Friday 10 August 2012

[wanabidii] JE SISI MPAKA LINI?

Mkenya David Lekuta
Rudisha ameibuka kuwa
mwanariadha wa kwanza
kuandikisha rekodi mpya
kwenye mashindano ya
riadha katika michezo ya
Olimpiki, inayoendelea
jijini London Uingereza na
kisha kushinda medali ya
dhahabu katika mbio za
mita mia mbili.
Akiwa anashiriki fainali ya
michezo ya Olimpiki kwa
mara kwanza, Rudisha
mwenye umri wa miaka
23 alinyakuwa ushindi huo
kwa kuwa mtu wa kwanza
kukimbia umbali wa mita
mia nane kunako dakika
1, sekunde 40 nukta 91.
Mwariadha wa Botswana
Nijel Amos, umri 18,
alinyakuwa medali ya
fedha huku chipukizi
mwingine kutoka Kenya
Timothy Kitum, akiridhika
na medali ya shaba.
Mwingireza Andrew
Osagie alimaliza katika
nafasi ya nane lakini
akaweza kuandikisha
muda bora wa dakika
1:43.77.
Rudisha ambaye ni bingwa
wa dunia aliongoza katika
mbio hizo tangu mwanzo
hadi mwisho na kuwaacha
wanariadha wenzake kwa
tofauti ya sekunde 49.28.
Kisha akafyatuka katika
hatua za mwisho mwisho
na kuivunja rekodi yake
mwenyewe.
Huku kila mwanariadha
akiwa na msukumo wa
kasi ya rudisha, ni
Abubakar Kaki wa Sudan
tu ndiye aliyeshindwa
kuandikisha muda wake
bora licha ya kukamilisha
mbio hizo katika nafasi ya
saba.
Rudisha ameiambia BBC:
"Lo! Nimefurahi sana. Huu
ni wakati ambao
nimekuwa nikisubiri kwa
kipindi kirefu. Kuja hapa
na kuivunja rekodi ya
dunia ni kitu ambacho
bado sijaamini.''
" Nilikuwa nimejiandaa na
sikuwa na shaka kwamba
nitashinda. Leo, hali ya
anga ilikuwa nzuri na
niliamua tu kuparamia taji
hili."
Ushindi wa Rudisha bila
shaka ni habari njema kwa
Kenya ambayo kinyume
na matarajio, ilikuwa
imeandikisha matokeo
duni katika michezo hiyo
ya Olimpiki kwa kuwa na
medali moja pekee ya
dhahabu.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment