Friday 28 February 2014

Re: [wanabidii] Re: [Mabadiliko] Neno Fupi La Usiku: Bunge La Katiba Na Kisa Cha Risasi Ya Mwisho...!

Dalili zote zinaonyesha wawindaji hawa watatuletea nyani badala ya nyati. Tangu juzi wanabishana ama kutumia kura ya wazi au ya siri. Mtikila Kawauliza mbona hata huyo Kificho (M/kiti) amepigiwa kura ya siri? Kundi kubwa la CCM wanataka kura ya wazi na wapo wengine wanaotaka kura ya siri wengi wakiwa wapinzani. Kwa vyovyote vile kipo kitu ambacho kimejificha na kuwafanya CCM wapendekeze kura ya wazi.

Hakuna hata mmoja mwenye hoja ya msingi juu ya kura ya wazi bali ubabaishaji tu. Eti kila mtu ajulikane yuko upande gani, kumbe tumewapeleka bungeni ili tuone sura zao tu?. Huo ni upuuzi mtupu, kama wanataka sura zao kuonekana sana wajiunge na vikundi vya kuigiza au music tutawaona kwenye CD au vipindi vya TV. Tunachotaka ni katiba nzuri siyo kuona sura zenu.

Hivi zoezi la kuhesabu watu zaidi ya mia sita litaruhusu kumuona vizuri kila mjumbe yuko upande gani? Kam akili zao ziko hivyo na kura za wazi zitaruhusiwa wapo watakaoamsha mkono juu mara mbili au zaidi maana shida yao ni kuonekana?

Hivyo kulifanya zoezi kuwa gumu na kuchukua muda mrefu. Hatutaki uzoefu mbaya wanaoutumia kwenye bunge la kawaida wa spika kuuliza wanaosema ndiyo, ndiyooooooo, wanaosema hapana hapanaaaaaa. Hivi intensity ya hizo sauti huwa anazipima vipi kama siyo mazabezabe? Mbona kupiga kura ya siri ni convenient kwa nini hawataki?  Wasitufanye watanzania mataahira wanachokusudia tumekwishakibaini. Wao ni wengi tatizo lao ni nini ziwe kura za wazi au za siri tunategemea matakwa yao yatatimizwa ya nini kujihofia?. Picha inayokuja ni kwamba wanataka kuwashinikiza wajumbe toka chama chao kufuata matakwa ya baadhi yao. Tunachotaka ni katiba ya maana siyo kuona nani kasema nini. wasifikiri wao ndo wenye hoja nzuri wapo watanzania wengi waliotoa hoja zao wakati wa kutoa maoni na wala hawakuwa na shida ya kuonekana kama wanavyotaka wao. Tafadhari fanyeni mambo ya maana badala ya mijadala isiyokuwa na kichwa wala miguu. Mukituletea nyani badala ya nyati ipo siku tutawadai fedha zetu mtakazokuwa mmelipwa


2014-02-28 0:39 GMT+03:00 Abdul Dello <abduldello@gmail.com>:
Tutaanza upya


On Friday, February 28, 2014, Maggid Mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com> wrote:


Ndugu zangu,

Leo katika nyakati tofauti nimefuatilia mjadala wa rasimu ya kanuni za Bunge hilo.

Kuna wakati nimejiuliza; hivi wote mle ndani wanajua maana ya dhamana kubwa waliyobeba kwa ajili ya nchi hii, leo, kesho na keshokutwa?

Kwamba hawapaswi kuonyesha aibu ile ya kujikita kwenye kujadili mustakabali wa taifa kwa kuvaa miwani ya makundi na vyama vyao vya siasa. Kuingia kwenye ushabiki kama wa Simba na Yanga. Maana, inahusua masuala ya msingi yaliyo mbele ya uhai wa vyama vya siasa.

Katiba ni dira ya nchi. Ni ramani ya kutuongoza Watanzania wa leo na wajao, bila kujali makundi na vyama vya siasa.

Kwa WaTanzania, madai ya kupata Katiba mpya ni madai halali yanayotokana pia na kukosekana kwa Haki, Uwazi na Uwajibikaji, hususan kutoka kwa baadhi ya wenye kupewa dhamana za uongozi.

Watanzania ni kama kisa cha wanakijiji waliokuwa kwenye shida ya njaa ya miaka hamsini. Na katika kuhangaika kwao,na kwa risasi yao ya mwisho waliyobaki nayo kwenye gobore moja na la pekee kijiji kizima, wamekaa kikao na kujadili wafanyeje ili wampate mwenzao atakayekwenda mbugani kuwinda mnyama ili aokoe njaa yao.

Na Jemedari wao, baada ya kutafakari, amewateulia mwenzao anayedhaniwa kuwa makini na mahiri kwa uwindaji. Mwenye uwezo wa kulenga shabaha, na hivyo, kuitumia vema risasi hiyo moja iliyobaki kwenye kumlenga nyati na kumwangusha. Kwamba abebe gobore lenye risasi moja, na aingie nalo msituni kuifanya kazi hiyo.

Aliyekwenda mbugani nyuma amewaacha wengi wenye matumaini ya kuusikia mlio wa gobore utakaoshiria mnyama mkubwa ameangushwa mbugani.

Na hakuna habari mbaya, kama wanakijiji wale watakapousikia mlio huo na kukimbilia mbugani kujionea. Na huko wamkute mwenzao ameitumia risasi ile ya mwisho kwa kumlenga na kumwangusha nyani badala ya nyati waliyemtarajia!

Na kwa mila za wanakijiji wale, nyani haliwi,na ni mwiko.

Na Bunge la Katiba lijione kuwa lina fursa adhimu ya kutimiza ndoto ya Watanzania ya kupata Katiba Bora yenye kukidhi mahitaji ya sasa na hata miaka mia moja ijayo.

Kwa Wabunge wa Bunge la Katiba kwenda Dodoma na kurudi na nyani badala ya nyati, sio tu kutawakatisha tamaa Watanzania, bali, kutawafanya Watanzania wawadharau Wabunge hao na hata kuhoji uzalendo wao kwa nchi yao waliyozaliwa.

Ni Neno Fupi La Usiku.

Maggid Mjengwa,
Dar es Salaam.
0754 678 252
http://mjengwablog.com

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la ‘Mabadiliko’.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
MUHIMU KWA WANACHAMA WOTE: Jukwaa hili litafungwa hivi karibuni hivyo hii ni taarifa ya Mwisho kwako kuhakikisha unajisajili www.mabadiliko.com
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.

For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment