Friday 24 August 2012

Re: [wanabidii] Wakazi wa Bonyokwa tunahitaji msaada wa kutengenezewa barabara

Ni Kweli Barabara hii inatia kero sana,
 
nami ni mkaazi wa maeneo hayo, ila nilisoma juzi Mnyika alisema barabara hizi ziko chini ya TANROAD sasa, and serikali imetenga 10Bilion kwa ajili ya kuzitengeneza, lengo ni kupunguza folleni,
 
I hope by Sept, 2nd Quarter fedha hizo zitatoka na kazi itaanza, ila wazo la kuchanga ni jema sana, Halmashauri ina Greda na Derever, so tunahitaji mafuta tuu, like 2M will be more than enough.....

2012/8/24 Matthew Mdidi <matthew.mdidi@yahoo.com>
Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Kimara, barabara ya kwenda Bonyokwa kuanzia eneo la Kimara Mwisho ina hali mbaya sana.
 
Kwa kuwa nafahamu serikali yetu haina pesa za kugharimia huduma muhimu za jamii niko tayari kuwahamasisha wenzangu tuchange pesa za kununulia dizeli kwa ajili ya greda la kusawazishia barabara hiyo.
 
Kama Mbunge wangu utakuwa umebanwa na majukumu mengi ya Kitaifa, unaweza kumtuma Diwani wetu apite nyumba hadi nyumba kuchukua michango hiyo.  
 
Kama Mheshimiwa Diwani naye atakuwa amebanwa sana, naamini Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wetu anaweza kutuchangisha pamoja na kuwa anatoka Chama Cha Mapinduzi.  
 
Kama haya yote yatashindikana itabidii umwombe Mama Salma Kikwete atembelee tena eneo letu ili barabara hii itengenezwe usiku na mchana.
 
Tunaomba ulipe umuhimu hili wasije akina Nchemba wakapata la kuongea. Asante sana Mheshimiwa.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
0 comments:

Post a Comment