Saturday 18 August 2012

Re: [wanabidii] TANZIA - ALFRED MBOGORA AFARIKI DUNIA

Huo ni msiba mzito kwa tasnia ya habari. Mwenyezi Mungu awapatie nguvu ndugu wa marehemu

Sent from my iPad

On Aug 18, 2012, at 11:51 AM, Nico Eatlawe <eatlawe@yahoo.com> wrote:

Poleni sana kwa msiba wa mwanahabari. Inasikitisha kuona jinsi mshumaa ulivyozima ghafla. Lazima chakula hicho kilikuwa na kitu!

From: Peter Lwegasira <petermakatu@yahoo.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Saturday, 18 August 2012, 9:40
Subject: Re: [wanabidii] TANZIA - ALFRED MBOGORA AFARIKI DUNIA

Poleni sana wanafamilia na wanahabari wote. Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi.
Raha ya milele ampe eeh Bwana. Na mwanga wa milele amwangazie. Apumzike kwa amani. Amina.

From: Neville Meena <nevilletz@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Saturday, August 18, 2012 11:09 AM
Subject: [wanabidii] TANZIA - ALFRED MBOGORA AFARIKI DUNIA

Wakuu,
Habari za leo, habari za Jumamosi,
Tumepata taarifa kutoka Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwamba mmoja wa maofisa wake na Mwanahabari na Mhariri wa siku nyingi, Alfred Mbogora amefariki Dunia leo saa 11.00 alfajiri katika hosipitali ya Taifa ya Muhimbili.
 
Katibu Mtendaji wa MCT, Kajumbi Mukajanga amesema kwamba Mbogora alilazwa Muhimbili tangu Jumanne baada ya kuwa ameanguka katika eneo la Tegeta, mara baada ya kupata chakula wakiwa njiani kwenda Bagamoyo kwa shughuli za kikazi.
 
Kabla ya kuanguka, Mbogora alikuwa akilalamika kwamba anasikia kuishiwa nguvu kwenye mguu na mkono na alipojaribu kusimama ili kutembea kutokana na hali aliyokuwa akiisikia mwilini alianguka.
 
Tangu wakati huo (baada ya kuanguka) alikata kauli na hakuwa kusema chochote hadi hapo alipokata roho leo alfajiri. Ni pigo kwa sekta ya habari nchini, kumpoteza mwanahabari mwenzetu ambaye ametoa mchango mkubwa katika sekta yetu ya habari.
 
Inasadikiwa kwamba msiba wa Mbogora uko nyumbani kwake Segerea, lakini taarifa zaidi tutazipata kadri tutakavyoendelea kuwasiliana na MCT pamoja na familia ya marehemu.
 
Tunachukua fursa hii kuwapa pole wafiwa wote, kwanza ni familia ya marehemu, MCT na wanahabari wote nchini. Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake luhimidiwe, Amen.

--

--
Neville C. Meena,
Secretary General,
Tanzania Editors Forum - TEF,
Dar es Salaam - Tanzania.
Cell: +255 - 787 - 675555
        +255 - 753 - 555556
 
--
Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/
Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/
Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
0 comments:

Post a Comment