Timu ya Polisi Tanzania yapokea msaada wa vifaa vya michezo toka NMB
Na Mwandishi Wetu
BENKI ya NMB imekabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya mchezo kwa Timu ya Mpira wa Miguu ya Jeshi la Polisi Tanzania inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.
Vifaa hivyo ni pamoja na mipira, mabegi ya wachezaji, viatu, tracksuit na jezi mbalimbali vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 13, vilikabidhiwa kwa jeshi la polisi na Meneja Mwandamizi wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa NMB - Ally Ngingite kwa Kamishna wa Polisi - Adrian Magayane.
Akizungumza kabla ya kukabidhi vifaa hivyo jana jijini Dar es Salaam, bwana Ngingite alisema NMB inaamini msaada huo kwa Timu ya Jeshi la Polisi utakuwa chachu ya kufanya vizuri zaidi katika michuano mbalimbali iliyopo mbele yao hususani Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara inayotarajia kuanza hivi karibuni.
"Vifaa tunavyokabidhi leo ni pamoja na jezi, track suti, mabegi, mipira, viatu vya kuchezea na vifaa vingine vingi vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 13," alisema bwana Ngingite
Msaada huo kwa timu ya jeshi la polisi ni mwendelezo wa kusaidia kukuza sekta ya michezo nchini huku benki hiyo ikijinasibu kuwa imekuwa mshirika mkubwa sana katima maendeleo ya michezo nchini. Mbali na kuisaidia timu ya polisi, NMB pia inaidhamini timu ya Azam MC ya Ligi Kuu Tanzania Bara na imekuwa ikisaidia timu mbalimbali kuendeleza michezo.
Bwana Ngingite alizitaja timu nyingine ambazo NMB imetia Mkono wake hapa nchini ni pamoja na clabu ya Gofu ya Lugalo, Singida United na Clabu ya jeshi ya Gymkana.
Akiongea baada ya kupokea vifaa hivyo, Kamisha wa Polisi - Adrian Magayane alishukuru kwa msaada na kusema kuwa utaongeza chachu ya ushindi na kuhakikisha kuwa wanatinga ligi kuu msimu ujao.
"Tunawashukuru sana NMB, benki hii imekuwa mshirika wetu mkubwa sana katika nyanja mbalimbali, tunaimani tutabeba nembo yao vizuri kwa kufanya vyema kwenye mashindano ya ligi daraja la kwanza." Alisema Kamishna Magayane.
Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com
Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470
Web:- www.thehabari.com
http://joemushi.blogspot.com
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment