Sunday 10 March 2013

[wanabidii] RE: MAMBO MAKUBWA YATAKAYOINYIMA CCM USHINDI MWAKA 2015

-Unyanyasaji wa watumishi wa umma kwa kuwanyima mishahara stahiki, kuwatishia, na pengine kuwateka na kuwapiga.

 

-Kunyima vijana ajira kwa kuua viwanda, na mashirika ya Umma kwa kujifanya Serekali haitaki kufanya biashara huku watoto wa vigogo walitumia mwanya huo.

 

-Kutumia mabavu kudhoofisha Demokrasia Tanzania kwa kuwapiga na kuwajeruhi na pengine kuwaua waandishi wa habari.

 

-Kuua Viwanda vya nguo na Wakulima wake wa Zao la Pamba kanda ya Ziwa na kwingineko Tanzania.

 

-Kuua Viwanda vya Kahawa na Wakulima wake kanda ya Ziwa, Kilimanjaro, na ukanda wa nyanda za juu Tanzania.

 

-Kuwanyima Watanzania kufaidika na rasilimali zinazopatikana kwenye vijiji, Kata, Wilaya na Mikoa yanakotoka madini.

 

-Kumaliza kabisa Elimu kwa watu wenye kipato cha chini Tanzania huku watoto wa vigogo na wenye kipato wakisoma shule za gharama za juu na nje ya nchi.

 

-Kuliua shirika la Reli Tanzania ili kuwapa watoto wa vigogo fursa ya kutumia mwanya huo kusafirisha bidhaa.

 

-Kuua Shirika Reli na kutowachukulia hatua yoyote wahusika.

-Kuingiza Wawekezaji kwenye sekta zinazoweza kuendeshwa na Watanzania wenyewe Mfano: Utalii wa ndani.

 

-Kudhoofisha Demokrasia Bungeni kwa kuwanyima Wabunge wa upinzani kuihoji Serekali na pia kuwanyima kujadili hoja za msingi zikiwemo kushuka kwa elimu nk.

 

-Kupandishia Wananchi kodi kiholela na bei za bidhaa muhimu bila kuangalia uwezo na kipato chao.

 

-Kuruhusi watu toka nje kugawiwa na pengine kujinunulia ardhi kiholela na kujenga ndani ya ardhi ya Watanzania bila kuangali madhara ya baadae.

 

-Kujilimbikizia mali kwa viongozi waliopo madarakani na kuficha fedha nje ya nchi bila kujali madhara yake.

 

-Kujiuzia mali za umma vikiwepo viwanda, migodi, viwanja, nyumba, mashirika na mali zingine zilizojengwa kwa kodi za Watanzania kama Mahoteli ya Kitalii nk.

 

-Kumilikisha kwa Wageni mali zisizohamishika bila kushirikisha Watanzania waliolipa kodi.

 

-Viongozi kuwa na hisa kwenye kampuni mbali mbali na Migodi ya wawekezaji ili kutoa misamaha ya kodi isiyo na tija kwa Watanzania.

 

-Kuwakingia kifua wezi na wahujumu wa mali za umma walio na kesi za bandia mahakamani.

 

-Kutokukubali kuwa na tume huru ya kusimamia uchaguzi kama ilivyokuwa Kenya.

 

-Kutokukubali kufuta kifungu cha kumzuia Rais wa Jamhuri kushitakiwa endapo akienda kinyume na Katiba ya nchi.

 

-Kulitumia Jeshi la Polisi vibaya kwa kuwanyanyasa, na kuwapiga Wananchi wasio na hatia na wale wanaodai huduma za msingi kama mishahara, maji, umeme, tiba, elimu nk

 

-Kujihusisha kuingiza nchini bidhaa bandia zenye kuleta madhara kwa watumiaji.

 

-Kutodhibiti fedha za Kigeni kwa Wafanya biashara wa kigeni wanaotorosha fedha nje baada ya kuichuma Tanzania.

 

-Kujihusisha na biashara za kuwinda wanyama na pengine kuwasafirisha wakiwa hai jambo linalochangia kupunguza wageni nchini huku ikipandisha kiholela bei za kutembelea hifadhi za Taifa.

 

-Kuwanyamazisha Watanzania na vyombo vya habari kutoa taarifa za kweli na muhimu kwa kupitia magazeti na mitandao ya kijamii mfano. Gazeti la Mwanahalisi.

 

-Kutoendeleza Mashule na Viwanja vya ndege alivyoviacha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kunakosababisha kuzorota na kushuka kwa uchumi wa nchi. Kenya wameingia kwenye uchaguzi shughuli zote za Kibiashara zikasimama. Katuwezi kuendelea kuwa tegemezi kwa kulinda na kutetea Sera za Chama cha CCM.

 

Sera za watu wasio na upeo wa kuona mbali na kufanya mabadiliko ya Hali mbaya ya uchumi wa Watanzania. Mnatoa madini yetu mpewe magari ya kutembelea huku Watanzania wanakufa kwa njaa, maradhi, mishahara duni, makazi dun nk. Watu wabishi wasiotaka ushauri wa bure toka kwa Wapinzania. Ama zenu ama zetu. Mnarithishana wenyewe viti vya Urais. Watu wanaopendwa na Watanzania mnawapiga chini mfano: Lowasa na Sitta. Nyie ndio mna mali za kutia kiberiti na petroli endapo mkigomea matokeo masikini tuna mali gani?. Wafanyakazi muhimu wanakimbilia kufanya kazi nje kwa kunyimwa mishahara stahiki. Nyie mnajilipa mara mbili mbili. Mtu mmoja vyeo na mishara mitatu. Eti Mbunge, Waziri, Mwenyekiti wa bodi, Mjumbe wa Halimashauri kuu, Mkuu wa mkoa. Mnataka kutuambia wasomi nchi hii hakuna ni nyie tu.

 

Hakuna Mtanzania mwoga sasa hivi. Majirani zetu wa Kenya tumekaa nao wametufundisha ujasiri. Silaha ya unyonge wetu sasa ni umoja wetu Watanzania bila kujali Kabila, Dini, wala vyama. CCM mumeibia nchi sana sasa pumzikeni kama KANU.

Mkereketwa.

Gilliard David

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment