au wangu. Nimebaki nimeduwaha hadi sasa kuwa hivi ni kweli  miaka  zaidi ya 50 baada ya uhuru nimekatishiwa safari yangu kwa kutoa maoni tu ambayo mhudumu yule wa shirika la ndege binafsi angeweza kupuuza. Bado sipati maelezo kwa nini haya yalinitokea zaidi ya kuhisi kuwa haya ni matokeo ya mfumo wa kuandaa wahudumu wa ndege wa Precision unaowavimbisha kichwa kuwa kwa kutamka kwa rubani kuwa kuna abiria anafanya fujo hiyo inatosha abiria yule kunyanyaswa kama nilivyonyanyaswa na kudhalilishwa kwa kutuhumiwa kufanya fujo ndani ya ndege. Lazima nikiri hata hivyo kuwa maafisa Kadhaa wa kituo cha polisi cha uwanja wa ndege pale Mwanza walinionesha uungwana sana  na walikuwa wakarimu kwangu kuliko hata wahudumu wale wawili wa Precsion Air.
> Mwl. Lwaitama"
> JANA POLISI Mwanza WALIKUWA WAKARIMU MARADUFU NA WAMENIPA SIKU KADHHA ZA ZIADA ZA DHAMANA WAKATI WAKIENDELEA NA UPELEZI WA KAMA TUHUMA ZILIZOELEKEZWA KWANGU ZILIKUWA ZA KWELI. WATAWAHOJI WALIOKAA KARIBU NA MIMI NA SIMU ZAO WAMEPATA na sina shaka ukweli ukijulikana labda hata Precision watataka kuniomba radhi maana mimi ni mteja wao mkuu.
> Mwl. Lwaitama
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>  
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>  
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit  https://groups.google.com/groups/opt_out .
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment