Mambo mawili yaligonga akili zangu:
1) Taasisi ya sekta binafsi Tanzania ikitaka serikali ya Tanzania kuharakisha kuzishika fursa hizo za China kwa manufaa ya Tanzania. Uongozi wa sekta binafsi ulienda mbali kumtaka rais wa Tanzania kuitembelea China ili fursa hizo zisiteleze zikaenda nchi nyingine.
2) Jibu la Serikali kuwa Rais Magufuli ataitembelea China wakati ukifika.
Mambo hayo mawili yalinipa wajibu kutafakari na kutafuta majibu katika mambo matatu:
Moja: Sekta binafsi: Mchango wake katika kutimiza malengo ya taifa na athari za kuikurupukia sekta hiyo.
Mbili: Nini malengo ya China kutaka kujenga viwanda katika nchi nne za Africa.
Tatu: Tanzania inayo mipango ya myaka mia mbele katika harakati zake za kujenga uchumi au inazoa tu kila fursa.
Nimeamua kuandika Makala haya sasa wakati Rais hajaenda China ili kama ikiwezekana akiamua kwenda awe ameamua kwa kutumia hoja mbali mbali zikiwemo za makala haya.
MOJA: Sekta binafsi: Mchango wake katika kutimiza malengo ya taifa na athari za kuikurupukia sekta hiyo:
Sekta binafsi hasa ni wafanyabiashara. Wao huangalia fursa zilizopo na kuziingia na kuzalisha fedha. Sijui kama kuna zaidi. Habari za kulipa kodi ni kwa sababu serikali inatoza kodi. Habari za kusaidia wenye shida ni kwa sababu wana huruma au wanatafuta usalama wao. Hata kama katika kazi zao wanatekeleza baadhi ya malengo ya mipango ya taifa lakini sijui kama ni kusudi lao. Kudhibitisha hilo tuangalie nyuma tuone wafanyabiashara wakubwa walikuwa wanafanya nini na sasa wanafanya nini. Bila ruhusa ya IPP naomba niitolee mfano. Myaka ya 1980 na 90 ungetembelea banda la IPP katika maonyeshjo ya sabasaba unguta banda limejaa bidhaa mbali mbali, kalamu ndefu na za kawaida; madaftari ya shule; sahani na chupa za chai. Ungekumbana na dawa za meno. Katika kipindi hicho IPP alikuwa mshirika wa serikali katika elimu. Sasa siyo ilivyo kwa kutengeneza daftrati na kalamu. Siyo kuwa serikali imeacha elimu. Siyo kuwa haitaki wafanyabiashara kujihusisha na madaftari na kalamu. Mfanyabiashara huyu muhimu amegundua kuwa fursa ziko katika vyombo vya habari zaidi. Hatumlaumu kwa kuamua hivyo. Ndiyo wajibu wake. Na nchi zetu zinazoendelea hatujafikia wafanyabiashara ku-specialize. Mfano kampuni ya Toyota haitakuja kuacha kutengeneza magari na kulima mpunga. Lakini kwa IPP kutelekeza haya na kufanya hayo ni halali. Mchango wake katika kuchangia malengo ya taifa ni katika kulipa kodi na mambo mengine kama hayo. Serikali inahitaji kufikiri mata mbili inapoletewa mapendekezo na taasisi hii.
MBILI: Nini malengo ya China kutaka kujenga viwanda katika nchi nne za Africa.
Naomba wachina wanisamehe kwa hili nitakalosema. Wachina kuleta viwanda Africa yawezekana wanaisaidia Africa kwa sababu inavihitaji viwanda hivyo. Lakini kwao hii si sababu ya msingi. Sababu yao ya msingi ni kupunguza viwanda vinavyochafua mazingira kwao. Kama wakisoma makala hii wakakana, ni sahihi kukana. Wakifanya lolote kuonyesha tofauti ni sahihi. Lakini ukiwapasua myoyo yao ukilikosa hili (la kutafuta pa kujenga viwanda vinavyochafua mazingira kwao); niite kabla hujashona, nikuonyeshe lilikofichika. Viwanda vimechafua nchi hiyo kiasi baadhi ya miji hupiti bila kufunika pua au uso wote. Ukipita unaona moshi umetapakaa kama ukungu hivi. Kwa hiyo katika mpango wao wanafikiri wakipata pa kuzalishia bidhaa zitokanazo na viwanda hivyo itawasaidia. Wamechagua Africa.
TATU: Tanzania inayo mipango ya myaka mia mbele katika harakati zake za kujenga uchumi au inazoa tu kila fursa.
Kuna msemo fulani wa kihaya usemao: 'If you don't know where you are going any way will take you there'. Kwa Kiswahili: "Kama hujui unakokwenda njia yoyote itakufikisha". Katika mpango wa taifa hili wa Muda mfupi yaani 2015- 2025 kuna lengo la kuinua uchumi wa watanzania kufikia uchumi wa kati. Yaani maskini wa Tanzania angalau ajitosheleze kwa chakula, asomeshe watoto wake katika shule za kawaida, awe na akiba Fulani kwa mahitaji ya baadaye. Kama ni mkulima basi atumie technologia ya kawaida isiyomchosha sana. Ili kufikia huko ni muhimu kujennga uchumi wetu katika kujenga viwanda. Viwanda vinatusaidia kuongeza pato la wananchi. Badala ya kuuza pamba tukiuza uzi mkulima wa pamba atafaidika. Tukiuza unga badala ya mahindi mkulima wa Rukwa atafaidika na mengi. Pumba ikibaki shambani kwake ikalisha mifugo atauza unga, kuku, mayai maziwa, nakadhalika. Tunahitaji kuhakikisha kujenga viwanda tunalinda mazingira. Tunahitaji kuhakikisha raslimali madini au mafuta sehemu ya mapato yake inaacha tumepanda misitu ili kuiweka raslimali inayojirudia. Sio kwa sababu tuna ardhi kubwa ya kilimo tuilime yote. Hatutakuwa na akili. Lakini sio kwa sababu tunajenga uchumi wa viwanda basi kila kiwanda tuseme "karibu". Wachina watachekelea na tutatumia fedha za mikopo kusafisha mazingira tuliyoyachafua kijinga.
Serikali kuchelewa kuamua juu ya ziara ya Rais kama ambavyo sekta binafsi ingetaka; na kama ambavyo China ingefurahi ni muhimu kama inayatafakari hayo yote, ili rais akienda China akionyeshwa kiwanda asiseme 'peleka hicho TZ'. Tunahitaji sasa kuwa na uongozi unaoangalia zaidi ya 'Mhula wake'. Rais Magufuli kwa mfano kuangalia Tanzania kama inaisha 2020 au 2025 ni dalili mbaya ya kiongozi asiyefaa. Uzoefu wa nyuma umetuonyesha hivyo kwa hiyo: "Tanzania mpya" inahitaji upya na kwenye misingi na misingi unaweza kuwekwa katika mhula wa uongozi. Kama hii itapunguza spidi ya kujenga wingi wa viwanda, hata kama itaeleweka kwa wachache lakini italifaa taifa letu.
Elisa Muhingo
0767 187 507
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 comments:
Post a Comment