Saturday 2 March 2013

[wanabidii] Vijana Tanzania tuinuke na kuwa sehemu ya mabadiliko ya kweli

Nataka kuona vijana wa Tanzania tunainuka na kuwa chachu ya mabadiliko ya kweli katika jamii zetu.
Tunahitaji mabadiliko ya kifikra katika nyanja muhimu mfano, kiucumu, kisiasa na kijamii.
Vijana tunaweza na tukisimama kwa umoja na kuiona Tanzania kama kiunganisho chetu tunafika mbali.

Natamani kuona siasa yenye kupeana changamoto ya kifikra kupitia sera ila lengo kuona tunakuwa na Tanzania bora yenye neema. Mungu ametujalia kuwa na wingi wa rasilimali za kila aina na ziko kona nyingi za nchi.

Vijana tuamke na kudai mabadiliko ambayo yanafaidisha jamii kubwa ya Watanzania.
Akina Nyerere, Mandela, Kwame Nkuruma, Martin Luther King Jr wote waligundua kuna kitu cha kuifanyia jamii wakainuka katika umri mdogo na kufukuzia agenda zao kwa manufaa ya jamii zao.

Wazee wetu naomba mtuunge mkono vijana pale mtakapoona tuko katika njia sawia. Tukoseapo naomba tuwe tayari kuonywa na kurekebishwa kwa nia njema ili tusimame na kupigania Tanzania na kuona kesho kuna kuwa na neema kuliko leo.
Tools kama Tanzania development vision 2025 ni moja ya funguo za kubua bongo pamoja na kufanya kila liwezekanalo kuona huo ndiyo mwelekeo wetu kama vijana na jamii yote katika ujumla wake.
Nawasilisha
 
Fred 
MATURITY does not come with age, it begins with acceptance of Responsibility
Change is Essence to maturation 

0 comments:

Post a Comment