Thursday 21 March 2013

Re: [wanabidii] Hili la watumishi wa umma wanaopoteza uaminifu na baadaye ati kushushwa cheo

Vigogo hawa wa Wizara ya Mambo ya Nje wapelekwe mahakamani

Yapo baadhi ya mambo yanayotokea Tanzania ambayo hakika hayawezi kutokea mahali pengine duniani. Ebu fikiria kisanga hiki. Pamoja na kuthibitishwa wizi wa zaidi ya Sh3.5 bilioni za Kitengo cha Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na waliohusika na wizi huo kujulikana, Serikali imesema haikuwafungulia watu hao mashtaka kutokana na kutokuwapo ushahidi wa kutosha.


Naibu Waziri katika wizara hiyo, Mahadhi Juma Maalim alisema hayo juzi mbele ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakati alipokuwa akijibu hoja ya Mwenyekiti wa kamati hiyo, Edward Lowassa aliyetaka kujua maendeleo ya sakata hilo na hatima ya maofisa waliodaiwa kuchota fedha hizo kwa ajili ya safari za Rais ambazo zilikuwa hewa.


Naibu waziri huyo alisema fedha hizo zilichukuliwa na maofisa hao kinyemela kutoka Hazina kwa ajili ya safari za viongozi za kufikirika tu, hivyo baada ya Wizara kubaini kwamba fedha hizo zilichotwa Hazina bila kuidhinishwa wakati Waziri, Naibu wake na makatibu wakuu wakiwa hawapo, iliomba msaada wa Takukuru ili kuchunguza zaidi tukio hilo.


Kwa mujibu wa kiongozi huyo, uchunguzi wa Takukuru ulibaini kwamba kweli fedha hizo zilichotwa Hazina kwa uzembe au kwa nia ya kuiba na ndipo wajumbe wa kamati hiyo walipohoji kwa nini maofisa hao hawakupelekwa mahakamani kama Takukuru ilikuwa tayari imebaini kwamba maofisa hao walikuwa wamechukua fedha hizo kwa nia mbaya.


Naibu waziri huyo alisema Takukuru ilishauri kuwa, licha ya wahusika wote kubainika kuhusika katika tukio hilo, ilikuwa ni vigumu kuwashtaki kwa kuwa hakukuwa na ushahidi wa moja kwa moja, hivyo ndiyo maana Wizara iliishia kuchukua hatua za kiutawala pekee. Kama ilivyotazamiwa, majibu ya Naibu waziri huyo yaliwaacha wajumbe wote wa kamati hiyo wakiwa katika mshangao mkubwa pasipo kujua nini la kufanya.


Tumeorodhesha mlolongo wa sakata zima la wizi huo kwa lengo la kuonyesha jinsi tatizo la ufisadi linavyozidi kuwa akubwa katika nchi yetu na jinsi vyombo vilivyoundwa kupambana na tatizo hilo vinavyoshindwa kutumia sheria zilizopo kwa visingizio mbalimbali. Fedha hizo zilizochotwa kutoka Hazina ni nyingi na wote waliohusika walipaswa kufunguliwa mashtaka.


Lakini pengine katika kuonyesha kwamba tukio hilo halikuwa la kwanza na kwamba nyuma yake ulikuwapo mkono wa baadhi ya watu wakubwa, maofisa hao hawakuchukuliwa hatua stahiki na baadhi yao hivi sasa wanaendelea na kazi zao kama kawaida. Takukuru inaposema hakukuwapo ushahidi wa moja kwa moja dhidi ya maofisa hao, inaonyesha bayana kwamba hali kama ndiyo hiyo vita dhidi ya rushwa na ufisadi haitafanikiwa katika nchi yetu.


Sakata hilo linatukumbusha wizi wa mabilioni ya fedha za Epa miaka kadhaa iliyopita, ambapo baadhi ya watu waliokwapua fedha hizo za umma na baadaye kuzirudisha hawakushtakiwa mahakamani. Hivi pia ndivyo ilivyo katika sakata hili la maofisa wa Serikali kukwapua Sh3.5 bilioni kutoka Hazina kwa ajili ya safari hewa za Rais.


Kwa kuwa wamezirudisha, Takukuru inasema wasishtakiwe kwa maelezo kwamba hakuna ushahidi wa moja kwa moja. Hiyo ni nini kama sio mwisho wa vita yetu ndefu dhidi ya rushwa na ufisadi?



2013/3/21 <lucsyo@gmail.com>
Wadau,

Mimi bado halijaniingia akilini; ninachoelewa mtumishi wa umma huwa anakula kiapo cha uaminifu pindi anapokabidhiwa kazi ya umma; sasa endapo atakiuka ama kuonyesha nia ovu ama kula njama kutenda kosa, huyo moja kwa moja anastahili aidha kuwajibishwa kwa kulazimishwa kujiuzulu ama kuachishwa kwa manufaa ya umma; sasa iweje leo hao wafanyakazi wa umma waliokula njama za kutaka kujichotea mabilioni ya shillingi bila hata ya chembe ya aibu kwa kutaka kuiba fedha za umma kwa kutumia jina la Raisi, ati washushwe vyeo!!!; jamani mie nadhani tufike mahali tuangalie na hizi sheria zetu za maadili kama vipi napendekeza zifanyiwe marekebisho na marekebisho hayo yaingizwe kwenye katiba mpya. Vinginevyo wanachi tuamini hapa kuna kulindana; watu kama hawa hawastahili kuwepo ama kukabidhiwa madaraka ya umma; sheria zetu ni mbovu ndio maana zinalinda ouvo; km zinashindwa kuwahukumu watu waovu kama hao

Regards,
Lucas
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom Tanzania

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.





--
RSM

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

0 comments:

Post a Comment