Sunday 19 August 2012

[wanabidii] RE: HAKUNA SABABU YA KUUNDA TUME KWA MWIZI WA MALI ZA UMMA

Mimi kama Mtanzania na Mzawa wa nchi hii nasema hakuna sababu ya wezi wa Mali za umma kuundiwa tume. Tabia ya kila kosa la jinai kama vile wizi wa viongozi waliopo madarakani kuundiwa tume ndilo linachangia kuwepo kwa rushwa nchini. Hakuna haja ya tume na kuingia gharama kulipa watu kuchunguza wizi. Ukishatajwa kuwa wewe mwizi ni kuondoka tu. Hakuna kiongozi amekatia uongozi wake lizi kwa Watanzania aongoze maisha. Umetajwa wewe mwizi au mhujumu uchumi ni kuondoka na mali zote kutaifishwa hata zilizo halali ndio watu waogope kukimbilia madaraka. Vinginevyo CCM lazima muondoke mpishe Watanzania wengine waongoze nchi. Mda wa kubembelezana umeisha.

 

Katika katiba tunayoiandaa sasa lazima kuweka bayana kuwa kila anayekula au kuiba mali za umma au kula rushwa sheria iweke wazi anachukuliwa hatua gani. Haiwezekani mwizi wa Kuku afungwe miaka saba lakini Mwizi wa Bilioni 90 anapeta uraiani. Hawa wamelirudisha nyuma Taifa na kuingia kwenye aibu. Hata ukiwa mtanashati kama wewe mwizi haisaidii kitu. Viongozi wa Tanzania tubadilike.

 

Haiwezekani mtu amekamatwa na mkono au kichwa cha binadamu awekewe zamana au kesi yake kuchukua zaidi ya wiki wakati ushahidi ni mkono au kichwa alichokutwa nacho. Serekali yetu ndiyo inafanya nchi inuke kwa rushwa. Sheria za nchi lazima zibadilike na zifanye kazi. Sheria zimepitwa na wakati. Wafungwa wa Kichina wanajenga magorofa hapa Dar es salaam na kwingineko hapa kwetu wafungwa wanakula kodi zetu bure. Tubadilike Watanzania na tuwe wabunifu. Mda wa kuvaa suti umepita. Kila Kiongozi mwenye Wizara awe mbunifu.

 

Tanzania inanuka kwa Wizi na Rushwa katika ofisi zote za Serekali kuanzia Ikulu na hii sio siri lazima tuambiane Wazi. Wizi umekuwa ni jadi ya viongozi wetu waliopo madarakani na hili lazima tulivalie njuga. Serekali inaishi kwa kukopa lakini viongozi hao hao ndio wameficha fedha nje ya nchi. Kila Mtanzania sasa ahakikishe anachukua maamuzi makubwa sana Mwaka 2015.

 

Tabia ya Serekali kusema haitaki kujiingiza kwenye biashara iache ndio maana na wizi unakuwa hauna mipaka. Lazima Serekali ifanye biashara ili iweze kujiendesha yenyewe. Kwani Serekali ikiwa na mashamba yake ya Ngano, Kahawa, Pamba, Katani, Korosho, Mpunga, haiwezi toa ajira kwa Watanzania. Msomi gani alisema akimaliza shule yeye hataki kusimamia watu wanaochuma Kahawa au Pamba. Nchi zingine Duniani zinaendelea kutokana na Kilimo Tanzania tunashindwa na kitu gani?. Ardhi tunayo, watu kibao kitu tumekosa ni Siasa safi na uongozi bora. Hatuna Siasa safi Tanzania na uongozi bora. Lazima tufufue viwanda vyote na Mashamba yote ya umma na kuanzisha mengine mengi tu. Tuache uvivu na woga wa kazi kwa kukimbilia kukaa maofisini.

Lengai ole Letipipi

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment