Sunday 19 August 2012

Re: [wanabidii] RE: KAULI ZA WAZIRI MKUU

Nilikuwa nimefanya makosa makubwa kutosoma maoni ya ndugu Lengai mpaka mwisho. Nakushukuru mwl Lwaitama kwa kunistua pamoja na ndugu Lengai kwa uchambuzi wa kina. Naungana nanyi kwa kusisitiza kwamba kauli ya waziri mkuu ni kauli inayotoka rohoni mwake na inaendana na wanachotegemea kufanya kwenye uchaguzi wa mwaka 2015. Kauli hiyo pia ni nyongeza ya kauli aliyoitoa wakati wa mgomo wa madaktari kwamba LIWALO NA LIWE.

Pinda anawaelewa sana watanzania kwamba si watu wa kufuatilia vizuri kauli wazitoazo viongozi. Kauli ya Liwalo na liwe iliondoka na maisha ya watanzania wengi, mimi mwenyewe niliondokewa na ndugu yangu hivyo nimekwishaonja shubili ya kauli zake vilivyo. Na wala siyo yeye tu ipo mifano mingi ya viongozi ndani ya serikali ya CCM wenye kauli design hiyo. Kwa vyovyote vile viongozi hao wamekwishajipa matumaini ya hati miliki ya uongozi wa nchi hii na ndiyo maana hawana haja ya kufanya aliyoyaorodhesha Lengai.

Katika hali ya kawaida tungetegemea watekeleze ahadi zilizopita na kuboresha maisha ya watanzania ili watakate mbele ya wapiga kura na kujihakikishia ushindi mwaka 2015. Kwa vile wanazo namna nyingi wanazozijua hayo kwao siyo ya msingi ili kubaki ikulu. Ningependa kusema kama CCM watafanikiwa kuchukua hayo majimbo na Ikulu mwaka 2015 kwa maneno na ujanja ujanja, huo hautakiwi kuitwa ushindi bali ni kitu kingine ambacho nashindwa kukipa jina. Si kitendo cha kiungwana mtu kutamba kwamba ushindi ni lazima kwa chama chako na kwamba utaendelea kushika hatamu wakati maisha ya watu wengi yanaangamia kwa sababu ya wachache. Inabidi tumuogope Mungu, maana akishusha hasira zake yatakuwa kama yale ya Idd Amini, SSeko tule, Sadam, Gadaff na wengine. Viongozi hao walikuwa na nguvu nyingi sana lakini waliishia kubaya. Mtu kama umekwisha pata angalia alama za nyakati ukiona ndo hivyo watu wamekuchoka kaa na  pembeni heshimu uamuzi wao hakuna sababu ya kulazimisha.

Wakati umefika kwa watanzania kuamua kusuka au kunyoa. Inahitaji uelewa kiasi fulani mtu kujua kama ananyanyasika, anaonewa na anapuuzwa. Wapo watanzania wengi wasiokuwa na uwezo wa kutambua hayo na ndiyo maana Pinda anatoa kauli hizo. Mtu akikosa elimu sahihi ujue huyo yuko kwenye sayari nyingine. Watu design hiyo ata mtandao kama huu hawana habari nao na pia ujumbe wa Lengai si rahisi wamiliki wa redio na magazeti wauweke maana wanaogopa kufungiwa.

Cha kumuelimisha Mzee Pinda ni kwamba majimbo yaliyo na watu anaowaita wapinzani nao pia ni watanzania wamechaguliwa na watanzania wenzao kama CCM inayahitaji majimbo hayo imalize kero alizozihainisha ndugu Lengai, wapiga kura watawapa bila umwagaji wa damu. Sina uhakika kama miaka iliyobaki itawatosha kufanya muliyoyahaidi ili mkubalike labda ifanyike miujiza. Pia kumbuka kwamba ata hayo majimbo yaliyochini ya CCM yako rehani kwa wapinzani mwaka 2015. CCM mkitaka kujua watanzania wamebadilika kiasi gani fanya tafiti acha kudanganyana kwenye vikao.

2012/8/19 Azaveli Lwaitama <kerezesia_mukalugaisa@hotmail.com>

Ndugu Lengai Ole Letipipi

Nimeguswa na ujumbe uliobebwa na Maoni yako kuhusu kauli za Waziri Mkuu Pinda. Nimependa zaidi uliponukuu Mwongozo wa Tanu wa 1970 kwa kuwaimiza Watanzania kusema : "Tumeonewa kiasi cha kutosha, tumepuuzwa kiasi cha kutosha na tumenyonywa kiasi cha kutosha. Sasa tunataka mapinduzi. Lazima Watanzania tufanye maamuzi mazito."  Nakupongeza kwa ujumbe huu. Tukiisha zalisha Watanzania wengi wenye mawazo kama yako, SAA YA UKOMBOZI ITAKUWA IMEFIKA. Sote tuongeze juhudi kuzalisha Watanzania wenye mawazo kama ya Lengai Ole Letipipi.

Mwl. Lwaitama

 


 

From: emmbaga@hotmail.com
To: wanabidii@googlegroups.com; info@butmaninternational.com; sematangotours@cybernet.co.tz; serenacarhire@habari.co.tz; sgresort@yahoo.com; sss@habari.co.tz; tours@albatros.co.tz; mia@albatros.co.tz; info@chadema.or.tz; rassingida@pmoralg.go.tz; mhariri@habarileo.co.tz; advertising@dailynews.co.tz; jennie@albatros.co.tz; shidolya@yako.habari.co.tz; sssafaris@cybernet.co.tz; s-s.kolowa@web.de; worldtourstanzania@hotmail.com; unasemaje@radiofreeafricatz.com; mwananchipapers@mwananchi.co.tz; globalpublishers@dar.bol.co.tz; educate@intafrica.com; costech@costech.opc.org; info@satif.or.tz; info@satf.org; eotf@raha.com; eotf@cats-net.com; zitto@chadema.or.tz
Subject: RE: [wanabidii] RE: KAULI ZA WAZIRI MKUU
Date: Sun, 19 Aug 2012 07:38:20 +0000

Ndugu

Lengai Ole Letipipi

 
 
Omeandika  ujumbe  wa  maana  sana  ambao  una  ukweli  hasa.  ni  jukukumu  lakila  atakae  usoma  na  kuuelewa    kuufanyia  kazi
Tanzania ni ya kila mtanzania na sio nchi ya baadhi ya watu 

 

.  naamini  kabiasa  Mungu  atawasikia  Wengi  wenye  Mapenzi  ya  ukweli   na  wanoumizwa  na  ubardhirifu  uliotendeka  naa  unaotendeka 
kwa  Visingizio  mbalimbali ,  Mungu  sio  athumani  siku  hio  inakuja
Ernest
 
 
 

 

Ndugu Watanzania mimi nilisikitishwa sana na Kauli za Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Peter Pinda kuwa Sera ya Serekali ya CCM ni kupita katika majimbo ya Wapinzani na hata majimbo yao kuhakikisha wanashinda katika uchaguzi Mwaka 2015. Kauli hii inamaanisha kwamba:

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kuruhusu kuboresha Katiba mpya inayoweza kusimamia masilahi ya wengi, bali kusimamia masilahi ya viongozi wa CCM.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kulipa Wafanyakazi wake malipo na mishahara sahihi inayolingana na kazi zao wanazofanya.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kuwataja watu walioficha fedha zetu nje ya nchi zaidi ya Bilioni 350.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kuwalipa Wazee waliokuwa wanatumikia Jumuiya ya Afrika Mashariki, wala mashirika mengine ya Serekali.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kuweka mkazo katika sekta ya elimu nchini. Madarasa, madawati, vyoo, vyote hivyo ni vitu vya anasa kwa Serekali sikivu ya CCM.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kuboresha huduma za tiba nchini. Wakiugua wao wanatibiwa nje ya nchi ila mwanakijiji akiugua anaachwa afe na ni mlipa kodi.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya juu. Ukiandamana kudai haki yako unamwagiwa maji ya pilipili uwashwe na ukamatwe uswekwe ndani.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kutoa huduma ya visima vya maji nchini. Lazima mwanakijiji utumie maji yanayotumiwa na mifugo yako.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini kuwazuia wawekezaji kuwakwapua Watanzania maeneo yao ya asili. Madini, na rasilimali za nchi ni za wawekezaji. Tanzania haifaidiki lolote na uwekezaji. Asilimia 3 haitoshi mtu kuchimba rasilimali za nchi. Kama tulisomeshwa kwa kilimo cha Katani, Pamba na Kahawa kwa nini madini na utalii visisomeshe watoto wa Kitanzania.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kufufua na kuendeleza viwanda watu wapate ajira. Matokeo yake thamani ya fedha imeshuka sana. Nchi inategemea wafadhili zaidi kuliko kuzalisha.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kumsaidia Mtanzania wa hali ya chini aweze kula milo mitatu kwa siku. Umasikini wetu umeletwa na wizi wa viongozi. Rasilimali za nchi zinanufaisha wageni. Madini, Wanyama, Misitu nk.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kusimamia mfumko wa bei za bidhaa nchini. Leo hii kuna Watanzania hawajui sukari ina ladha gani. Tusidanganyane. Lazima Serekali ya CCM inakula sahani moja na wafanya biashara wakubwa. Tuchukue tahadhari.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kusimamia uingizaji holela wa watu kutoka nchi za nje. Watu wanajijia hovyo na kujazana nchini na kuhamisha fedha za kigeni.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kuwataja na kuwashitaki watu walioiba mali za umma. Viongozi wamejiuzia mashirika ya umma, nyumba za umma nk.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kuzuia uwindaji na uuzwaji wa wanyama ambao kila kukicha idadi yake inapungua. Wawekezaji kwenye sekta za uwindaji wa Kitalii na Picha wanahamisha wanyama.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kufufua na kuendeleza mashamba ya Serekali ili kuzalisha chakula kwa wingi. Sera zao ni kuuza ardhi na kumilikisha ardhi kwa wageni.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kutekeleza ahadi zake za kufufua mashirika ya umma yaliyofilisika mfano: Shirika la reli na ndege. Sera zao ni kuwekeza hata pale anakonufaika Mtanzania.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kuingia kwenye ushindani wa kuboresha viwanja vya ndege. Kenya wanajenga kiwanja Taveta wao wanalalamika kwa nini wajenge karibu na kiwanja chetu nyie mnasubiri nini msikiboreshe.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kupunguza tofauti ya walionacho na wasio nacho. Watanzania wengi ni masikini. Tajiri ndiye anakopeshwa masikini anakimbizwa alipe kodi.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kuboresha makazi ya wapiga kura wake. Watanzania mpaka leo wanaishi nyumba za tembe wakati Viongozi wanaficha fedha ulaya.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kumaliza migogoro ya wafanyakazi ambao kila kukicha wanagoma. Sio kumaliza migogoro ya Wakulima na Wafugaji.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kumaliza tatizo la deni la Taifa. Nchi inadaiwa Trilioni 22 Serekali inaona ni sawa tu, na inaendelea kukopa na kujininulia magari ya kifahari.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kurekebisha bajeti ya nchi. Nchi inaendeshwa kwa fedha za wahisani. Nchi imefulia. Hazina hakuna kitu.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kupunguza utitiri wa wabunge bungeni. Nchi masikini lakini wabunge 400 na vikao visivyo na tija zaidi 66.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio sikivu na ni Serekali yenye kulindana na kutetea watendaji wabovu. Watu ni wezi wa mali za umma wanapewa madaraka. Fisadi anakuwa Waziri. Mwizi anakuwa naibu Waziri.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kuzuia viongozi wake wasile rushwa. Ndani ya CCM rushwa ni amri ya chama. Lazima ukiwa mwana CCM uwe unajua kula rushwa. Vinginevyo unatimuliwa chama.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio ya kuwalipa watumishi malipo mazuri bali kujilimbikizia mishahara minono na marupurupu kibao.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini na sio Serekali ya Watanzania bali ya Mafisadi. Ukidai haki yako lazima utekwe, upigwe, na kutupwa ufilie mbali.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kuacha ushabiki wa Siasa za ukandamizaji. Masilahi ya CCM mbele ndio Kiongozi atizame shida za Watanzania hasa katika jimbo lake.

 

-Sera ya Serekali ya CCM ni kuhakikisha wanashinda uchaguzi mwaka 2015 lakini sio kuwakamata watendaji wabovu ila kuwakingia kifua. Mapato na matumizi ya Serekali hayawekwi wazi.

 

Mwisho nataka niwaambie Watanzania wakati umefika wa kuwataja kwa majina watu wote walioibia nchi hii na kuhakikisha hawabaki madarakani mwaka 2015. Hakikisheni tunaweka sura mpya kabisa kwenye Serekali ijayo. Tanzania ni ya kila mtu na sio nchi ya baadhi ya watu. Kauli ya Waziri Mkuu ndiyo kauli ya Rais na ndiyo kauli ya wana CCM wote nchi nzima. Sera zao ni za kujilimbikizia mali na sio sera za kujenga nchi. Tukiendelea kuwapa madaraka tutakuwa tumeweka watoto na wajukuu zetu rehani na watakuwa watumwa baadae. Tumeonewa kiasi cha kutosha, tumepuuzwa kiasi cha kutosha na tumenyonywa kiasi cha kutosha. Sasa tunataka mapinduzi. Lazima Watanzania tufanye maamuzi mazito.

Mkereketwa.

Lengai Ole Letipipi


--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment