Saturday 2 March 2013

[wanabidii] Re: Vijana Tanzania tuinuke na kuwa sehemu ya mabadiliko ya kweli

Hatuwezi kuwa wote kwenye meza ya mabadiliko na kupigania mabadiliko
wengine waonyeshe mabadiliko kwa kutumia fursa zilizokuwepo kuanzia
bidhaa kwa ajili ya kuuza kwenye masoko na kutengeneza ajira zaidi kwa
vijana wengine , kwa wale wa TEHAMA wajiunge kwenye vikundi au waende
COSTECH kuna kitengo cha kuwezesha vijana wa TEHAMA katika
kijiendeleza na kuendesha biashara zao wafike pale waone wenzao
wanafanya nini .

Hatuwezi wote kuwa wanasiasa au kungangania kuwa kwenye vyama vya
siasa hapana tutumie taaluma zetu kujiendeleza na kuendeleza wengine .

On Mar 2, 11:53 pm, Fred Alphonce <fredrick197...@yahoo.com> wrote:
> Nataka kuona vijana wa Tanzania tunainuka na kuwa chachu ya mabadiliko ya kweli katika jamii zetu.
> Tunahitaji mabadiliko ya kifikra katika nyanja muhimu mfano, kiucumu, kisiasa na kijamii.
> Vijana tunaweza na tukisimama kwa umoja na kuiona Tanzania kama kiunganisho chetu tunafika mbali.
>
> Natamani kuona siasa yenye kupeana changamoto ya kifikra kupitia sera ila lengo kuona tunakuwa na Tanzania bora yenye neema. Mungu ametujalia kuwa na wingi wa rasilimali za kila aina na ziko kona nyingi za nchi.
>
> Vijana tuamke na kudai mabadiliko ambayo yanafaidisha jamii kubwa ya Watanzania.
> Akina Nyerere, Mandela, Kwame Nkuruma, Martin Luther King Jr wote waligundua kuna kitu cha kuifanyia jamii wakainuka katika umri mdogo na kufukuzia agenda zao kwa manufaa ya jamii zao.
>
> Wazee wetu naomba mtuunge mkono vijana pale mtakapoona tuko katika njia sawia. Tukoseapo naomba tuwe tayari kuonywa na kurekebishwa kwa nia njema ili tusimame na kupigania Tanzania na kuona kesho kuna kuwa na neema kuliko leo.
>
> Tools kama Tanzania development vision 2025 ni moja ya funguo za kubua bongo pamoja na kufanya kila liwezekanalo kuona huo ndiyo mwelekeo wetu kama vijana na jamii yote katika ujumla wake.
> Nawasilisha
>
> Fred
> MATURITY does not come with age, it begins with acceptance of Responsibility
> Change is Essence to maturation

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

0 comments:

Post a Comment