Monday 10 December 2012

[wanabidii] “Sisi wana CCM tunapaswa kutambua kwamba Tanzania siyo mali yetu” – Deo Filikunjombe - Mwanzo

MBUNGE wa Ludewa, Deo Filikunjombe (CCM) amekipasha chama chake, kwamba kimewafanya Watanzania waamini kwamba rasilimali za nchi ni mali ya chama hicho, jambo ambalo siyo sahihi.

Filikunjombe alitoa kauli hiyo Dar es Salaam jana jijini Dar es Salaam wakati wa kongamano lililoandaliwa na Kikundi cha Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDASA).

Alisema kwamba, kuna mitazamo imejengeka kwa wana CCM walio wengi, kwamba Watanzania wote ni mali ya CCM.

"Sisi wana CCM hasa wale ambao tumepewa ridhaa na wananchi kuwatumikia, tunapaswa kutambua kwamba Tanzania siyo mali yetu, hivyo jambo la muhimu la kufanya ni kutumia nafasi zetu kuwaongoza na kuwaletea maendeleo kwa kutumia rasilimali za nchi. Kwa mfano, hawa maprofesa wa chuo kikuu wana nafasi kubwa katika kulijenga taifa na kuandaa kizazi chenye elimu lakini utashangaa kuona wasomi ndiyo wanaalikwa kwenye harusi na kuchangia mamilioni lakini kwenye sekta ya elimu hawahudhurii. Leo kila mtanzania akiamua kuchangia Sh 24,000 ni dhahiri wanafunzi wa vyuo vikuu vyote nchini watasoma bure, hivyo tuungane tuijenge Tanzania,"alisema Filikunjombe.


http://wotepamoja.com/archives/10857#.UMbiAw8_tds.gmail

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 360,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment