Thursday 7 March 2013

Re: [wanabidii] Mzee Makunga Mwananchi Mnatuangusha!



On Thursday, March 7, 2013, Chambi Chachage wrote:

Kwa kweli ni aibu kwa habari kama hiyo ya hao mapacha 'wenye akili za ajabu'!!
 
  MFANO WA KWANZA:
Vijana pacha wawili wa Kitanzania, Sylvanus na Salvanus wa umri wa miaka 21 wenye vipaji vya kipekee wanang'ara katika Chuo Kikuu cha Havard kilichoko Massachusetts, Marekani.
Kwanza, hawa mapacha hawana jina lao la ubini?! Kweli huo ndio uandishi? Sylvanus na Salvanus waweza kuwa wengi tu hata pale Harvard!!
 
 
Salvanus amekwishafanya upasuaji mkubwa kwa wagonjwa zaidi ya 14 huko Karatu na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Karatu, ambako pia upasuaji ulifanyika, Dk Lucas Kazingo alisema: "Hawa ni vijana wa ajabu, wana uwezo wa aina yake."
Huyo Lucas Kazingo amepata wapi uwezo wa kusema, "hawa vijana wa ajabu, wana uwezo wa aina yake"!! Amegeneralise hata kwa pacha aliye mwandisi?! Amefahamu vipi umaajabu wa mwandisi katika pacha daktari kufanya upasuaji mkubwa wa wagonjwa zaidi ya 14?
 
Vijana hawa wako nchini lakini chini ya uangalizi maalumu wa Serikali ya Tanzania na ile ya Marekani hasa kutokana na uwezo wao mkubwa wa kiakili.

Kama alivyosema Chambi, kwa Marekani inavyopenda sifa ya kuonekana ina nurture watu wenye vipaji, hakika hawa mapacha wangekuwa headline makers siku nyingi tu! Na jambo jingine, tukizingatia safari za kaka mkuu kwenda Marekani, hawa mapacha wangekuwa wameshafotowa naye. 
"Vijana hawa, wamekuwa wakishirikiana katika kazi zao, ikiwamo ya udaktari na utafiti wa sayansi hali yao imewafanya sasa kuwa watu wa kipekee duniani," alisema Dk Kazingo.
Dk. Kazingo pamoja na mwandishi, tutafahamu vipi upekee wao katika utafiti wa sayansi duniani kama hamjasema majina yao ya ubini?
 

Wakizungumza na Mwananchi juzi, vijana hao ambao wamekuwa wakiishi pamoja kwa wakati mwingi, walisema walipata nafasi ya kwenda kusoma Marekani kutokana na msaada wa Rais Kikwete baada ya kupata taarifa za uwezo wao.
"Rais ndiye aliyetusaidia na anaendelea kutusaidia, hadi sasa tunaendelea vizuri na masomo," alisema Salvanus.
Hii hapo juu ndiyo pengine inaleta uwepo wa maswali mengi juu ya habari hiyo kuchapishwa!! 
 
Hata hivyo, vijana hawa hawakuwa tayari kuelezea historia na maisha yao kwa sasa... "Nadhani tutazungumza zaidi baada ya kuonana na Rais, kuna tafiti tumefanya ambazo zimekuwa na mafanikio makubwa." Aliongeza Salvanus.
Mtu aliye 'extraordinary brainiac' hawezi kukataa kutoa japo historia yake kwa ufupi. Kwani rais ndiye atawaambia nini cha kuzungumza juu ya historia yao? Hizo tafiti, bila majina ya ubini, zitafahamikaje kama zimefanywa nao?
 
Meneja Uhusiano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Adam Akyoo alisema kwa sasa mamlaka hiyo, ndiyo imepewa jukumu la kuwasimamia vijana hao hadi watakaporejea chuoni.
Kwa hiyo 'watasimamiwa' kwa pesa za Akyoo ama za NCAA? Kama kwa pesa za NCAA, huko 'kusimamiwa' kwao kulikuwemo kwenye mipango ya matumizi ya fedha za NCAA?
 
Kutokana na hali hiyo wanatumia jina la Kawasange, pengine kama njia ya kuficha jina lao la ukoo wao kwa sababu za kiusalama.
Sasa, kwa sifa walizotunikiwa, jina lao la ukoo lilikuwa muhimu ili tupate kujifunza zaidi kutoka kwa hawa 'mapacha wenye akili za ajabu'. 
Kwa hiyo wanalindwa kwa sababu wana akili za ajabu ama? 
 
Akyoo alisema kabla ya kwenda Havard, walikuwa wakisoma Shule ya Sekondari Ilboru, Arusha mwaka 2004 hadi 2005. Pia walisoma Shule ya Msingi ya Arash wilayani Ngorongoro mwaka 1997 hadi 2003.

Ina maana jamaa baada ya kumaliza darasa la saba, walisoma sekondari kwa mwaka mmoja tu, kisha wakaenda kusoma Harvard?
Historia yao ya elimu ipo nusunusu. Ina maana walienda kumalizia Harvard 'elimu ya sekondari?
Kama sasa wana miaka 21, ina maana walianza darasa la kwanza wakiwa na miaka mingapi? Kwa maana inaonekana walimaliza wakiwa na miaka 10-11!! Hiyo inawezekana kwa hapa Tanzania?
Labda kama alirushwa madarasa na vidato, jambo ambalo halijasemwa!
 
Pacha hao ambao umahiri wao wa kutafiti umekuwa kivutio cha Kituo cha Utafiti wa Sayansi ya Anga cha Marekani (Nasa), wako likizo kwa sasa.
Sasa hapa napo ni balaa. Mmoja daktari na mwingine mwandisi (ingawa haijasemwa nimwandisi  wa kitu gani); vitu ambavyo haviendani na NASA. Pengine labda huyu mwandisi kama ni mwandisi wa mambo ya anga, inakuwa sawa. Sasa kwa huyo daktari utafiti wake kuivutia NASA, inaleta utata. Pengine labda anafanya utafiti wa kidaktari kwa extraterrestrial being!!


--
Mathew Bukhi
Geography Department
University of Dodoma
P.O Box 395
+255 688 724063
Skype account: mathew.mabele.bukhi
Twitter account: Mathew Bukhi @atuyu

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment