Saturday 2 March 2013

[wanabidii] Neno Fupi La Usiku Huu; Afrika Mama Mkwe Anapokuja Dukani Kwako....!

Ndugu zangu,
Inahusu mila na tamaduni. Unafanyaje unapokuwa na duka na mteja aliye mbele yako ni mama mkwe wako?

Mwalimu, Profesa Mbele ameligusia hili la mila na destruri za Kiafrika kwenye kitabu chake kiitwacho African and Americans; Embracing Cultural Differences.

Kijinini unapokuwa na duka usifikiri tu hesabu za faida ya kibiashara, kuna hesabu za faida za kijamii pia.

Kawaida mama au baba wa mke uliyemuoa haji mwenyewe dukani kwako. Atamtuma mtu. Lakini siku ukimwona mkweo  amekuja mwenyewe ujue nyumbani mambo hayajakaa sawa.

Atakutajia mahitaji yake. Atajifanya pia yuko tayari kukulipa. Lakini, unachotakiwa kufanya, ni kuchukua mahitaji yote ya mkweo. Kisha utoka kabisa nje ya duka kumkabidhi mwenyewe kwa mikono yako.  Naye atajaribu kufungua mkoba wake atoe pesa. Umwombe radhi haraka, kuwa siku hiyo usingependa atoe hata senti tano!

Na usipofanya hivyo, mkwe atakuona kuwa ni mwanamme usie mwelewa  wa mila na desturi.

Maana, Afrika mkwe hawezi kuja mwenyewe dukani kwako, na akija, ujue kaishiwa....Usisubiri akwambie!
Ni Neno Fupi La Usiku Huu.
Maggid Mjengwa,
Iringa
http://mjengwablog.co.tz

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment