Tuesday, 22 August 2017

Re: [wanabidii] TANZANIA YA VIWANDA: TUTAZOA KAMA DODOKI?

Elisa Mhingo,

Ahsante kwa mchango wako huu. Ila mimi ninahoja nawafanya biashara wa TZ na hiyo TPSF yao.
Kamakweli wapo serious nakuushikauchumi Wachina na Wahindi na wageni wengineo wasije kuushikanakutuchafulia masingira pia-mbona kunaviwanda baadhi yao walipewa hawajavifufua?Kwaufahamu wangu ninaelewa unapopewa kiwanda na hatimiliki unaweza kupata na mkopo. Ndio hao wamejaza ktk magodown magunia ya mitumba ya used clothes, yard ya kiwanda imejaa used cars toka nchi za nje na kuzunguka kuta za kiwanda wamejenga frame za biashara wamepangisha. Badala ya zile chupi za Sunguratex za kutudondoka ukishaifua kwa mara ya kwanza- sasa wanatuagizia chupi za mitumba, vitaulo na mashati labda khanga tu ndio tunapata za hapa.

Kama mchina pekee ni mchafuzi wa mazingira-Mchina alijenga Urafiki Textile miaka ile ya 1965 tena akitumia wafungwa (hawakuzaa wale kipindi kile indentured labourers ambao ni wafungwa wakipigwa sindano na kuvaa sare. Kwa sasa wachina wanazaa na dada zenu/zetu kuwapa makazi mitaani). Angalia urafiki ilivyo. Angalia lile Bwawa la Urafiki la maji machafu ya Kiwanda na ambalo pia ni sewage stabilization pond. Wananchi wamevamia na wanakaa hapo kwenye maji machafu kuna nyumba za makazi na Bar wanakunywa mpaka usiku wa manane. Maji machafu yapo hapo bar ndio wanaona kama wapo beach! Mbu wa matende na mabusha-culex anazaa anawauma na anaambukiza ugonjwa huo usiku tu ila-WAPO hapo uchafuni. Kisha-pamoja na kuvamia maeneo ya maji machafu na taka ngumu kuweka makazi na taka zikichomwa moshi hujaa ndani ya nyumba na madhara ya maeneo ya dampo yanajulikana-TANESCO shirika la wasomi TZ na DAWASA wapo wanawawekea huduma ya Umeme na Maji ya GVT-mchafuzi nani hapa, mjinga nani hapa. Mchina ndio anatufanya tuishi ktk maziongira machafu? Wakilazimiashwa kuondoka au kubomolewa-mnawawekea mawakili-Wanaonewa! Ila electronic waste inavyowaua kwa mwaka angalau watu 5-hakuna Tiba hospitali serikali haijali na hela za kumpeleka mtoto India hatuna!

Bado pita njia ya kwenda kwa wawekezaji locals kuna viwanda na mijengo ya kupaa angani hapo ukitoka Mwenge Mataa kuelekea cocacola-kwenda Msasani unapita huko kwa Mama Rwakatare. Barabara ya Kuelekea IPP pia angalia ilivyo uhalisia, madogo mpaka pembezoni mwa barabara, mauzo ya vyakula mama/baba ntilie barabarani na malori yanatimua mavumbi, mifereji imejaa maji na taka! Hivi wanashindwa kuwajengea vibanda vya biashara hao wauza chakula ambao hutoa huduma kwa wafanyakazi wao. Maji na mashimo yanayofaa maji mvua ikinyesha, malori mazito hutengeneza makorongo! Wanashindwa wazaledo wa viwanda hao kuchanga kuboresha barabara ipitayo malori yao ya mizigo pia? Ingekuwa mchina yupo barabara hiyo ana kiwanda-tungeimba wimbo wa lawama ila ni IPP na wengineo ambao nimatajiri wa bongo.

Waliopimiwa plots za kujenga viwanda wakapewa hati in 1980s huko maeneo ya viwanda Africana wamejenga? Kuna interchick na viwanda vingine vichache. Sehemu kuwa maeneo yapo wazi au wamekodisha wanaotengeneza fanicha au kuna halls za Arusi na Mikutano, Restaurants na vinyweo mbele ya mjengo ambao ndani upo wazi-Tumbua!.

Anayempa Hati Miliki na Kibali TZ Mchina au mwingineyo kujenga Kiwanda ndani ya maeneo ya makazi kinamwaga maji machafu kwa wananchi ktk makazi yao ni nani? Nani anatoa kibali cha biashara kuna bar na halls za sherehe makelele mpaka saa 6 za usiku? Bar na mapishji ya moshi yanayochafua na kuharibu indoor air quality ya nyumba za makazi zilizo na watoto ndani na wajawazito na wagonjwa. Kelele na moshi ni hatarishi, bado maji machafu yatokayo hapo bar na mama ntilie anayepika na kuosha vyombo anamwaga maji machafu barabarani. Wanaokosha magari na kumwaga maji machafu yenye oils na lead barabarani. Wanakosha magari wanaonekana jirani na makazi na wanapokanyaga watu ardhi hiyo. Katikati ya mtaa lkuosha gari na kumwaga maji ya mabishi na wanapika vumbi linaingia ktk chakula, mbuzi na kuku kunywa maji na kudokoa. Kunguru naye utamkuta anawania kuondoka na tonge na kunguru wamejaa mfano hapa DSM-Hewa na mazingira kuchafuka ingawaje levels za uchafuzi za C02 bado ndogo lakini watu tunaugua.

Nenda machimbo ya wachi,baji wadogo wadogo kawaone wanavyochezea zebaki kwa mikondo, kuingiza mitoni tegemewa kwa vyanzo vya maji na kuingiza mercury ktk mito na ziwani zinaingia katika samaki na dagaa, mifugo kunywa maii, majani kuliwa yana zebaki. Tunajimaliza. Ila-serikali ipo kukusanya kodi-Usiowaondoe wapiga Kura wangu-wamejiajiri! Huyu ni mchina na tunaharibu wenyewe na leseni zinatolewa na tunategemea Ushuru huo wa uchafuzi na tunamalengo ya makusanyo kuongezeka? Unatakiwa ukusanye milioni 100 wewe umekusanya milioni moja-Jieleze! Bado utoaji Leseni za Mbao, Mkaa, Magogo wakati leseni inatolewa kwa mtu ambae-Hana Shamba la Miti la kupanda au ya kienyeji anayoilinda na kuivuna sustainably! Ila, wanaweka vizuizi kuona kuwa anayep[ita na mali asili alizovuna ana leseni au kibali. Hawahakikishi kuwa wanampa Leseni kwanza wanakagua kuona Tree plantation yake na kwamba miti imefika umri wa kuvunwa na anavuna sustainably na kuwa wanahamasisha kila raia na kumkagua ana miti aliyopanda kwa matumizi yake. Wale wa mijini wapate mkaa kutoka hao wenye mashamba ya miti. Unatoa kibali cha mkaa na mbao-wanaingia kukata protected forests na kuvuna mashamba ya wengine usiku au mchana wenyewe wakiwa mbali. Kwa nini tulaumu wageni tu? Mchina ndio mchafuzi anahamia kwetu kuchafua!

Hebu pita nje ya majengo makubwa maghorofa mpaka ya serikali uangalie mfereji wa maji machafu nje uone kuna nini. Anzia Tegeta Kibo complez hadi Kariakoo na Azikiwe. Fika kwenye Vyuo uangalie mazingira ya mito, substations za waste collection. Angalia mauzo ya vyakula mitaani na utaona vilivyo wazi na jirani mtu anaranda mbao na nondo anapaka rangi zenye fumes hatarishi. Bwana afya anakagua na Diwani anapita hapo na viongozi wakuu pia.

Mabadiliko ya Tabia Nchi na Athari zake ni wimbo Tanzania na kuna Centre za Climate Change, Masomo ya madogrii, Strategies za Climate change na vikao vya taifa na kimataifa-Leseni za kukata miti zinatolewa; wenye mifugo mingi kupata ruksa ya kuhama hapa kwenda kule na huku wakiharibu ardhi; wakulima wanalima milimani Morogoro, Lushoto na kwingineko bila ya makinga maji. Wanalima hivyo mpaka jirani na vyuo vya Ardhi au Kilimo na unplanned settlements au squatters ziopo mpaka jirani mpaka vyuo vya Ardhi na mito inayochimbwa pia na ujenzi na taka kutupwa mtoni mpaka jirani na vyuo vya ardhi na Maji! Uchafuzi huu unaonekana na Maafisa Mazingira-Wapo! NEMC na Division of Env Ipo lakini fika Mto Ubungo hapo Daraja la Ubungo uone, Mto Mlalakua, fika Ubungo Tanesco kuelekea Kibangu na Fika Tandale kwa Mtogole daraja la kuelekea Kijitonyama-Mbona Universities na Vyuo vya Mazingira, Ardhi, Afya vimejaa DSM-Mfumo wa serikali upo poa multisectoral na kamati zake! Kuwaje mpaka Mitaa iliyopimwa sasa ni chaotic ujenzi holela unakua na wasomi kibao, sera, sheria, mikatati ya sekta ipo poa sana? Tatizo ni nini uchafu na uchafuzi unaendelea?

Tembelea Visiwa vizuri kama Mafia, Kilwa Kisiwani-Majengo kama si UNESCO na wawekezaji wageni yangeishia kuanguka mengi. Bado mengi yameanguka ya historia kubwa. Mbona Matajiri wazawa wapo? Akija mwekezaji mgeni kuyajenga-Kelele nyingi sana. Angalia wanaoingia kujenga ndani ya protected area na tupo kuwatetea! Kwanza lkula na local gvt na maofisa husika, tunawaona wanajenga tunawaachia, wanaishi miaka 5+ mpaka 20 halafu ndio tunashituka leo kuwaondoa kwa nguvu! Anajenga ndani ya jiwe la Mh Magufuli tunamuachia, miaka kumi baadae ndio unambomolea. Bomoa mara anapoanza na Tumbua Ofisa aliyekagua na kumpa Hati. Kapangisha nyumba ya Makazi kafungua Kiwanda. Mwenyenyumba hajui? Anajua-Tumbua!

Kama tunataka kwenda Nchi ya Viwanda bila ya uchafuzi wa Mazingira-Tuzingatie NAPA, UNFCC, Climate Change Strategy, Sera na Sheria kuhusu mazingira. Sheria za Housing Urban and Rural Planning Vitini vipo wa upangaji wa matumizi bora ya Ardhi Mijini na vijijini. Ukiona anaziba feeder road-Bomoa mara. Eneo la wetland la kilimo anajenga nyumba-Bomoa mara tupunguze athari mbaya na mzunguko wa hali ya hewa uwe mzuri.


Viwanda Nchi za Latin America ni vya Waingereza, Wamarekani matajiri. Vinatoa ajira huko na kununua mazao ya mashamba pia wanazalisha. India ni sub-metropolis ya Uingereza sasa wapo mbali wanatuuzia mpaka magari. Sisi mashamba ya katani, pamba, minazi waliopewa local yapo misitu kisha tunalalamika uchumi kushikwa na wageni. Wape wageni Viwanda kama WATAZINGATIA sheria za nchi yetu kuhusu ujenzi wa Kiwanda, Emissions za Hewa, maji na utupaji wa taka ngumu na maji itakiwavyo; kutoa ajira na kununua mazao ya kulisha viwanda yatoke hapa hapa TZ yawe madodoki ya kututakasa umasikini na ujinga wetu. Mwangalie Bakhresa-magari yanakwenda vijijini kununua nazi, maembe etc. Tunataka hiyo sio kuagiza unga wa sodaza rangi na uji wa nyanya wa rangi. Mwekezaji local na hii TPSF wazingatie-wawe na extesion staff wa kufanikisha kilimo na uzalishaji bora wa mazao watakayo nunua kutoka wakulima, wafugaji na kuelimisha wavuvu, wafugaji samaki mabwawani ili kupungura uwepo wa kemikali ktk mazao ili yakiuzwa nje ya nchi yasikataliwe kuwa yana residuals nyingi za kemikali. Mwekezaji gani local ameajiri extension staff wapo Kata na makabi vijijini wanakolima heavily mazao ya bustani kulisha viwanda vyao? Ni matikiti, mbaazi, nyanya, kunde, njegele kulimwa kienyeji bila tya support ya TPSF kusema ina planattions heavy kwa wakulima Dodoma, Iringa, Dumila etc-Labda wapo mimi sipo informed ni dodoki tu.


