Saturday 4 August 2012

[wanabidii] VIJANA NAO WAMTOLEA UVIVU MZEE MOYO



VIJANA NAO WAMTOLEA UVIVU MZEE MOYO
Wanasema kuwa Mzee Moyo:
·         Sio Mwana-mapinduzi wa kweli na hakuyajua Mapinduzi ya 1964
·         Mwezi moja kabla ya Mapinduzi ya 1964 alikipiga pande chama cha ASP
·         Alisherehekea kifo cha Wazanzibari Wana-mapinduzi cha akina Hanga na Othman Sherrif

Na Geofrey Kimbitikiri
August 05, 2012.

 
Pichani: Mzee Moyo akiwataka Vijana kuendelea na harakati za ukombozi wa nchi ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar

Zanzibar, Tanzania.
Katika mgeuko wa maneno vijana wa kizanzibari katika tovuti lao la Mzalendo.net wakitoa maoni yao chini ya mada –
"Muungano waibua mpasuko CCM Zanzibar" iliyotoka kwenye gazeti la NIPASHE, wamemshambulia vikali kikongwe wa CCM
Bw. Moyo kwa kile walichokiita kuwa Bw. Moyo ni mwenye siasa ya kurukaruka.

"Ni kweli tumshukuru Mzee Moyo kwa kutuunga mkono katika hii vita yetu ya ukombozi, lakini tusimuamini sana huyu Mzee,
kwani huu ndio mtindo wake. Kila akiona jahazi karibu ya kuzama huwa anarukaruka. 1964 alifanya haya haya dhidi ya ASP
na tukiwauliza wazee wa mitaani watatueleza zaidi."
Muandishi wa maoni haya anasema kuwa anashangazwa kuwa leo Mzee Moyo anataka Muungano wa Mkataba, kwani hataki
Zanzibar igubikwe na Bara. Huo ndio ulikuwa msimamo wa akina Hanga na Othman Sherrif. Walipomuona Karume anazidi kuelekea
Bara wakataka kumsimamisha na hapa ndipo walipokutwa na vifo vyao.
"Zaidi kinachonishangaza mimi ni kuwa haya haya anayoyaunga mkono yeye leo ndio akina Hanga na Othman Sherrif wakiyapigania",
anafafanua muandishi chini ya jina la kipiganaji (nom de guerre) la Saidi Sudi – ambalo ni jina la mwarabu maarufu wa zamani aliekuwa akiitikisha Unguja enzi zilizopita.
Muandishi anaendelea kuandika kuwa Bw. Moyo alishiriki katika mauaji ya Wana-mapinduzi hawa wawili, yaani Bw. Abdallah Kassim Hanga na Othman Sherrif
na siku ya mauaji hayo Bw. Moyo alivalia nguo za kijeshi akiwa na bastola kiunoni. Siku hio kama inavyojulikanwa kulikuwa na curfew Unguja nzima."
"Eh Mzee Moyo we, kaa kimya mzee wetu upate kusitirika!", alimalizia maoni yake muandishi huyo.
 
Na Geofrey Kimbitikiri.


0 comments:

Post a Comment