Tuesday, 29 August 2017

Re: [wanabidii] Kumbe Lissu alishawahi kuinanga IMMMA Advocates bungeni, alidai ilitumika kuanzisha makampuni yaliyochota fedha za EPA

Kumbe?! Hata hivyo kipindi kile wizi na hasa kuibia umma ndio ulikuwa mtindo. Hata hivyo kumbe IMMMA ni kampuni ya kutiliwa shaka. ubaya wa kuipiga mabomu kunaweza kutusaidia kuijua zaidi kuliko tulivyoijua 2013



From: fadhil fadhil <fadhil.fadhil96@gmail.com>
To: 'Hildegarda Kiwasila' via Wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Monday, August 28, 2017 9:13 AM
Subject: [wanabidii] Kumbe Lissu alishawahi kuinanga IMMMA Advocates bungeni, alidai ilitumika kuanzisha makampuni yaliyochota fedha za EPA

Julai 13, 2012 Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni iliwasilisha maoni yake kuhusu Mpango na Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha wa 2012/2013.

Pamoja na mambo mengine, maoni hayo ya Kambi Rasmi ya Upinzani yaliyowasilishwa na Msemaji wa Wizara ya Katiba na Sheria, Tundu Lissu, yalikosoa utaratibu wa uteuzi wa majaji wa Mahakama ya Tanzania.
Lissu alieleza kwa kirefu uteuzi huo, na kwenye aya kadhaa, alimgusa pia Jaji Mujulizi.

Alisema: "Jaji Aloysius Mujulizi alikuwa miongoni mwa watu ishirini walioteuliwa Majaji wa Mahakama Kuu mwezi Februari, 2006. Kabla ya uteuzi wake, Jaji Mujulizi alikuwa wakili wa kujitegemea katika kampuni ya mawakili ya Ishengoma, Masha, Magai & Mujulizi Advocates (IMMMA) ya Dar es Salaam.

Kampuni hii ya mawakili ndiyo iliyoshiriki katika kuanzishwa kwa kampuni iitwayo Deep Green Finance Co. Ltd. mnamo tarehe 18 Machi 2004. IMMMA Advocates vile vile walikuwa mawakili wa TANGOLD LTD.

"Makampuni haya mawili yanatuhumiwa kutumika kupitishia mabilioni ya fedha zilizoibiwa Benki Kuu ya Tanzania kati ya mwaka 2005 na 2006. Kwa mfano, katika kipindi kifupi cha miezi minne kati ya Agosti 1 na Desemba 10, 2005 kampuni ya Deep Green Finance ilipokea jumla ya shilingi 10,484,005,815.39 kutoka akaunti ya kulipia madeni ya nje (EPA) iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania.

"Katika kipindi hicho hicho, kampuni ya TANGOLD LTD. ililipwa dola za Marekani 13,736,628.73 kutoka kwenye akaunti hiyo ya EPA. Nyaraka zilizowasilishwa BRELA na mawakili wa IMMMA Advocates na kusainiwa na Gavana wa Benki Kuu wa wakati huo Daudi Ballali tarehe 20 Mei 2005 zinaonyesha kwamba TANGOLD LTD ilikuwa kampuni ya kigeni kutoka Jamhuri ya Mauritius. Haya yote yalitokea wakati Jaji Mujulizi akiwa wakili mwenza wa IMMMA Advocates."

HII NIMEIKUTA KWENYE GAZETI LA JAMHURI LA MAY 24,2017,NIMECHUKUA KIPENGELE HIKI UNAWEZA SOMA THE REST OF STORY HAPAUtata wa Jaji Aloysius Mujulizi | Gazeti la Jamhuri

sorce jf

Virus-free. www.avast.com
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.


0 comments:

Post a Comment