Waje tu Wachina na Wawekezaji wengine. Kwa sasa Wachina Wanatuzalisha ile mbaya hati miliki ya kubaki nakuishi TZ na kumiliki mali!

Tuwaache matajiri wetu locals na miashara zao za mabasi ya abiria, malori ya kubeba mizigo na magunia ya mkaa na mbao (Maghembe yupo kukamata malori yanayobeba mali asili na Mwigulu kufirisi na kuuza malori yanayobeba wahamiaji haram) ambayo ndio wanaona uzalishaji mali pamoja na kuuza soda za rangi kutujazia chupa za plastiki mitaani kila kona na mifuko ya plastiki. Ya viroba sasa imepungua. Utajiri wa kuuza meno ya tembo na ukiwafuatilia wanakuua au wanakuanzishia mauaji Kibiti. Huyo ndio Mbongo/Mtanzania anayedai kuwa Nchi ya viwanda itatukomboa. Lakini kubadilika akili hataki kufanya maendeleo yanayostahili kisheria, kijamii kuwafaisisha na kimazingira. Kaangalie maeneo ya uchimbaji madini uone kupoje-kichefuchefu! Angalia mashamba ya katani yalivyo na katani na miti/machaka manene! Anza kuangalia kuanzia Chalinze Mpaka unaimaliza Morogorona Kilosa pia! Hao ndio investors Watanzania!!

Mimi huu uwekezaji na matajiri wetu kumiliki uchumi na sisi wabongo kulinda na kuacha uharibifu na uchafuzi wa mazingira na kuharibu mali asili zetu inaniumiza ninaweza kuandika mpaka kesho! Kaangalie wanavyochimba hovyo alrdhi Lindi ktk kupeleka mawe kwa Dangote. Angalia wanavyouza ardhi mijinikama DSM na kuhamia mashimo ya kuchimba mawe. Angalia wanavyouza kariakoo, magomeni, Ilala na kuhamia mabondeni ktk mazingira machafu; mashamba ya miembe, minazi, mikorosho yanavyogeuka kuwa maeneo ya bar na lodges na kaya kukosa maeneo ya kilimo na kuvamia ya umma. Hata waliovamia ya Wazo na ya Sumaye-watauza tu kama walivyofanya wale waliopewa Mabwepande baada ya kuondolewa Hananasif-Kinondoni Mkwajuni au wale wa kwingineko Tanzania wanauza maeneo hela kulewea pombe na kisha kuvamia kwingine moaka kwa wawekezaji na wengineo wenye hati miliki! Tumbua tabia hii mbaya ili tuwe na nidhamu wa utii wa sheria.

Nakwerwa na mengi naweza kuandika mpaka kesho.

Kama Kawa.

--------------------------------------------
On Tue, 22/8/17, 'ELISA MUHINGO' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com> wrote:

Subject: [wanabidii] TANZANIA YA VIWANDA: TUTAZOA KAMA DODOKI?
To: "prudence karugendo" <prudencekarugendo@yahoo.com>, "hussein siyovelwa" <uhalisi@yahoo.co.uk>, "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Cc: "stanley.nshange@nsn.com" <stanley.nshange@nsn.com>, "innokahwa@yahoo.com" <innokahwa@yahoo.com>, "akiobya@yahoo.com" <akiobya@yahoo.com>, "tkiobya@yahoo.com" <tkiobya@yahoo.com>, "hkahyoza@yahoo.com" <hkahyoza@yahoo.com>, "emmanuelelias2005@yahoo.com" <emmanuelelias2005@yahoo.com>, "repeatitagency@yahoo.com" <repeatitagency@yahoo.com>, "stanley.nshange@nokia.com" <stanley.nshange@nokia.com>, "tundu.lissu@gmail.com" <tundu.lissu@gmail.com>, "pkarugendo@yahoo.com" <pkarugendo@yahoo.com>, "mbowe2008@gmail.com" <mbowe2008@gmail.com>, "bilhuda2006@yahoo.co.uk" <bilhuda2006@yahoo.co.uk>, "davidkafulila@yahoo.com" <davidkafulila@yahoo.com>, "muddy.kiobya@gmail.com" <muddy.kiobya@gmail.com>, "emmanuelelisa46@yahoo.com" <emmanuelelisa46@yahoo.com>, "wilfredlwakatare@gmail.com" <wilfredlwakatare@gmail.com>
Date: Tuesday, 22 August, 2017, 16:10



Wiki chache zilizopita kulifanyika mkutano
uliowahusisha wafanya
biashara wa Tanzania na China. Nikikumbuka vizuri ulilenga
kuisaidia Tanzania
kuziona fursa zilizoko China sasa, hasa kusudi lake la
kujenga viwanda katika
nchi nne za kiafrika Tanzania ikiwa mojawapo.

Mambo
mawili yaligonga akili zangu:

1)     
Taasisi
ya sekta binafsi Tanzania ikitaka serikali ya Tanzania
kuharakisha kuzishika
fursa hizo za China kwa manufaa ya Tanzania. Uongozi wa
sekta binafsi ulienda
mbali kumtaka rais wa Tanzania kuitembelea China ili fursa
hizo zisiteleze
zikaenda nchi nyingine.

2)     
Jibu
la Serikali kuwa Rais Magufuli ataitembelea China wakati
ukifika.

 

Mambo
hayo mawili yalinipa wajibu kutafakari na kutafuta majibu
katika
mambo matatu:

Moja:
Sekta binafsi:
Mchango wake katika kutimiza malengo ya taifa na athari za
kuikurupukia sekta
hiyo.

Mbili:
Nini malengo ya
China kutaka kujenga viwanda katika nchi nne za
Africa.

Tatu:
Tanzania inayo mipango
ya myaka mia mbele katika harakati zake za kujenga uchumi au
inazoa tu kila
fursa.

 

Nimeamua
kuandika Makala haya sasa wakati Rais hajaenda China ili
kama
ikiwezekana akiamua kwenda awe ameamua kwa kutumia hoja
mbali mbali zikiwemo za
makala haya.

 

MOJA:
Sekta binafsi: Mchango
wake katika kutimiza malengo ya taifa na athari za
kuikurupukia sekta hiyo:

Sekta
binafsi hasa ni wafanyabiashara. Wao huangalia fursa
zilizopo na
kuziingia na kuzalisha fedha. Sijui kama kuna zaidi. Habari
za kulipa kodi ni
kwa sababu serikali inatoza kodi. Habari za kusaidia wenye
shida ni kwa sababu
wana huruma au wanatafuta usalama wao. Hata kama katika kazi
zao wanatekeleza
baadhi ya malengo ya mipango ya taifa lakini sijui kama ni
kusudi lao. Kudhibitisha
hilo tuangalie nyuma tuone wafanyabiashara wakubwa walikuwa
wanafanya nini na
sasa wanafanya nini. Bila ruhusa ya IPP naomba niitolee
mfano. Myaka ya 1980 na
90 ungetembelea banda la IPP katika maonyeshjo ya sabasaba
unguta banda limejaa
bidhaa mbali mbali, kalamu ndefu na za kawaida; madaftari ya
shule; sahani na
chupa za chai. Ungekumbana na dawa za meno. Katika kipindi
hicho IPP alikuwa
mshirika wa serikali katika elimu. Sasa siyo ilivyo kwa
kutengeneza daftrati na
kalamu. Siyo kuwa serikali imeacha elimu. Siyo kuwa haitaki
wafanyabiashara
kujihusisha na madaftari na kalamu. Mfanyabiashara huyu
muhimu amegundua kuwa
fursa ziko katika vyombo vya habari zaidi. Hatumlaumu kwa
kuamua hivyo. Ndiyo
wajibu wake. Na nchi zetu zinazoendelea hatujafikia
wafanyabiashara
ku-specialize. Mfano kampuni ya Toyota haitakuja kuacha
kutengeneza magari na
kulima mpunga. Lakini kwa IPP kutelekeza haya na kufanya
hayo ni halali.
Mchango wake katika kuchangia malengo ya taifa ni katika
kulipa kodi na mambo
mengine kama hayo. Serikali inahitaji kufikiri mata mbili
inapoletewa
mapendekezo na taasisi hii.

 

MBILI:
Nini malengo ya China
kutaka kujenga viwanda katika nchi nne za Africa.

Naomba
wachina wanisamehe kwa hili nitakalosema. Wachina kuleta
viwanda Africa yawezekana wanaisaidia Africa kwa sababu
inavihitaji viwanda
hivyo. Lakini kwao hii si sababu ya msingi. Sababu
yao ya msingi ni kupunguza viwanda vinavyochafua mazingira
kwao.
Kama wakisoma makala hii wakakana, ni sahihi kukana.
Wakifanya lolote kuonyesha
tofauti ni sahihi. Lakini ukiwapasua myoyo yao ukilikosa
hili (la kutafuta pa
kujenga viwanda vinavyochafua mazingira kwao); niite kabla
hujashona,
nikuonyeshe lilikofichika. Viwanda vimechafua nchi hiyo
kiasi baadhi ya miji
hupiti bila kufunika pua au uso wote. Ukipita unaona moshi
umetapakaa kama
ukungu hivi. Kwa hiyo katika mpango wao wanafikiri wakipata
pa kuzalishia
bidhaa zitokanazo na viwanda hivyo itawasaidia. Wamechagua
Africa.

 

TATU:
Tanzania inayo mipango ya
myaka mia mbele katika harakati zake za kujenga uchumi au
inazoa tu kila fursa.

Kuna
msemo fulani wa kihaya usemao: 'If you don't know where
you are
going any way will take you there'. Kwa Kiswahili: "Kama
hujui unakokwenda njia
yoyote itakufikisha". Katika mpango wa taifa hili wa Muda
mfupi yaani 2015-
2025 kuna lengo la kuinua uchumi wa watanzania kufikia
uchumi wa kati. Yaani
maskini wa Tanzania angalau ajitosheleze kwa chakula,
asomeshe watoto wake
katika shule za kawaida, awe na akiba Fulani kwa mahitaji ya
baadaye. Kama ni
mkulima basi atumie technologia ya kawaida isiyomchosha
sana. Ili kufikia huko
ni muhimu kujennga uchumi wetu katika kujenga viwanda.
Viwanda vinatusaidia
kuongeza pato la wananchi. Badala ya kuuza pamba tukiuza uzi
mkulima wa pamba
atafaidika. Tukiuza unga badala ya mahindi mkulima wa Rukwa
atafaidika na
mengi. Pumba ikibaki shambani kwake ikalisha mifugo atauza
unga, kuku, mayai maziwa,
nakadhalika. Tunahitaji kuhakikisha kujenga viwanda
tunalinda mazingira.
Tunahitaji kuhakikisha raslimali madini au mafuta sehemu ya
mapato yake inaacha
tumepanda misitu ili kuiweka raslimali inayojirudia. Sio kwa
sababu tuna ardhi
kubwa ya kilimo tuilime yote. Hatutakuwa na akili. Lakini
sio kwa sababu
tunajenga uchumi wa viwanda basi kila kiwanda tuseme
"karibu". Wachina
watachekelea na tutatumia fedha za mikopo kusafisha
mazingira tuliyoyachafua
kijinga.

 

Serikali
kuchelewa kuamua juu ya ziara ya Rais kama ambavyo sekta
binafsi ingetaka; na kama ambavyo China ingefurahi ni muhimu
kama inayatafakari
hayo yote, ili rais akienda China akionyeshwa kiwanda
asiseme 'peleka hicho
TZ'. Tunahitaji sasa kuwa na uongozi unaoangalia zaidi ya
'Mhula wake'. Rais Magufuli
kwa mfano kuangalia Tanzania kama inaisha 2020 au 2025 ni
dalili mbaya ya
kiongozi asiyefaa. Uzoefu wa nyuma umetuonyesha hivyo kwa
hiyo: "Tanzania mpya"
inahitaji upya na kwenye misingi na misingi unaweza kuwekwa
katika mhula wa
uongozi. Kama hii itapunguza spidi ya kujenga wingi wa
viwanda, hata kama
itaeleweka kwa wachache lakini italifaa taifa letu.

Elisa
Muhingo

0767
187 507

elisamuhingo@yahoo.com

 










Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and
Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
























--

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

 

Kujiondoa Tuma Email kwenda

wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

 

Disclaimer:

Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

---

You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.

To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.

For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

0 comments:

Post a Comment