Sunday 12 August 2012

[wanabidii] Re: Tamko la DKt. Lwaitama na Prof. Shivji kuhusu habari ya "Shivji, Lwaitama wataka Muungano uvunjwe"

On Aug 12, 10:21 am, Yona F Maro <oldmo...@gmail.com> wrote:
> Tamko la Prof. Shivji kuhusu habari ya "Shivji, Lwaitama wataka
> Muungano uvunjwe"
> 09/08/2012
> JUU YA MUUNGANO: TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
>
> Nimeshitushwa na gazeti moja la kila siku  (Tanzania Daima la tarehe7
> Agosti 2012) lilonipandikizia maneno katika kichwa chake cha habari
> kwamba 'Shivji, Lwaitama wataka Muungano uvunjwe'. Siwezi nikamsemea
> Dr. Lwaitama lakini kwa upande wangu sijasema wala kumaanisha kwamba
> 'Muungano uvunjwe'.
>
>  Mosi, kwamba wasomi, wakiwemo wanahabari, wana jukumu zito la
> kutokupinda  ukweli wa kihistoria kwa lengo la kuhalalisha mtazamo na
> msimamo wao kuhusu  Muungano. Nikatoa mfano wa jinsi Merehemu Sheikh
> Karume anavyodekezwa  katika msimamo wake juu ya Muungano. Wasemaji
> hapa bara wanamsifu kwa kuwa  muasisi mwaminifu na mshabiki mkubwa wa
> Muungano tangu mwanzo. Huko  Zanzibar, wasemaji hawachoki kumnukuu
> Mzee Karume kuwa tangu mwanzo yeye  hakutaka Muungano isipokuwa
> alikuwa anafikiria Shirikisho.
>
> Wanaendelea kusema kwamba aliposaini Mkataba wa Muungano, Mzee Karume
> alifikiri kwamba anasaini Shirikisho la Serikali tatu, lakini kutokana
> na kiwango cha  elimu yake hakuelewa vizuri mantiki na maana ya
> alichokuwa anasaini.
>
> Nikaendelea kueleza kwamba maelezo haya yote mawili hayaungwi mkono na
> ushahidi wa kihistoria. Ukweli ni kwamba, Mzee Karume aliingia katika
> Muungano kutokana na hesabu zake mwenyewe za kisiasa. Muungano kwake
> ulikuwa njia ya kuondoa upinzani, au upinzani tarajiwa, wa utawala
> wake. Yaani ilikuwa ni tendo la mwanasiasa yeyote yule kudumisha
> utawala wake (political survival).
>
> Na kwa watawala wote wa Zanzibar waliomfuata, wakiwemo wa upinzani,
> ndivyo ilivyokuwa. Wamekuwa wakitumia mwavuli wa muungano wakati
> utawala wao uko hatarini na kushawishi wananchi wao dhidi ya muungano
> wakitafuta umaarufu wa kisiasa.
>
> Nikitoa mfano nikasema kwamba kuna taarifa kwamba chama kimoja huko
> Zanzibar kinapandikiza pendekezo la 'muungano wa mkataba, sio wa
> katiba' bila ya kueleza waziwazi maana yake. Ukweli ni kwamba huwezi
> ukawa na muungano wa mkataba bila kwanza kuuvunja muungano. Kwa hivyo,
> wanachoshawishi moja kwa moja ni kuuvunja muungano. Basi waseme hivyo
> badala ya kujificha nyuma ya pazia la 'muungano wa mkataba'.
>
> Jambo la pili nililorudia ni kwamba tuliangalie suala zima la muungano
> kwa mtazamo na maslahi na matakwa ya Umma wa Zanzibar na Umma wa
> Tanzania bara, hususan matabaka ya hali ya chini. Katika hali yao
> kimaisha – kiuchumi na kisiasa – hakuna tofauti kati ya wananchi wa
> Zanzibar na wananchi wa Tanzania bara. Uduni wa hali yao ni uleule;
> ukosefu wa ajira ni uleule; kutokuwa na mfumo wa dhati wa demokrasia
> unaojali walalahoi ni kulekule.
>
> Kwa hivyo, umuhimu kwao ni mshikamano wao kuboresha mifumo ya uchumi
> na siasa. Wasiburuzwe na wanasiasa na vyama vyao kwa maslahi yao
> binafsi ya muda  mfupi ya kudumisha, au kuingia kwenye, utawala.
>
> Jambo la mwisho nililogusia ni kwamba kiini cha suala la muungano si
> idadi ya serikali (mbili au tatu) bali ni mgawanyo wa madaraka
> (distribution of power) kati ya  dola la Zanzibar na dola la Muungano.
> Na katika hili kila muungano duniani ni wa kipekee kutokana na hali
> halisi yao ya kihistoria na uwiano wa kisiasa. Sisi pia
> tukiwashirikisha wananchi kikamilifu na tukaelewa vizuri matakwa yao
> tunaweza kubuni muundo wetu wa muungao ambao ni wa kipekee bila kujali
> idadi ya serikali.
>
> Nimeona niweke wazi mtazamo wangu kwa sababu ya baadhi ya vyombo vya
> habari kuwa na hulka ya kupotosha mambo kutokana na ushabiki wao bila
> kujali madhara  yanayoweza kutokea.
>
> Mwishoni ningependa kusema kwa dhati kwamba uvunjaji wa muungano
> hauwezi kuwa kwa manufaa ya walio wengi. Ukweli ni kwamba unaweza
> ukasambaratisha  nchi na jamii zetu pande zote mbili za muungano.
> Tukianza kubaguana kati ya Watanganyika na Wazanzibari, tutaendelea
> kubaguana kwa msingi wa Uislamu na  Ukristo, na Usukuma na Uchaga,
> Uarabu na Uafrika, weusi na weupe bila kikomo.
>
> Kama alivyosema Mwalimu, ukishaonja nyama ya mtu basi utaendelea
> kumtafuna.
>
> Issa Shivji
> Profesa wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere,
> Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
> Agosti 8, 2012
>
> On Aug 12, 10:13 am, Yona Maro <oldmo...@gmail.com> wrote:
>
>
>
>
>
>
>
> > 11/08/2012
>
> > *JUU YA MUUNGANO: TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI ***
>
> > Nimesikitishwa na aina ya uandishi wa habari  uliojiweka wazi  katika
> > taarifa iliyonukuliwa kuandikwa na  mwandishi  wa gazeti moja la kila
> > siku  (Tanzania Daima la tarehe7 Agosti 2012), Datus Boniface.  Huyu
> > mwandishi, pamoja na wahariri wake walioruhusu habari hiyo kuchapwa
> > walithubutu kusema uongo kuwa  eti " Dk Lwaitama, Prof. Sheriff na Prof
> > Shivji waliushambulia Muungano.." Tena, mwandishi huyu na wahariri
> > walioruhusu habari hiyo ichapishwe  wakaenda mbali zaidi na kutumia
> > kichwa  cha habari kilichosema eti 'Shivji, Lwaitama wataka Muungano
> > uvunjwe'.
>
> > Nafahamu Prof Shivji tayari ameisha toa tamko juu ya upotoshwaji wa hali ya
> > juu uliobebwa na kichwa cha habri hiki na makala nzima ya mwandishi huyu
> > mwenye aina yake ya ujuzi wa kuandika habari, Datus Boniface. Mimi katika
> > tamko langu sitojisemea mimi tu kama alivyosema Prof. Shivji katika tamko
> > lake. Nitajaribu kueleza kile ambacho nilidhani kilizungumzwa na kila
> > aliyechangia katika Mazungunzo ya yale ya Kifungua Kinywa       ( Breakfast
> > Talk), Jumatatu tarehe 6 Agosti 2012, yaliyofadhiliwa na Baraza la Habari
> > Tanzania( MCT).
>
> > Wakwanza kuzungumza alikuwa Prof Abdul Sheriff na aliainisha kile
> > alichotaka kibainike kama historian a sababu za kuwepo Muungano katika ya
> > Tanganyika na Zanzibar. Alieleza kile alichotaka kieleweke kama mapungufu
> > ya  kisheria katika mchakacho wa kuwepo Muungano. Pia alieleza kile
> > alichotaka kieleweke kama Muungano kukosa kuwa na uhalali wa kisiasa (
> > political legitimacy) kutokana na ushirikishwaji hafifu wa viongozi wa
> > Serikari ya mapinduzi wa wakati huo  na wananchi kwa ujumla. Akahitisha
> > maelezo yake kwa kusema Wazanzibari walio wengi sasa hivi wamefikishwa
> > mahali ambapo wanatamani kutumia mchakato wa kuandika katiba mpya
> > uliozinduliwa hivi karibuni unaoongozwa na Jaji SJoseph Sinde Warioba
> > kujaidili Muungano kwa kina na kuingia kwenye maridhiano mapya  juhuu ya
> > kama Muungano uendeleee kuwepo na kama ndiyo kwa mfumo wa serikali ngapi.
> > Ilikuwa wazi kuwa Prof Sheriff alikuwa hafikiri kuwa walikuwepo Wazanzibari
> > wengi waliokuwa tayari kuendelea na Muungano wa serikali mbili kama wa
> > sasa.  Si kumsikia mahali popote ambapo Prof Sheriff alitamka kuwa eti
> > anataka Muungano uvunjwe, yeye kama yeye. Sasa hyu mwandishi Datus Boniface
> > halipata wapi ujasiri wakumlisha mwanataaluma ya historia  huyu wa
> > Kitanzania, hata kama ni Mzanzibari pia? Ni uandishi wa habari wa aina hii
> > ni wa kusikitisha.
>
> >  Aliyezungumza wa pili alikuwa mimi, Dkt Azaveli Lwaitama.  Mimi kazi yangu
> > ilikuwa kujibu hoja za mzungumzaji mkuu ( Discussant) ambaye kwa kweli
> >  alikuwa Prof. Abdul Sheriff peke yake.  Kwanza nilimkosoa ndugu yangu
> > Mtanzania mwenzangu Prof Abdul Sheriff kwa kuomba wote tukubali kuwa
> > viongozi wetu waliotuunganisha kuzaliwa taifa letu la Tanzania walikuwa
> > watu walioongozwa na dhamira safi  iliyojimbuka katika kuwa waumini thabiti
> > wa itikadi ya *Umajumui wa Kiafrika ( Pan Africanism)* ya kutaka
> > kuwaunganisha watu wa dola zetu hizi waliokuwa wamekusanywa pamoja na
> > wakoloni na kupachikwa majina kama Tanganyika na Zanzibar bila ridhaa ya
> > wakazi walikuwa ndio  wengi wa sehemu hii ya Bara la Afrika wenyewe.
> > Nikaeleze jinsi mbavyo *mwelekeo wa viongozi hawa haukuwa wa kufungwa sana
> > na matakwa ya kisheria bali na kile walichokiamini kingesadia kufanikisha
> > lengo la kuwaunganisha Waafrika* wote bila kujali kabila ( tribe) au uzawa
> > ( race).  Nikatolea mfano wa jinsi Mwalimu Nyerere alivyoshirki katika
> > kuimiza kuungana kwa Shiraz Association na African Association kuzaa Afro
> > Shiraz Party ( ASP) tarehe 5 Februari 1959, siku na mwezi ambavyo mwaka
> > 1967 vilikuja kuwa siku na mwezi  wa kuzaliwa Azimio la Arusha , na mwaka
> > 1977 vilikuja kuwa ni siku na mwezi kilizaliwa Chama cha Mapinduzi kutokana
> > na  kuunganisha Tanganyika African National Union ( TANU) na Afro Shiraz
> > Party ( ASP).
>
> > Nilisisitiza kuwa leo tunaweza kuyaona wazi mapungufu makubwa katika *taratibu
> > za kisheria* zilizogubika mchakato wa kuunda Muungano lakini si vizuri
> > kukataa Muungano kutokana na mapungufu haya ya kisheria tukasahau kuwa
> > Muungano uliundwa kwa *sababu za dhamira ya kuunganisha Washiraz, Waafrika,
> > Waarabu, Wahindi na Wazungu  na kuwaweka pamoja kama Waafrika waumini wa
> > Umajumui wa Kiafrika (Pan Africanism),* wawe wa dola lilosimikwa na
> > wakoloni la Zanzibar au dola lililo simikwa na wakoloni la  Tanganyika.
> > Mwalimu Nyerere na Mzee Abedi Karume walisukumwa na kutaka kuunda taifa ya
> > Kiumajui wa Kiafrika jipya la TANZANIA, baada ya kuona Mzee  Jomo Kenyata
> > wa Kenya  na Ndugu  |Milton Obote wa Uganda   hawakuwa tayari kwa wakati
> > huo, mwaka 1964, kuunda dola jipya ambalo lingeongozwa na itikadi ya
> > vuguvugu la utaifa wa Umajumui wa Kiafrika ( Pan Africanist nationalist
> > movement) la Shirikisho la Afrika Mashariki. Kwa waasisis hawa wa Muungano
> > taratibu za kisheria hazikupewa kipaumbele bali dhamira safi ya kutenda
> > liloonekana kuwa la manufaa kwa wananchi walio wengi  wa sehemu hii ya
> > Afrika. Tukumbuke  kuwa Mzee Karume na Mwalimu Nyerere walikuwa wanafanya
> > kazi katika mazingira ya kivuli cha Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 1964
> > mwezi mmoja baada ya Uhuru wa Zanzibar tarehe 9 Desemaba 1963 uliopatikana
> > kwa kufuata taratibu za kisheria lakini matokeo yake yakapinduliwa kijeshi
> >  tarehe 12 Januari 1964 kwa vile taratibu hizo za kisheria zilitumika
> > kukwepa kupatikana kwa ridhaa ya kisiasa ya walio wengi katika kupatika
> > Uhuru ule wa Zanzibar wa Desemba 1963 !!
>
> >  Nilitumia muda kuelezea jinsi ambavyo
>
> ...
>
> read more »

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment