Friday 3 August 2012

[wanabidii] HOTUBAYA MGOMBEA NAFASI YA MAKAMU MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA- SANGOGUNGU KASERA

PRESS STATEMENT

HOTUBAYA MGOMBEA NAFASI YA MAKAMU MWENYEKITI WA UMOJA WA VIJANA
(UVCCM) TAIFA- SANGOGUNGU KASERA

2August 20112

Ndg:Wanahabari
Ndg: wanaUVCCM wenzangu

Kwa heshima na unyenyekevu mkubwa naomba kutoa salamu zangu za dhati
kwa Watanzania na vijana wenzangu wanchi hii pamoja nanyi waandishi wa
Habari kwa kushiriki nami katika safari hiiinayolenga kuunganisha na
kujenga hatua za mabadiliko ya maisha ya Vijana waTanzania. Kwa namna
ya pekee kabisa niwashukuru na kuwaomba mshikamano vijanawenzangu wa
Chama cha Mapinduzi ambao kupitia kwao ninatumia nafasi hii kuomba
ridhaa yao ili nipate nafasi ya kuwa chemchem ya mafanikio na
mabadiliko katika maisha yetu kwa kuanzia na chama chetu. Leo hii
naungana na vijana wenzangu hawa wa ndani ya CCM, kufanya jambo moja
kubwa, jambo la kuchukua fomuya kuwania moja ya nafasi kubwa katika
jumuiya ya Vijana wa CCM Tanzania. Ninafanya kazi hii leo nikitambua
mambo yafuatayo:

Kwanza, ninalenga kuleta mabadiliko yanayotazama aina ya vijana
tuliopo sasa, aina ya maisha tunayoishi na aina ya changanoto
zinazotukabili mimi nikiwa mmojawapo.

Pili kwa upekee mkubwa, nachukua fomu hii nikibaini hali ya vijana
huko tulikotoka na , changamoto tulizopitia na hatari inayotukabili
mbele kama hatua stahiki hazitaanza kuchukuliwa na vijana wa aina
yangu ambao tuna uzoefu wa kutosha wa maisha ya kawaida ambayo
yanahitaji nguvu na akili zetu na za wenzetu waliotutangulia katika
kuboresha maisha yetu ili tuweze kuwa raia wema katika nchi yetu na
wanachama waadilifu wa chama chetu na jumuiya zake.

Ndugu Waandishi wa Habari;

Kazi hii ya kuchukua fomu ninayoifanya leo hii na kisha kuanza zoezi
la kutafuta kuungwa mkono. Ni kazi inayohitaji ushirikiano mkubwa kwa
uongozi wa Jumuiya yetu pamoja na vijana mbalimbali bila kujali
itikadi zao za vyama vya siasa. Nasema hivi kwa kutambua kuwa UVCCM
ndiyo Jumuiya pekee yenye kubeba taswira na matarajio ya vijana wa
Tanzania na ambayo siku zote inatakiwa kusimamia maslahi na matakwa ya
vijana wa Tanzania na kwakuwa jumuhia hii ni jumuhia ya chama
kinachoongoza si chama tawala .

Ndugu zangu wanahabari na wana CCM tunafahamu tofauti kati ya kuongoza
na kutawala ndio maana nimetumia neno kuongoza, na Kama kazi hii
ilikuwa haifanyiki huko nyuma na kama ilifanyika bila kuridhisha, mimi
nimeamua kwa moyo mkunjufu kuingia kuonesha namna jumuiya yetu
itakavyoweza kuwatumikia vijana wa Tanzaniana kukiboresha chama cha
Mapinduzi ili kitambue wajibu wake kwa vijana wote waTanzania na kwa
kufanya hivi kiweze kusimamia misingi iliyolijenga Taifa hili na
kuachwa na waasisi wa Taifa letu Hayati Baba Wa Taifa na Hayati Rais
Karume ambao walilijenga taifa letu katika misingi ya haki, usawa na
ustahimilivu.

Ndugu wana habari; Katika kipindi hiki chakutafuta nafasi ya kuteuliwa
kuwa mgombea wa nafasi hii nitabakia kuongozwa na Moto isemayo: Vijana
kwanza kwa taifa lenye amani na maendeleo. Bila vijana kuangaliwa na
kupewa yale wanayostahiki, ni wazi taifa lenye amani na maendeleo
halitakuwepo. Natambua fika kuwa vijana wa Tanzania wanakabiliwa na
changamoto kubwa hasa ile inayolenga kubaini ndoto ya maisha yao ya
sasa na siku zijazo. Naamini mimi ni mmoja wa vijana hawa ambaye pia
ninahitaji kuona vijana walio katika kilimo basi wanaweza kupata soko
la mazao yao. Vijanawabeba mikokoteni nao wanafanya kazi hiyo kwa
miaka kadhaa na kisha kuboreshaajira zao.

Vijana wanaosoma basi wanahitimu vema na kupata ajira wanazostahiki na
pia walio makazini na waliopata nafasi za kuongoza wanaonesha mfano
wakufanya kazi kwa kujituma na kwa bidii ili kuonesha kuwa vijana
tunaweza na hatuwezi kuliangusha taifa. Natambua haya ninayoyazungumza
ni mambo magumu lakini pia natambua yanahitaji mbinu nyingi ili
kukabiliana nayo. Kwa sasa natumia nafasi hii kukiomba Chama changu,
kuiomba Jumuiya Yetu ya Vijana kutambua kuwa nina dhamira, nina nia,
nina sifa za kutosha, nina uwezo wa kufanya majukumu haya ninayoyaomba
na ninafahamu kazi za majukumu haya.

Tena nina rekodi katika umri wangu huu wa kufanya mambo ya kutukuka
ambayo rekodi yake inaweza kutazamwa pote nilipobahatika kutoa
utumishi wangu. Kwa namna isiyoonyesha kuyumba naomba kuwaeleza vijana
wenzangu kuwa kutokanana mshikamano wa vijana wenzangu kwangu ni wazi
tumejiandaa kushinda katika nafasi hii ili tuweze kuleta mwanga wa
mabadiliko katika jumuiya yetu na chama chetu katika maandalizi ya
chaguzi zijazo. Ndugu wanahabari ninatambua zipo changamoto nyingi
zinazoikabili UVCCM na changamoto hizi zinahitaji kiongozi ambaye
atakuwa na uthubutu wakuweza kukabiliana nazo, changamoto kuuni
kitaswira, kimuundo, kiimani, kimadhumuni kama ambavyo zimehainishwa
kwenyekanuni za ummoja wa vijana. Nina maanisha nini ninapozungumzia
taswira ya UVCCM.Taswira ya UVCCM Taifa leo siotaswira ya kimapambano.

Historia yetu ipo wazi jumuiya ya vijana ilishiriki katika mapambano
ya kuleta Uhuru, Umoja na mshikamano mtakumbuka wakati TANU
Inahangaika na kutafuta Uhuru wa Tanganyika na Afro-Shirazi party
ikipambana kuleta Uhuru wa Zanzibar vijana waliunganishwa na jumuiya
za umoja wa vijana wa vyama hivi viwili ambavyo ni TANU YOUTH LEAGUE
na ASP YOUTH LEAGUE, zinafahamika kazi zilizofanywa na wabeba mizigo
wa Kariakoo mfano Mzee Rajabu Diwani, leo UVCCM sio tena yawabeba
mizigo, sio tena ya wamachingasio tena ya wakulima ,sio tena jumuiya
ya wafanyakazi ni jumuiya ya wafanyabiashara, watoto wa vigogo ama
wenyenasaba nao ama rafiki zao, inahitaji viongozi wenye dhamira ya
dhati ambao watarudisha jumuiya hii kwa vijana wakitanzania na
kurudisha taswira ya kimapambano ambayo ni mapambano ya kiuchumi, kazi
ya Uhuru imeshafanyika imebakia jukumu la kuleta Uhuru wa kiuchumi na
kuwa kimbilio la vijana wote.

Ni dhamirayangu ya kugombea nafasi hii ni kuhakikisha awamu ya pili ya
mapambano ya kiuchumi ya umoja wa vijana inaanza rasmi. Nafahamu zipo
changamoto za kiutawala, kiuchumi na jumuiya kuendelea kuishi kwa
kutegemea misaada na Ruzuku kutoka kwenye chama, nafahamu
watendajiwana hali mbaya kiuchumi hasa katika mawilaya, nafahamu ofisi
zetu za wilaya zina upungufu wa vitendea kazi ni dhamira yangu
kubadili mwelekeo wa utendajiwa jumuiya yetu kutoka "Business as
usual" kuvalisha skafu viongozi na kuimba nyimbo, kuwa jumuiya yenye
dira namwelekeo sahihi wa kuwaunganisha na kumkomboa kijana wa
kitanzania.

Ndugu waandishi wa Habari; Ninafahamu matarajio yavijana wa kitanzania
yatafikiwa kupitia CCM imara na CCM inatokana na uimara wajumuiya zake
kuwa imara na hili inawezekana kwa kupatikana viongozi Imara na mimi
nina amini ni mmoja waviongozi ambao wataifanya jumuiya yetu kuwa
Imara.

Kwa kuhitimisha Hotuba yangu naomba kutoa shukrani zangu kwa Mwenyezi
Mungu kwa kunifanikisha kuwananyi hapa, niwashukuru wana familia
yangu, marafiki na nyie ndugu zanguwaandishi wa Habari kwa kukubali
kujumuika nami kunisikiliza leo. Niwaombe Vijana wenzangu wa CCM
kuniunga mkono katika azma hii kubwa niliyo nayo na niwakumbushe tu
kuwa, zoezi hili la kuchukua fomu nililofanya hapa leo si langu bali
la vijana wote wa Tanzania wakiwakilishwa na Vijana wa Chama cha
Mapinduzi.

Ni imani yangu kuwa, wana UVCCM hawatakubali kuangusha taa
hiiwaliyoiwasha kule Rorya mkoa wa Mara wao wenyewe na badala yake
wataungana namibega kwa bega ili kuufikia ushindi. Tutapitisha fomu
hii pamoja nao, tutachujwa pamoja nao na kisha tutashinda pamoja nao
na kisha kuanza kuwaongoza vijana wa Tanzania pamoja nao. Mwenyezi
Mungu Mwingi wa Rehma atubariki na kutupa nguvutufanikishe azma hii
muhimu pamoja. Kidumu Chama cha Mapinduzi

Asanteni kwa kunisikiliza.

Mimi Ndg Sango Gungu Kasera- Mjumbe Mkutano Mkuu UVCCM (W) Rorya

Kauli mbiu Mbiu "Vijana kwanza kwa taifa lenye amani namaendeleo''.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment