Monday 10 December 2012

Re: [wanabidii] Nkrumah Hall Yesterday: One Of My Greatest Moments In My Life... I Wish My Father Was Alive.....!

Hongera sana Mjengwa.

Nilijifunza mambo mawili muhimu, ukitaka "presentation" yako "inoge"; i) Kwamba "practice makes perfect", hivyo kupanga "presentation" yako na kuirudia rudia kabla ya muda ni muhimu. ii)Timing; hakuna kitu kibaya kama kuambiwa kuwa una dakika mbili, nawe ndo kwanza uko nusu ya "presntation", of course, it goes back to practice. Mwisho, hakuna kitu kinatia raha, kama kumaliza kuongea, ukasikia makofi ya nguvu yanakufuata na hata mara nyingie "standing ovation", zikifuatwa na maswali mengi mengi; hapo unajua kwamba "you made it - you played your part". Hongera. LKK
 


From: maggid mjengwa <mjengwamaggid@gmail.com>
To: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>; mabadilikotanzania <mabadilikotanzania@googlegroups.com>
Sent: Monday, December 10, 2012 4:27 PM
Subject: [wanabidii] Nkrumah Hall Yesterday: One Of My Greatest Moments In My Life... I Wish My Father Was Alive.....!

to witness his son doing his very first live ( televised)public presentation. During my childhood at Ilala, I remember my late father, John Ramadhan Mjengwa telling me to follow him to a number of public rallies, at Jangwani grounds and even at the National Stadium.
I grew up at Ilala, Iringa Street, House Nr. 27. I remember, in the evenings, seeing my father, outside our Baraza, debating lively with his friends, on issues relating to social- political and even sports. And my father possesed some few political litteratures; books like, ' The Life of Patrice Lumumba' and the one, and banned one, written by John Okelo, ' The Zanzibar Revolution'. Surely, not only my mother, but, my late father, played a role in forming me to become the person I am today.

Na presentation ya jana?

Ilikuwa ni moja ya mitihani migumu kuipitia. Nilielewa dhamana na heshima kubwa niliyopewa; kwamba kwenye mwaka wa 51 wa Uhuru. Mwaka wa kwanza kuelekea miaka 50 ijayo, hivyo basi, miaka 100 ya Uhuru ifikapo Desemba 9, 2061, napewa jukumu la kutoa mchango wangu wa fikra juu ya Amani na Utulivu wa Taifa letu kwa miaka 50 ijayo.
Nilielewa, kuwa sitakuwa hai itapofika siku ya Desemba 9, 2061, lakini, historia itakuja kunihukumu kwa nitakachokisema kwa taifa katika dakika kumi nilizopewa.

Hivyo, kama ilivyo kawaida yangu, kwenye fikra zangu hakukuwa na Chadema, CCM wala majina ya wagombea Urais, bali, kwa siku mbili nzima za matayarisho, kichwa changu kilijaa fikra ya nchi yetu kwa miaka 50 ijayo. Ilihusu kuchangia ndoto ya taifa letu.

Kwa kawaida kwenye jambo zito lililo mbele yangu huwa kwa kiasi nafunga kula chakula pia. Jana asubuhi nilikunywa chai ya rangi isiyo sukari na vipande viwili vya vya tikiti . Mchana sikula chochote, nilikunywa maji tu.
Nilipofika Nkrumah Hall niliendelea kunywa maji. Chupa mbili nilizowekewa mezani nilizimaliza ndani ya dakika 20.

Nilitamani kuchukua chupa ya maji ya Profesa Gaudence Mpangala aliyekaa jirani yangu. Na alikuwa hajazifungua. Sikufanya hivyo, ingelikuwa utovu wa adabu.

Mara nilimwona ndugu yangu January Makamba akimalizia presentation yake. Nilifahamu kuwa inayofuata ni yangu. Mwenyekiti wa mjadala alishaninong'oneza, kuwa ningekuwa na dakika 8, lakini angeweza kuongeza 2. Nilimshukuru, maana, presentation yangu niliipangia dakika 8, na mbili za dharura, kama ingehitajika. Niliamua kuwa ningewasilisha bila kusoma kwenye karatasi. Kwamba ningeongea kutoka kichwani tu.

Nilichukua kipande cha karatasi kilichokuwa na mihili minne ya presentation, kunisaidia kama ingetokea nikapata ' break-down' kwenye kuwasilisha.

Na ndugu yangu January Makamba aliniumiza kichwa pale kwenye presentation yake alipogusia central theme ya presentation yangu. January aliongelea kidogo juu ya Haki pale unapojadili amani na utulivu. Na mimi nilipanga kujikita kwenye mambo mawili; Uzalendo na Haki. Bahati nzuri January alihama mapema kwenye reli yangu ya fikra. akaenda kwenye Elimu na Rasilimali. Nilipumua. Hivyo, alichogusia January kuhusu haki hakikuathiri flow yangu ya hoja.

Nikaanza presentation yangu. Niliyafanyia kazi mashaka ya sekunde za mwanzo kwa kumlink Dr. Semboja kwenye hoja ya kuwa na ndoto ya taifa na kuhusisha suala la rasilimali aliloliongelea Dr. Semboja. Nikawa comfotable katika hilo, hivyo, nikapata entry muafaka ya presententation yangu. Nikaendelea kujitahidi kuwa composed and focused.

Na presentation kufanikiwa ama kutofanikiwa huchangiwa pia na namna unavyoanza na kuhitimisha. Kichwani nilikuwa na mahitimisho mawili; moja la dakika moja na nusu, lingine la dakika 3. Mwenyekiti wa mjadala aliponiashiria kuwa zimebaki dakika 2, basi, sikuwa na wasi wasi. Nikaswitch kwenye hitimisho la dakika moja na nusu.

Nikahitimisha presentation yangu. Nikasikia ukumbi ukishangilia sana. Nikasema moyoni; Wow, I Made It! I realised that I did a more than a 'Ok' job.

For a while, my thoughts went to my late father, John Ramadhan Mjengwa. I realy wish he was alive to see and hear his son doing that presentation. And I dedicate to him , that piece of presentation I made for our country's future.

I thank you too, for following what I am doing.
Maggid Mjengwa,
Dar es Salaam.
http://mjengwablog.com
0788 111 765 --
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
DELL LATITUDE D 620 & D30
 
80 GB HardDisk ,CORE 2 DUO , 2.0 GHZ CPU ,1 GB RAM
DVD/CD - RW ,WINDOWS 7 /WINDOWS XP ,WIRELESS , BLUE TOOTH .
 
TSHS : 360,000 , 1 YEAR WARRANTY
 
CALL : 0786 806028
Free Delivery in Dar es salaam
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 


0 comments:

Post a Comment