Thursday 7 March 2013

Re: [wanabidii] Re: [Mabadiliko] Mzee Makunga Mwananchi Mnatuangusha!

bandugu na hasa chambi chachage
 
unawaonea mwananchi, tafadhali usiwaonee mwananchi. siyo kila mhariri ni msomi wa uchumi na maswala ya uhusiano wa kimataifa nikimaanisha geopolitics kwa kiwango unachofikiria.
 
siyo kila mwandishi na mhariri ni mtaalamu wa worl affairs na current affairs hata kama tungependa iwe hivyo. kumbuka kwamba kiwango cha uandishi wa habari katika tanzania hakijafikia pale ambapo wote tungependa kifikie kwa maana kwamba kukawepo na specialization.
 
yaani mhariri wa siasa awe mhitimu mwenye experience ya political science, mhariri wa michezo akawa na uzoefu na shahada ya michezo, mwandishi na mhariri wa habari akawa mhitimu mwenye uzoefu wa habari, mhariri wa makala akawa mhitimu wa udaktari, mazingira, sheria, michezo, siasa na akapewa wandishi walio wahitimu katika nyanja hizo ili kilwa mwandishi aandike kile alichokisomea na kukipatia digirii. la hasha, hatujafikia kiwango hicho na sekta ya habari siyo pekee ambayo haijafikia kiwango hicho cha maendeleo.
 
ndiyo maana kutarajia kuwa mhariri wa makala wa mwananchi atagundua jinsi kingwangala anavyoegelezea katika makala yake is, to say the least, demanding too much from the poor mortal.
 
mimi ningefurahi sana tena sana na ningekupongeza na kukutumia shilingi mia nane za kununua sprite ya plastic bw. chambi kama haya uliyoyaandika kwenye mtandao ungeyaandika kwenye gazeti la mwananchi ili wasomaji wake wajue kuwa maandishi ya kingwangalla hayakuwa ya kwake bali kayaiba. kalifti kutoka kitabu cha wenzake akidhani ni yeye pekee katika tanzania anayesoma vitabu vya kingereza. nikubali kuwa ni wachache sana watz wanaosoma maandishi ya kingereza.
 
mfano mzuri wa hili ni wangu mwenyewe. nikiwa mhariri wa habari wa sunday citizen 2005 - 2007 niliandika habari za richmond, alex stewart assayers (ASA) na twin tower lakini miezi sita hadi nane baadaye habari ile ile iliposemwa bungeni na dk slaa tena baada ya kusoma gazeti letu nikashangaa kusikia na kusoma magazeti ya kiswahili eti, dkt slaa alipua bomu bungeni!!! stale news to us at mwananchi generally and sunday citizeni in particular was now a scoop!
kicheere, tungi, kigamboni, tanganyika territory
 
--- On Thu, 3/7/13, KIULA KIULA <p2k77@yahoo.com> wrote:

From: KIULA KIULA <p2k77@yahoo.com>
Subject: [wanabidii] Re: [Mabadiliko] Mzee Makunga Mwananchi Mnatuangusha!
To: "mabadilikotanzania@googlegroups.com" <mabadilikotanzania@googlegroups.com>, "Theo Makunga" <tmakunga@mwananchi.co.tz>, "Theophil Makunga" <themakunga@yahoo.co.uk>
Cc: "Wanazuoni" <Wanazuoni@yahoogroups.com>, "Wanabidii" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Thursday, March 7, 2013, 10:50 AM

Heko Chambi!


From: Chambi Chachage <chambi78@yahoo.com>
To: Theo Makunga <tmakunga@mwananchi.co.tz>; Theophil Makunga <themakunga@yahoo.co.uk>
Cc: Wanazuoni <Wanazuoni@yahoogroups.com>; Wanamabadiliko <mabadilikotanzania@googlegroups.com>; Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Thursday, March 7, 2013 4:41 PM
Subject: [Mabadiliko] Mzee Makunga Mwananchi Mnatuangusha!

Salaam Mzee Makunga! Kwanza, poleni kwa mapigo yanayowapata waandishi wetu makini. Pili, hongereni kwa kulizindua upya gazeti la Mwananchi likiwa na mvuto mpya na wa kipekee. Baada ya hayo naomba niwasilishe haya malalamiko yangu ya wazi.

Gazeti lenu tunalipenda sana kwa sababu ya umakini wake. Lakini hivi karibuni limekuwa likichapisha baadhi ya vitu ambavyo havijahakikiwa vizuri na kuthibitishwa kama ni vya kweli. Mfano wa kwanza ni wa hii makala hapo chini ambayo nimetumiwa na mwanafunzi wa zamani wa Chuo Kikuu husika. Ukitazama kwenye mfumo wa usajili wa wanafunzi wa Chuo hicho hao mapacha hawapo. Na kwa jinsi taarifa yenyewe ilivyo na kwa jinsi Chuo chenyewe na taasisi zake zinazoshughulikia masuala ya Afrika zinavyopenda kujisifu, kama hiyo taarifa ni ya ukweli hakika wangekuwa wameshaitangaza sana. Naomba mchunguze.

Mfano wa pili ni wa hayo maneno hapo chini kabisa kutoka kwenye makala ya Mheshimiwa. Nimemueleza ila anabisha kuwa hajaegelezea. Naomba uihakiki kwa kuilinganisha na nukuu niliyoiweka kutoka kwenye kitabu maarufu cha Profesa Daron Acemoglu na Profesa James Robinson. Ni aibu kuwaegelezea na kudhani wao au wafuasi wao (ambao ni wengi) hawatajua kwa kuwa kuegelezea kwenyewe kumefanywa kwa Kiswahili. Uvumilivu umenishinda ndio maana sasa nimeamua kulivalia njuga hili suala na kuliweka wazi. Tabia za kufumbia macho haya masuala na kuacha vitu viende hivi hivi tu ndio kunachangia sana kudorora kwa nchi yetu katika sekta ya elimu n.k. Tafadhali naomba muitunze heshima ya gazeti tulipendalo la Mwananchi.

MFANO WA KWANZA:

Pacha wa Kitanzania wenye vipaji vikubwa wang'ara Marekani

By  Mwandishi Wetu, Arusha

Imewekwa  Wednesday, March 6  2013 at  00:26
Vijana pacha wawili wa Kitanzania, Sylvanus na Salvanus wa umri wa miaka 21 wenye vipaji vya kipekee wanang'ara katika Chuo Kikuu cha Havard kilichoko Massachusetts, Marekani.
Salvanus anasomea udaktari wakati pacha wake, Sylvanus anasomea uhandisi kwenye chuo hicho.
Havard ni chuo kikuu cha bora cha tatu kwa ubora duniani, baada ya Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Massachusetts na kile cha Cambridge cha Uingereza.
Salvanus amekwishafanya upasuaji mkubwa kwa wagonjwa zaidi ya 14 huko Karatu na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Karatu, ambako pia upasuaji ulifanyika, Dk Lucas Kazingo alisema: "Hawa ni vijana wa ajabu, wana uwezo wa aina yake."
Salvanus yupo mwaka wa nne katika masomo yake ya udaktari. Sylvanus anasomea uhandisi wa kompyuta kwenye chuo hicho.
Vijana hawa wako nchini lakini chini ya uangalizi maalumu wa Serikali ya Tanzania na ile ya Marekani hasa kutokana na uwezo wao mkubwa wa kiakili.
"Vijana hawa, wamekuwa wakishirikiana katika kazi zao, ikiwamo ya udaktari na utafiti wa sayansi hali yao imewafanya sasa kuwa watu wa kipekee duniani," alisema Dk Kazingo.
Salvanus yupo katika mazoezi ya udaktari kwa vitendo na kabla ya kutua nchini, pia alifanya majaribio hayo Botswana.
"Walikuja ofisini, nimezungumza nao, kweli ninachoweza kusema ni kwamba wana uwezo mkubwa na ndiyo maana wanasoma chuo cha watu wenye vipaji maalumu cha Havard," alisema Dk Kazingo.
Wakizungumza na Mwananchi juzi, vijana hao ambao wamekuwa wakiishi pamoja kwa wakati mwingi, walisema walipata nafasi ya kwenda kusoma Marekani kutokana na msaada wa Rais Kikwete baada ya kupata taarifa za uwezo wao.
"Rais ndiye aliyetusaidia na anaendelea kutusaidia, hadi sasa tunaendelea vizuri na masomo," alisema Salvanus.
Hata hivyo, vijana hawa hawakuwa tayari kuelezea historia na maisha yao kwa sasa... "Nadhani tutazungumza zaidi baada ya kuonana na Rais, kuna tafiti tumefanya ambazo zimekuwa na mafanikio makubwa." Aliongeza Salvanus.
Meneja Uhusiano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Adam Akyoo alisema kwa sasa mamlaka hiyo, ndiyo imepewa jukumu la kuwasimamia vijana hao hadi watakaporejea chuoni.
Kutokana na hali hiyo wanatumia jina la Kawasange, pengine kama njia ya kuficha jina lao la ukoo wao kwa sababu za kiusalama.
Jina hilo ni la Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Ngorogoro anayeitwa Bruno Kawasange, ambaye ndiye mwangalizi mkuu wa vijana hao.
Akyoo alisema kabla ya kwenda Havard, walikuwa wakisoma Shule ya Sekondari Ilboru, Arusha mwaka 2004 hadi 2005. Pia walisoma Shule ya Msingi ya Arash wilayani Ngorongoro mwaka 1997 hadi 2003.
Aliongeza: "Salvanus amefanya upasuaji katika hospitali hii, kwa mafanikio makubwa hapa na mwenzake huwa anamsindikiza. Kweli hawa ni vijana wa aina yake na ni hazina kubwa kwa taifa."
Pacha hao ambao umahiri wao wa kutafiti umekuwa kivutio cha Kituo cha Utafiti wa Sayansi ya Anga cha Marekani (Nasa), wako likizo kwa sasa.
MFANO WA PILI:

"Hizi tofauti zinazoonekana leo siyo za kihistoria. Na kwa hakika hazikuwepo kabla ya ile vita kuu ya pili ya dunia. Kilichotokea baada ya mwaka 1945 ni kwamba hizi serikali mbili, ya Kusini na ile ya Kaskazini zilifuata mifumo miwili tofauti ya kiuchumi, moja ilijenga mfumo wake kufuatia mfano wa kiliberali wa soko huria lililoruhusu uhuru wa masoko na mitaji kama ule unaofuatwa na nchi za magharibi na marekani, na nyingine, Korea ya Kaskazini, ilifuata mfumo wa kikomunisti. Japokuwa marais wa kwanza wa Korea ya Kusini hawakuweka mfumo wa kisiasa wa kidemokrasia, wengine wanasema kwa kuhofia kuvamiwa na mfumo wa kitawala wa kikomunisti uliokuwa unasambaa kwa kasi sana maeneo ya Asia wakati huo, walisimamia mfumo wa soko huria. Marais hao, Syngman Rhee, ambaye alisomea vyuo mashuhuri duniani vya Harvard na Princeton, na mwenzake Jenerali Park Chung-Hee, ambaye ni baba mzazi wa Rais wa kwanza wa kike wa nchi hiyo aliyeshinda uchaguzi mkuu juzi tu hapa, wameingia kwenye historia za marais waliotumia nguvu kuongoza nchi yao na ikafanikiwa" - Hamisi Kigwangalla, Nini Sababu ya Umaskini au Utajiri wa Nchi? Mfano wa Tofauti kati ya Korea ya Kusini na Korea ya Kaskazini; Makala Mwananchi Alhamisi 10, January 2013 : Dr. Hamisi Kigwangalla's Round Table   

"These striking differences are not ancient. In fact, they did not exist prior to the end of the Second World War. But after 1945, the different governments in the North and the South adopted very different ways of organizing their economies. South Korea was led, and its early economic and political institutions were shaped, by the Harvard- and Princeton-educated, staunchly anticommunist Syngman Rhee, with significant support from the United States. Rhee was elected president in 1948. Forged in the midst of the Korean War and against the threat of communism spreading to the south of the 38th parallel, South Korea was no democracy. Both Rhee and his equally famous successor, General Park Chung-Hee, secured their places in history as authoritarian presidents. But both governed a market economy where private property was recognized, and after 1961, Park effectively threw the weight of the state behind rapid economic growth, channeling credit and subsidies to firms that were successful" - Daron Acemoglu and James Robinson's (2012) Why Nations Fail: The Origins of Power, Prosperity, and Poverty (pp. 71-72).
--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda; mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
 
TEMBELEA Facebook yetu:
http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
 
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forums" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 


--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment