Tuesday 28 August 2012

Re: [wanabidii] Sensa na Swali la Dini..................UKWELI NI HUU!!!

Baada ya kusoma habari iliyonukuliwa toka kwenye blog ya Zanzibar ni kwetu, nimepata majibu ya maswali niliyokuwa najiuliza kuhusu baadhi ya waislamu kugomea sensa. Japo majibu hayo yanazua maswali mengine ya kutisha. Hivi mtu anavyodai kuwa misrepresented kidini katika nafasi mbalimbali za kisiasa na kwenye ajira anakuwa na maana gani? Nijuavyo mimi kama ni mambo yanayohitaji kupata maoni ya viongozi wa dini, dini zote kubwa huwa zinahusishwa. Hapo napata wazo kwamba kumbe ata kwenye uchaguzi wa nafasi za kisiasa wapo wanaochagua dini badala ya mtu alimradi wawepo wawakilishi wengi wa dini yake katika siasa. Tulio wengi hatumchagui mtu kuwa diwani au mbunge ili akatuwakilishe kidini kwa vile hatumchagui audhurie mikutano ya uwakilishi wa kidini

Kuhusu leseni za biashara sioni ni wapi dini inatakiwa maana mambo yote ya msingi yanakuwa yamefikiriwa kama ni sehemu iliyopimwa basi kuna eneo la makazi ya watu, kuna maeneo ya biashara, maeneo ya wazi na maeneo ya kuabudia. Hivyo hakuna sababu ya kujua dini ya mtu. Kwa mtazamo ulioonyeshwa kwenye hizo hoja ata makazi ya watu itabidi yatengwe kwa misingi ya dini ya mtu. ata kwenye nyumba za kupanga itabidi mtu aulizwe dini yake kwanza nk

Kuchoma makanisa eti kwa sababu yako kwenye maeneo yenye waislamu wengi nayo ni hoja hafifu. Hivi sauti zinazotoka kwenye vipaza sauti vya misikiti mbalimbali wakati wa swala, tunafikiri kila mtu anapenda sauti hizo? unasemaje juu ya misikiti itayoonekana imejengwa kwenye maeneo yenye wakristu wengi? Ni jambo la kuvumiliana kiimani kwa vile Tanzania siyo nchi ya kiislamu wala kikristu. Watu wote wanaoonyesha kukerwa sana na imani za wenzao na kutotaka kuchanganyika nao ni watu wenye kujipenda kupindukia, ni vyema wakasoma historia vizuri juu ya ujio wa hizo dini wanazojifanya wao ndo waanzilishi na kuanza kubaguana kwa vigezo vya udini

Kupitia makala hiyo nimefahamu kisa kizima cha kug'ang'ania kipengele cha dini. Tatizo kubwa hapa linaonekana ni kutaka nchi itamke kwamba ni ya kiislamu. Musitake kuiga mambo yasiykuwa na asili ya Tanzania, watanzania ni ndugu moja na ndiyo maana tunasema tuna mila na desturi zetu. Ndicho kitu kinachotufanya tuitwe watanzania na wala siyo dini tulizoziridhi toka nje. Wapo babu na bibi zetu waliozaliwa na mama mmoja na baba mmoja lakini leo  ndugu hao si waumini wa dini moja. Ni vyema tukafuata imani zetu kwa kuvumiliana siyo kulazimishana. Acha kutuletea mifano ya India, uingereza na Marekani maana wanazokatiba na taratibu zao tofauti na sisi. Wanavyo hadi vifungu vya kuruhusu ushoga na mabo mengine machafu navyo munataka tukaviige?
Kama hoja zenyewe ni hizo kumbe kuna kila sababu ya kutoweka kipengele cha dini katika sensa ya taifa. Siku zote ninasema kwamba matatizo yetu ya kiuchumi na kijamii kwa sasa siyo kwa sababu ya tofauti zetu kidini ni vyema tukajikita kutafuta vyanzo halisi badala ya kukaririshwa na wenye agenda zao za siri



2012/8/28 John Nkumbaruko <nkumbaruko@yahoo.com>
Wandugu,
Ninajua kuwa kwa kutoa posting hii ninajiweka kwenye shooting range ya ndugu yangu Abdalah Hamis na sio punde
tu nae atalalama kuwa ni kweli 'Nyani haoni ....ule'. Lakini, sitochelea hilo kwasababu huu ndio ukweli na atake aujue!
Anyway, mamilioni kati yetu tunangojea kwa hamu kubwa hio amri itakayotoka on Friday ya ku-march to Lilongwe na kuikomboa 
Malawi baada ya mazungumzo kuwa stalled. Kila mmoja wetu anatakiwa kuzuru blog la ZANZIBAR NI KWETU on 31st August, 2012,
kwani gazeti zima la The Citizen litawekwa hapo kwenye blog kama Wagagagigikoko News Network (WANENE) watafuzu katika
mazungumzo na wamiliki wa gazeti la The Citezen kufanya hivyo hapo yatakapoanza!

/Nkumba.



Posted: 27 Aug 2012 09:30 AM PDT by ZANZIBAR NI KWETU - the only voice of the downtrodden mass in Tanzania!

***Wanaotaka kujua: Ukweli ni huu***
Sensa na Swali la Dini
 Makala hii haina lengo la kuunga mkono au kupinga Waislamu kuhesabiwa bali inalenga kutoa faida za kuuliza swali la dini ya kila muhesabiwa. Ningeomba tusome kwa makini sana ili tuifahamu kadhia hii.

MWAKA 2001 Uingereza iliingiza kwenye sensa swali la Dini. Walifanya hivyo baada ya kufanya utafiti na kusikiliza wananchi wanataka nini, ninamnukuu mwandishi Aspinall anasema "The decision to include the question was made subject to general public support, as assessed in the June 1997 Census Test (97,000 households in Great Britain), the April 1999 Rehearsal (114,800 households in England and Wales), and other public consultation exercises." (Aspinall, 2000).


TARJUMA: Uamuzi wa kuliingiza swali umefanyika baada ya jamii kuliunga mkono, kama ilivyotafitiwa mwezi Juni 1997 katika sensa ya majaribio [Nyumba 97,000 za Great Britain], na zoezi la mwezi April 1999 (Hyumba 114,800 za England na Wales) na mazoezi mengine yaliyofanyika kwenye umma.

Cha kusikitisha sana ni kuwa serikali ya Tanzania inapuuzia wito wa kundi fulani la wananchi juu ya suala sawa na hili. Tena Tanzania tunaambiwa haina Dini, hivyo kimtazamo hili lilikuwa liwe jambo rahisi. Uingereza ni nchi ya Kianglikana, hivyo wangeweza kusema kwamba nchi hii inaendeshwa kianglikana kwa hiyo suala la dini halina maana yoyote, lakini hawakufanya hivyo.

Baadhi ya nukta muhimu za kuzingatia kuhusu kuingiza suala la dini katika sensa.

::::: LESENI ZA BIASHARA ::::::

 Si jambo sahihi kuweka bishara ambayo haiendani na maadili ya jamii au watu wa eneo husika. Moja kati ya kesi maarufu ambayo imewahi kutokea Duniani ni McDonald kuuza nyama ya ng'ombe katika Fast Food za India. Hili lilikuwa ni tusi kwa mabaniani kwani kwao wao Ngo'mbe ni Mungu. McDonald iliomba msamaha na wakaacha mara moja kuuza Beaf Burger (baga za nyama ya ng'ombe) katika maeneo yenye mahindu wengi nchini India. Tafadhali kumbuka kadhia ya mabucha ya nguruwe Dar -es -salaam katika maeneo ya waislamu wengi katika miaka ya tisiini.

Hivyo hii itasaidia serikali kujua ni wapi pakutoa aina fulani ya leseni ya biashara kulingana na dini ya watu wa eneo hilo.


::::::::: NYUMBA ZA IBADA ::::::::

 Ni imani yangu kuwa moja kati ya sababu za kuchomwa makanisa huko Zanzibar ni kuwepo kwa makanisa  katika maeneo yasiyostahiki (hii inahitaji utafiti zaidi) kwa sababu katika maeneo ambayo makanisa yale yalijengwa ni mitaani na ni mitaa yenye waislamu wengi mno kulinganisha na wakristo wenyewe.

Matokeo yake makanisa yamechomwa moto. Tafadhali mimi siungi mkono kuchomwa moto kwa makanisa yale, kitendo kile kilikuwa ni uvunjaji wa sheria, lakini je kujenga makanisa yale katika maeneo yale ilikuwa sahihi?

Moja kati ya kesi maarufu Duniani ni ile ya Waislamu kukataliwa kujenga msikiti katika kiwanja chao kilichopo karibu na Ground zero (New York) na sababu ya msingi ni kwamba wakaazi wa eneo hilo wengi wao ni wakristo halafu bado wana uchungu wa tukio la Septemba 11, hivyo huenda ingepelekea waisalmu kudhuriwa iwapo serikali ingetoa kibali cha kujengwa msikiti ule. Haya ni maamuzi ya busara ambayo yanaepusha matatizo ya baadae, maamuzi haya yanaweza tu kuchukuliwa iwapo serikali inatambua dini za watu wa eneo husika. Hivyo hii inaonyesha umuhimu wa kuuliza dini za wahusika.

:::::::::::: MISREPRESENTATION (KUTOWAKILISHWA) ::::::::::

 Ni utaratibu unaokubalika nchini Tanzania kwamba kila kundi katika umma au jamii linahitaji uwakilishi katika mambo mbali mbali ya kimaendeleo. Bunge la Tanzania hutoa viti maaum vya upendeleo kwa wanawake kwa sababu kuna kutowakilishwa kwa wanawake katika Bunge. Hivyo ni wazi kuwa kila kundi katika jamii lina haki ya kuwakilishwa katika sehemu na ngazi mbali mbali za uongozi na sehemu zinazohusika na maendeleo ya jamii. Ndio maana kunakuwepo na nafasi za upendeleo (positive segregation) ili kuzipa jamii uwakilishi wa haki.

:::::::::::::TENSION ZA UDINI :::::::::::::

 Ni wazi kuwa Tanzania inakabailiwa na tatizo la UDINI. Moja kati ya njia ya kuuvunja udini ilikuwa ni kujenga jamii ambayo kila kundi likapewa haki yake na likajihisi linapata haki zake, kujihisi kuwa umepata haki ni jambo la muhimu kwani Tanzania inaamini kwa < > Yaani haki sio tu itendeke bali pia ionekane kuwa imetendeka. Lakini leo serikali ya Tanzania imekuwa ikipuuza masuala ya UDINI na kudhani suluhu ni kufukia madai na kelele za makundi mbali mbali. Kamwe hili sio suluhisho na ule "uongo" Tanzania haina Dini lakini Watanzania wana Dini ni wazi kuwa haufanyi kazi sasa hivi.

Mwisho ningependa kumnukuu tena Aspinall anasema:
"Information on religions will meet government needs arising from the increasing involvement of faith communities as collaborators in urban regeneration and health improvement. (Aspinall, 2000)
Tarjuma:
<> (Aspinall, 200)

Ndio maana leo Nandos na kampuni nyingi kubwa za vyakula nchini Uingereza vinauza vyakula halali katika miji kama vile Leicester na Birmingham, hii inawanufaisha wananyabishara na pia wananchi kwa vile wanafahamu kuwa hii ni miji yenye Waislamu wengi.

Reference: 
Aspinall, P 2000, 'Should a Question on 'Religion' be Asked in the 2001 British Census? A Public Policy Case in Favour', Social Policy & Administration, 34, 5, pp. 584-600, Academic Search Premier, EBSCOhost, viewed 23 August 2012.

Appendix:
https://www.census.ac.uk/Documents/CensusForms/2001_England_Household.pdf
Hii ni specimen ya fomu halisi ya Population Census ya UK in 2001, angalia ukurasa wa sita swali namba 10, linauliza "What is your religion?" Hivyo Waislamu kudai kuingizwa swali hili sidhani kama ni kiroja kipya katika Population Census.

www.census.ac.uk

Source: Mapara

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment